Mada za sehemu hiiMatumizi Ya SarufiMada 7
-
Dhana ya sarufi ya lugha imefafanuliwa na wataalamu mbalimbali wa sarufi.
-
Mtaalamu James Salehe Mdee (1999) anafafanua maana ya sarufi kuwa ni mfumo wa kanuni za lugha zinazomwezesha mzungumzaji kutunga sentensi sahihi na zenye kukubaliwa na wazawa wa lugha.
- Kanuni hizi hujitokeza katika lugha ya mzawa wa lugha inayohusika ambaye anaifahamu barabara lugha yake.
- Sarufi inajumuisha mfumo wa sauti, maumbo ya maneno, muundo, na maana.
-
Mtaalamu Mbundo Msokile (1992) na Khamisi (1978) wanasema sarufi ni mfumo wa taratibu na kanuni zinazotawala matumizi sahihi ya:
- Matamshi,
- Maumbo ya maneno,
- Miundo ya tungo,
- Maanda ya miundo ya lugha.
- Ni mfumo wa taratibu zinazomwezesha mzungumzaji wa lugha kutoa tungo sahihi.
- Inamwezesha mtu yeyote anayezungumza kuelewa tungo zinazotolewa na mtu mwingine anayetuma lugha hiyo hiyo.
-
Nkwera (1978) anasema sarufi ni utaratibu wa kanuni zinazomwezesha mzawa au mtumiaji yeyote wa lugha kuelewa tungo zinazotolewa na mtu mwingine anayetunza lugha hiyo hiyo.
- Kufafanua na kuzielewa kwa undani tungo mbalimbali zitumikazo katika lugha hiyo pamoja na kutoa tungo sahihi na zinazoeleweka.
-
Kwa ujumla, maana zote zilizotolewa na wataalamu wote ni sahihi.
-
Tunaweza kuhitimisha kuwa sarufi ni kanuni, sheria au taratibu zinazotawala lugha katika viwango vyote vya uchambuzi wa lugha:
- Kiwango cha sarufi matamshi (fonolojia),
- Sarufi maumbo (mofolojia),
- Sarufi miundo (sintaksia),
- Sarufi maana (semantiki).
Ujumla, sarufi inaweza kugawanywa katika aina kuu zifuatazo:
-
Sauti katika lugha: jinsi ambavyo vitamkwa au sauti za lugha zinavyoungana ili kujenga maneno yanayokubalika katika lugha husika.
-
Sarufi matamshi hujishughulisha na uchambuzi wa sauti zilizomo katika lugha, namna zinavyotamkwa, mahali zinapotamkwa, na namna sauti hizo zinavyopangwa ili kujenga maneno ya lugha fulani.
-
Lugha mbili tofauti zinaweza kuwa na sauti zinazofanana lakini zikatofautiana katika utaratibu wa kuzipanga sauti hizo.
-
Kila lugha ina utaratibu wake wa mpangilio wa sauti ili kujenga ama mofimu, silabi au maneno.
-
Sauti zitumikazo katika lugha zinaweza kugawanywa katika makundi mawili:
- Irabu: mfano a, e, i, o, u.
- Kansonati: mfano k, g, ch, i, d.
Fonimu ni kipashio kidogo kabisa cha kifonolojia, ni kitamkwa cha msingi cha kifonolojia kinachobadili maana ya neno.
- Fonimu ni kipashio kidogo kabisa cha kifonolojia, ni kitamkwa cha msingi cha kifonolojia kinachobadili maana ya neno.
- K, P, B ni fonimu kwani ndio zinafanya maneno hayo kutofautiana kimaana.
- T na g ni fonimu zinazofanya maneno haya kutofautiana kimaana.
- Irabu na konsonanti zinapotumika katika lugha huitwa alfabeti.
- Irabu ni sauti za lugha ambazo hutamkwa bila kuwepo kwa kizuizi chochote kwenye mkondo wa hewa utokao mapafuni kwenda nje kupitia chemba ya kinywa na pua.
- Irabu hutolewa kwa mrindimo wa ujenzi sauti Irabu hutolewa kwa kutumia mlingano wa sauti fulani na maumbo ya kifonolojia katika mchakato wa kutamka maneno. Hii ina maana kuwa, irabu hutolewa kwa njia ya mitindo ya ujenzi wa sauti zinazozunguka katika midundo ya neno.
- Irabu zinapotamkwa midomo ya mtamkaji huviringwa na kutandazwa Irabu zinapotamkwa, midomo ya mtamkaji inashiriki katika kutengeneza sauti hizo. Sauti hizi huviringwa na kutandazwa kulingana na mkao wa midomo ya mtamkaji, ambayo inaweza kuwa wazi au fupi, kuendana na maumbile ya irabu husika.
- Utamkaji wa sauti hizi utegemea mkao wa ulimi katika chemba ya kinywa Irabu zinatamkwa kulingana na mkao wa ulimi katika chemba ya kinywa. Mkao huu unaweza kuwa juu au chini, mbele au nyuma, na hivyo kuathiri sauti inayotolewa. Ulimi husogea kwenye sehemu tofauti za mdomo ili kutoa irabu zenye sifa maalum.
- Irabu huchukua muda mrefu na ni wazi katika sauti Irabu ni sauti ambazo hutolewa kwa muda mrefu, tofauti na konsonanti ambazo hutolewa kwa muda mfupi. Hii inafanya irabu kuwa sauti wazi na rahisi kutofautishwa.
- Irabu zinaweza kuwa za vifonolojia tofauti kulingana na lugha Katika lugha mbalimbali, irabu zinaweza kuwa na tofauti katika fonolojia. Hii ina maana kwamba sauti ya irabu katika Kiswahili inaweza kutofautiana na sauti ya irabu katika lugha nyingine, kulingana na muktadha wa kimaumbo na kimatamshi.
Ni sauti ambazo hutamkwa kwa kuzuia mkondo wa hewa katika sehemu mbalimbali kinywani hasa kwa kutumia ulimi.
- Konsonanti ghuna: ni zile ambazo hutamkwa zikiwa na mrindimo mkubwa wa nyuzi sauti
- Konsonanti zisizosighuna (sighuna): ni zile ambazo hutamkwa zikiwa na mrindimo mdogo wa sauti Katika Kiswahili sanifu, kuna konsonanti 23 na viyeyusho viwili hizo ni b, ch, d, dh, f, g gh, j, k, l, m, n, h, ny, ng, p, r, s, sh, t, th, v, z. Na viyeyusha viwili ambavyo ni :
Ni kitamkwa au sehemu ya neno ambayo hutamkwa mara moja na kwa pamoja kama sehemu ya fungu moja la sauti. Silabi zinagawanyika katika makundi mawili:
- Silabi funge
- Silabi humo
- Silabi funge Ni silabi zinazoishia na konsonanti
Ni kitamkwa katika lugha (sauti katika lugha)
Ni vitamkwa tofauti yaani sauti zinabadili maana ya neno. Mfano

Bh na b ni alafoni zinazobadili maana ya neno.
-
Sarufi maumbo hujishughulisha na namna maneno ya aina mbalimbali yanavyoundwa katika lugha.
-
Maneno katika lugha hujengwa kwa kuunganisha vipengele vidogo vya maneno ambavyo hubeba dhana mbalimbali kama vile nafsi, wakati, wingi, umoja, uyakinishi na kauli mbalimbali n.k.
-
Vipande hivi vidogo vya maneno vijengavyo neno hufahamika kama mofimu. Katika kila lugha kuna utaratibu wake wa kuzipanga mofimu ili kujenga maneno yenye maana katika lugha husika.
-
Kwa kawaida, mofimu hupangwa kwa kufuata utaratibu maalumu. Utaratibu huu hujengwa kama utaratibu wa mpangilio kwa kufuata kanuni.
-
Huu utaratibu wa mpangilio wa mofimu usipofuata maumbo ya maneno yasiyokuwa na maana, yaani yaliyokataliwa na wazawa wa lugha husika, basi maneno hayatakuwa na maana.
-
Mfano:
-
Katika lugha ya Kiswahili, mofimu za umoja na wingi katika nomino huwekwa mwanzoni. Huu utaratibu haukubaliki katika lugha ya Kiingereza, ambapo mofimu za umoja na wingi huwekwa mwishoni mwa nomino:
- Boy – boys
- Girl – girls
- Idea – ideas
-
-
N.B: Kwa ujumla, sarufi maumbo (mofolojia) hujishughulisha na jinsi ambavyo mofimu mbalimbali zinavyoungana ili kujenga maneno yatumikayo katika lugha. Kipashio cha msingi katika mofolojia ya lugha ni mofimu.
- Uchunguzi wa mpangilio wa maneno katika sentensi na uhusiano wa maneno hayo. Sintaksia huchunguza sheria au kanuni zinazofuatwa katika kuyapanga maneno ya lugha.
- Mpangilio wa neno moja baada ya jingine hufanyika kwa namna ambayo itayafanya maneno hayo yalete maana inayokubalika katika lugha inayohusika.
- Wakati mwingine mpangilio wa maneno unaweza kuwa sahihi na kuunda utaratibu, lakini ukazalisha tungo zisizo na maana. Hii inaweza kutokea katika mpangilio wa maneno wenye kuleta maana.
- N.B: Katika lugha ya Kiswahili, kanuni kubwa ya kisintaksiani ni ile inayosema, kila sentensi iliyo sahihi na yenye kukubalika kwa wazao wa lugha ya Kiswahili sharti iwe na muundo wa kiima na kiarifu au kikundi nomino na kikundi kitenzi.
- Tawi hili la sarufi huchunguza maana inayoonekana wazi na maana iliyofichika. Huchunguza muundo wa tungo ili kupata maana iliyofichika.
- Katika lugha, kila neno au tungo huwa na maana yake.
- Mfano: "Mtoto amelalia uji." Neno "amelalia" kama lilivyotumika, katika sentensi hii halina maana moja, hivyo kuifanya sentensi hiyo kuwa na maana zaidi ya moja. Mara nyingi, maana ya neno hutegemea matumizi ya neno katika muktadha fulani.
- N.B.: Lugha inaweza kufanya kazi sawasawa ikiwa taratibu na kanuni za lugha husika zimefuatwa. Taratibu hizi ni zile zinazohusu matamshi, maumbo, muundo, na maana. Taratibu hizi ndizo humwezesha mzawa au mtumiaji yeyote wa lugha kutoa tungo sahihi na zinazoeleweka kwa matumizi mengine ya lugha na kuelewa tungo zinazokataliwa na watumiaji wengine wanaotumia lugha hiyo hiyo.
-
Lugha hujengwa na vipashio mbalimbali ambavyo vinatabia ya kujengana, yaani vipashio vidogo huungana kujenga vipashio vikubwa zaidi.
-
Lugha ina vipashio vikuu vitano:
- Mofimu
- Neno
- Kirai
- Kishazi
- Sentensi
-
Vipashio hivi wakati mwingine hufahamika kama tungo. Isipokuwa kipashio kidogo kwa vingine vyote katika lugha ni mofimu na kipashio kikubwa kuliko vingine vyote ni sentensi.
-
Vipashio vyote katika lugha vina muundo maalum unaoonesha jinsi vinavyojenga vipashio vikubwa, isipokuwa mofimu.
Mwalimu
Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.
Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.
Ingia ili kuuliza