Mada za sehemu hiiMatumizi Ya SarufiMada 7
Sentensi
- Sentensi ni kifungu cha maneno kinachoanzia neno moja na kuendelea lakini chenye muundo wa kiima na kiarifu au kikundi nomino na kikundi kitenzi.
- N.B: Sentensi ndiyo tungo kubwa kuliko tungo nyingine zote katika mpangilio wa tungo.
- Sentensi ina sehemu kuu mbili (2):
- Sentensi ikigawanywa kwa kutumia kigezo cha kidhima ina sehemu kuu mbili ambazo ni KIIMA na KIARIFU.
- Sentensi ikigawanywa kwa kuangalia muundo wa sentensi basi sentensi hugawanywa katika sehemu kuu mbili yaani KIKUNDI NOMINO na KIKUNDI KITENZI.
- Mgawanyo huu hutokana na kanuni kuu ya kisintaksia ambayo hudai kila sentensi iliyosahihi na inayokubaliwa na wazawa wa lugha ya Kiswahili ni lazima iwe na muundo wa kiima na kiarifu au kikundi nomino na kikundi kitenzi.
- Kiima hutaja mtenda au mtendwa wa jambo na kiarifu huarifu jambo linalotendwa na kiima au alilotendwa na kiima.
- Mfano: Juma anacheza mpira. Juma ni kiima (mtendwa) na kiarifu ni anacheza mpira.
- Hapa pia nomino mpira ndiyo kiima, lakini kiima hiki kinataja kile kinachotendwa, yaani mpira.
- Kiima ni sehemu ya sentensi ambayo hujaza nafasi ya mtenda au mtendwa katika sentensi.
- N.B: Aghalabu kiima hutokea upande wa kushoto wa kitenzi.
- Mfano: Mwalimu anafundisha wanafunzi.
- Kwa kawaida kiima hukaliwa na jina au kikundi jina ambalo hujaza nafasi ya mtenda au mtendwa katika sentensi.
Kiima kinajengwa na vipashio vifuatavyo:
- Jina peke yake
- Mfano: Mwalimu anafundisha wanafunzi.
- Jina na Jina
- Mfano: Baba na mama wanakula.
- Jina na kivumishi
- Mfano: Mtoto mzuri amepewa zawadi.
- Kivumishi na jina
- Mfano: Yule mwizi amekamatwa.
- Kiswahili peke yake
- Mfano: Wewe ni mzembe.
- Kiwakilishi na kivumishi
- Mfano: Yule mzembe amefukuzwa.
- Kitenzi jina na jina
- Mfano: Kulia kwa mtoto kunasikitisha.
- Kitenzi jina na kivumishi
- Mfano: Kuimba na kucheza kwake kunafurahisha.
- Jina na kishazi tegemezi kivumishi
- Mfano: Mtoto aliyepotea ameupata leo asubuhi.
- Kivumishi nomino kivumishi na Bv
- Mfano: Yule mtoto uliyemuona jana ni mwanafunzi.
- Hii ni sehemu muhimu zaidi katika sentensi na wakati mwingine huweza kusimama peke yake bila kiima kwa kuwa hubeba viwakilishi vya kiima.
- Kiarifu ni sehemu katika sentensi ambayo hukaliwa na maneno ambayo huarifu tendo lililofanywa, linalofanywa au litakalofanywa na kiima.
- Mfano: Mwalimu anafundisha wanafunzi darasani.
- Kitenzi kikuu peke yake
- Mfano: Mtoto anacheza.
- Kitenzi kisaidizi au visaidizi vilivyo sambamba na kitenzi kikuu
- Mfano: Mtoto alikuwa anataka kucheza.
- Kitenzi kishirikishi na shamirisho
- Mfano: Watoto wanacheza uwanjani.
- Kitenzi kikuu na chagizo
- Mfano: Watoto wanacheza uwanjani vizuri.
- Kitenzi kikuu shamirisho na chagizo
- Mfano: Mwalimu anafundisha wanafunzi darasani.
- Kitenzi kisaidizi kikuu na shamirisho
- Mfano: Mwalimu alikuwa anafundisha wanafunzi wengi.
- Kitenzi kisaidizi kikuu na chagizo
- Mfano: Mwalimu alikuwa anafundisha darasani.
- Vitenzi visaidizi kikuu, shamirisho na chagizo
- Mfano: Mzazi alikuwa anataka kuwarudisha watoto wake nyumbani.
- Shamirisho ni jina au kikundi jina (kirai nomino) kinachojaza nafasi ya mtendwa au mtenda, mtendwa katika sentensi.
- Shamirisho hutokea baada ya kitenzi kikuu au kitenzi kishirikishi katika sentensi, na hujibu maswali: Mtenda amemtenda nani? Au mtendwa ametendewa nini?
- Mfano: Wanafunzi wanasoma vitabu.
- Mfano: Juma alimimisomea Asha kitabu.
- Chagizo ni sehemu ya sentensi ambayo hutokea upande wa kiarifu na huwa na neno au kikundi cha maneno ambacho hujaza nafasi ya kielezi.
- Mfano: Mama ameenda nyumbani.
- Mfano: Mtoto anacheza mpira vizuri sana.
- N.B: Chagizo huweza kutokea mara baada ya kitenzi kikuu au mara baada ya shamirisho.
Kuna aina kuu nne za sentensi:
- Sentensi sahili/huru.
- Sentensi shurutia.
- Sentensi ambatano.
- Sentensi changamano.
Hii ni aina ya sentensi ambayo hutawaliwa na kishazi huru.
- Mfano: Juma ni mzembe.
- Mfano: Juma alikuwa mzembe sana.
- Mfano: Mwalimu alikuwa anafundisha darasani.
Miundo ya sentensi huru/sahili
- Muundo wa kitenzi kikuu peke yake (tawaliwa):
- Mfano: Wanacheza, Alinipiga, Wanasoma.
- Muundo wa kitenzi na kitenzi kikuu:
- Mfano: Alikuwa anasoma, Walikuwa wanataka kufundishwa.
- Muundo wa kirai na kirai kitenzi:
- Mfano: Mwalimu anafundisha, Wanafunzi wanamsikiliza.
- Muundo wa virai nomino na virai kitenzi vinaambatana na vijalizo:
- Mfano: Baba yangu alinunua machungwa mawili usiku.
Sifa za sentensi sahili/huru
- Inakiima ambacho kinaweza kutajwa wazi au kisitajwe kama kinaeleweka.
- Inakiungo ambacho kinaunda kitenzi kikuu kimoja au kitenzi kiuu na kitenzi kisaidizi au kitenzi kuku na shamirisho na chagizo.
- Haifungamani na sentensi nyingine na inajitosheleza kimuundo na kimaana.
- Kuchanganua sentensi ni kitendo au mbinu ya kuitenga au kuigawa sentensi katika sehemu mbalimbali ambazo hujenga au kuiunda sentensi hiyo.
- Kuna mikabala mikuu miwili ya uchanganuzi wa sentensi:
- Kwa kutumia mkabala wa kimapokeo ambapo sentensi hugawanywa katika kiima na kiarifu na baadaye hufuatiwa na vipashio vinavyojenga kiima na kiarifu.
Mkabala wa kimuundo/kisasa
Huu ni mbinu ambapo sentensi hugawanywa katika sehemu kuu mbili, yaani kirai nomino na kirai kitenzi, kisha hufuatiwa na vipashio vijengavyo kirai nomino na kirai kitenzi.
Mfano: Wanafunzi wale walikuwa wanasoma darasani.
N.B:
- Katika uchanganuzi wa sentensi, ni muhimu kutofundishwa mikabala yote miwili (haipaswi).
- Hata hivyo, baadhi ya wataalamu wanachanganya mikabala yote miwili katika uchanganuzi wao wa sentensi, kama vile F. Nkwera (1978), TUMI (1988), J.S. Mdee (1996), Mohamed Taasisi ya Dimu (1966).
- Kutaja aina ya sentensi
- Kutaja sehemu za sentensi, yaani kiima/kikundi nomino, kiarifu/kikundi kitenzi
- Kutaja vipashio vinavyojenga kiima na kiarifu
- Kutaja aina za maneno yote yaliyomo katika sentensi
- Kuandika upya sentensi hiyo
- Mishale/ mistari
- Matawi/msonge/ngoe
- Maelezo/maneno
- Parandesi/mabano
- Jedwali/visanduku
Mkabala wa kimapokeo
- Sentensi: Mtoto Yule alikuwa anataka kucheza mpiraake uwanjani
- Hii ni sentensi sahili
- Kiima: Mtoto Yule
- Kiima kinanomino na kivumishi:
- Nomino: Mtoto
- Kivumishi: Yule
- Kiarifu: Alikuwa anataka kucheza mpiraake uwanjani
- Kiarifu kina vitenzi visaidizi viwili kitenzi kikuu, shamirisho, chagizo:
- Kitenzi kisaidizi cha kwanza: Alikuwa
- Kitenzi kisaidizi cha pili: Anataka
- Kitenzi kikuu: Kucheza
- Shamirisho: Mpiraake
- Nomino: Mpira
- Kivumishi: Ake
- Chagizo:
- Kielezi: Uwanjani
Mkabala wa kisasa
- Sentensi: Mtoto Yule alikuwa anataka kucheza mpiraake uwanjani
- Hii ni sentensi sahili
- Kirai nomino: Mtoto Yule
- Kirai nomino kina nomino na kivumishi:
- Nomino: Mtoto
- Kivumishi: Yule
- Kirai kitenzi: Alikuwa anataka kucheza mpiraake uwanjani
- Kirai kitenzi kina vitenzi visaidizi viwili kitenzi kikuu kirai, nomino, na kirai kielezi:
- Kitenzi kisaidizi cha kwanza: Alikuwa
- Kitenzi kisaidizi cha pili: Anataka
- Kitenzi kikuu: Kucheza
- Kirai nomino kina nomino na kivumishi:
- Nomino: Mpira
- Kivumishi: Ake
- Kirai kielezi kina kielezi:
- Kielezi: Uwanjani
Njia ya Mishale
Mkabala wa kimapokeo
Sentensi: Mtoto Yule alikuwa anataka kucheza mpiraake uwanjani
Mkabala wa kisasa
Njia ya Matawi
Njia ya Jedwali
Mkabala wa kimapokeo
Mkabala wa kisasa

- Ni sentensi inayotawaliwa na kishazi huru kimoja au zaidi, na kishazi tegemezi kimoja au zaidi.
- Kishazi huru/tegemezi hicho kinaweza kutokea upande wa kiima au kiarifu.
- Mfano: Wanafunzi waliotoroka jana wameadhibiwa leo asubuhi
- B
- Mfano mwingine: Mwalimu amewaadhibu wanafunzi waliotoroka jana
- B
- N.B: Sifa kubwa ya sentensi changamano ni kuwa na kishazi tegemezi ambacho hutegemea kishazi huru kilichomo ndani ya sentensi hiyo.
Miundo ya Sentensi Changamano
- Vishazi tegemezi vilivyomo ndani ya sentensi changamano ndiyo hutupatia miundo mbalimbali ya sentensi.
- Hii ni miundo ambayo kirai nomino hubeba kishazi tegemezi kirejeshi ambacho hurejesha tendo kwa mtenda au mtendwa.
- Mfano: Mbuzi aliyenunuliwa juzi ameibwa leo asubuhi
- BV
- Miundo yenye vishazi tegemezi wielezi.
- Hii ni miundo ambayo vishazi tegemezi hurejelewa/hueleza hali ya vitenzi vilivyomo kutoka vishazi huru.
- Mfano: Mimi sikuvutiwa alivyosema
- BE
- Mfano mwingine: Juma aliponiona alikimbia
- BE
Uchanganuzi wa Sentensi Changamano
- Kutaja aina ya sentensi
- Kutaja kiima/kirai nomino na kiarifu/kirai kitenzi
- Kutaja vishazi vilivyomo katika sentensi na kisha kueleza kazi ya kila kishazi
- Mfano: Kutaja kama kishazi tegemezi kinavumisha jina au kikundi jina kilichopo katika kiini
- Mfano: Mbuzi aliyenunuliwa juzi ameibwa leo asubuhi
- BV
- Mfano mwingine: Mwalimu aliwaadhibu wanafunzi waliotoroka
- Bv
- Mfano: Mbuzi aliyenunuliwa juzi ameibwa leo asubuhi
- Mfano: Kutaja kama kishazi tegemezi kinavumisha jina au kikundi jina kilichopo katika kiini
- Kutaja kama kishazi tegemezi kinavumisha nomino au kikundi nomino kilichopo katika shamirisho.
- Kutaja kama kishazi tegemezi kinatoa maelezo zaidi kuhusu kitenzi kikuu kilichopo katika kishazi huru.
- Mfano: Juma aliponiona alikimbia
- BE
- Mfano mwingine: Juma alikimbia aliponiona
- BE
- Mfano: Juma aliponiona alikimbia
- Kutaja aina zote za maneno katika sentensi hiyo
- Kurudia kuandika sentensi hiyo
Njia ya Matawi
Mkabala wa kimapokeo
Sentensi: Mtoto aliyekuletea maji ya kunywa ni mwanangu

Ni sentensi ambayo huwa na vishazi tegemezi viwili ambavyo utegemezi wake hutokana na mofimu "nge", "ngali", "ngeli", na "ki-".
Mofimu hizi hufanya vishazi hivyo vitegemeane, yaani kufanyika kwa tendo moja kunategemea tendo jingine au kutokuendeka kwa jambo fulani hutegemea kutokutendeka kwa jambo fulani.
Mfano: Juma angejibu maswali yote angefaulu mtihani.
Mfano mwingine: Ukisoma kwa bidii utafaulu mtihani.
N.B: Mofimu hizi zinapotumika katika sentensi shurutia huwa hazitakiwi kuchanganywa.
Mwalimu
Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.
Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.
Ingia ili kuuliza