Sonzaschool
Rudi

Sekondari ya Juu · Kidato cha Tano

Kiswahili 1

Kauli za kiswahili

takriban dakika 2 kusoma

Mada za sehemu hiiMatumizi Ya SarufiMada 7

Kauli za kiswahili

Kauli ya Kutenda

  1. Hueleza jambo lililotendwa na mtenda.

  2. Kiambishi tamati: -a

  3. Mfano:

    • gand-a
    • pig-a
    • som-a

Kauli ya Kutendwa

  1. Hueleza kuwa mtu/vitu wametendewa jambo.

  2. Alomofu: -w-, -liw-, -lew-

  3. Mfano:

    • pig-w-a
    • sem-w-a
    • chom-w-a
    • o-lew-a
    • vu-liw-a
    • ambi-w-a

Kauli ya Kutendewa

  1. Huonyesha mtu ametendewa jambo kwa niaba yake.

  2. Alomofu: -iw-, -ew-, -liw-, -lew-

  3. Mfano:

    • lim-iw-a
    • chez-ew-a
    • som-ew-a
    • kimbi-liw-a
    • zo-lew-a
    • va-liw-a
    • chomo-lew-a

Kauli ya Kutendea

  1. Tendo limefanyika kwa manufaa/faida ya mwingine.

  2. Alomofu: -i-, -e-, -li-

  3. Mfano:

    • pig-i-a
    • lal-i-a
    • ruk-i-a
    • chez-e-a
    • zo-le-a
    • o-le-a

Kauli ya Kutendesha

  1. Huonyesha mtu anavyosababisha mwingine kutenda jambo.

  2. Alomofu: -ish-, -esh-, -lish-, -lesh-, -sh-, -z-

  3. Mfano:

    • imb-ish-a
    • kimbi-z-a
    • tembe-z-a
    • pit-ish-a
    • ru-sh-a

Kauli ya Usababishaji (Kutendesha)

  1. Huonyesha wasababishi wa tendo kutokea kwa mhusika mwingine.

  2. Alomofu: -esh-, -lesh-, -lish-

  3. Mfano:

    • og-esh-a
    • zo-lish-a
    • ka-lish-a
    • va-lish-a
    • shon-esh-a
    • som-esh-a
    • chem-sh-a

Kauli ya Kutendana

  1. Hushirikisha wahusika wawili kutendeana kwa pande zote mbili.

  2. Alomofu: -an-

  3. Mfano:

    • pend-an-a
    • suk-an-a
    • sukum-an-a
    • sem-an-a
    • ruki-an-a

Kauli ya Kutendeana

  1. Mhusika wa kwanza hutenda kwa niaba ya mwingine na kinyume chake.

  2. Alomofu: -an- kati ya mzizi na kiambishi tamati.

  3. Mfano:

    • suk-i-an-a
    • sem-e-an-a
    • som-e-an-a
    • zo-le-an-a
    • va-li-an-a
    • o-le-an-a

Kauli ya Kufungamana (Kutendana maalum)

  1. Huonyesha watu/vitu kukaa pamoja kwa muda mrefu.

  2. Alomofu: -am-

  3. Mfano:

    • ung-am-a
    • ach-am-a

Kauli ya Kinyume cha Kutenda

  1. Huonyesha kinyume cha tendo (kubatilisha).

  2. Alomofu: -o-, -u-

  3. Mfano:

    • umb-u-a
    • teg-u-a
    • chom-o-a
    • kunj-u-a
    • pang-u-a

Kauli ya Kishikanishi (Kutendana maalum)

  1. Huonyesha mshikamano au kushikana kwa vitu/watu.

  2. Alomofu: -at-

  3. Mfano:

    • pak-at-a
    • kam-at-a
    • fumb-at-a

Mwalimu

Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.

Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.

Ingia ili kuuliza