Sonzaschool
Rudi

Sekondari ya Juu · Kidato cha Tano

Kiswahili 1

Makosa ya kisarufi na kimantiki katika lugha

takriban dakika 6 kusoma

Mada za sehemu hiiMatumizi Ya SarufiMada 7

Makosa ya kisarufi na kimantiki katika lugha

Haya ni makosa yanayotokana na kukiukwa kwa taratibu za kisarufi yaani matamshi ya maneno, miundo ya tungo, miundo ya maneno na maana za maneno.

Mara nyingi makosa haya hutokana na utumiaji mbaya wa lugha miongoni mwa wazungumzaji.

Kwa ujumla makosa ya kisarufi yanaweza kugawanyika katika makundi yafuatayo:

Makosa ya matamshi

Makosa hayo hujitokeza watu wanapozungumza kwa kushindwa kutamka baadhi ya sauti za Kiswahili au kuzichanganya na wakati mwingine kwa kutumia sauti zisizo sahihi au za kigeni.

Haya ni baadhi ya makosa yanayotokea:

  • Kuna baadhi ya watu huchanganya 'r' na 'l'.

    • Mfano: Naenda kurara.
  • Wengine wanatumia 's' badala ya 'z', 'dh' na 'h'

    • Mfano: Sahabu badala ya dhahabu.
    • Mfano: Samani sile badala ya zamani zile.
    • Mfano: Sambi badala ya dhambi.
    • Mfano: Dhibiti badala ya thibiti.
    • Mfano: Anapashwa badala ya paswa.

Kwa kawaida, makosa haya hutokana na athari ya lugha ya kwanza ambapo mzungumzaji huathiriwa na matamshi ya lugha aliyojifunza kwanza au aliyoizoea, ambayo mara nyingi hutofautiana na matamshi sahihi ya Kiswahili.

Aidha, makosa haya yanaweza kuonekana zaidi katika mikoa au maeneo yenye athari ya lugha nyingine kama vile lugha za kienyeji au lugha za kigeni zinazozungumzwa na jamii fulani.

Kuongeza vitamkwa

Makosa haya hufanya na wazungumzaji wanapokuwa wanazungumza kwa kuongeza vitamkwa katika maneno ambayo huwa havihitajiki katika maneno hayo na hivyo kuiharibu lugha hiyo.

  • Mfano: Tunakwendaga kwao mara kwa mara.
  • Hakunaga kitu kama hicho.
  • Yule mbaba jamani!

Kosa la kuacha maneno

Wazungumzaji baadhi wanapozungumza Kiswahili huacha maneno fulani katika sentensi na bado wakifikiri wanatoa ujumbe ulio kamili.

Mfano:

  1. Mama ameondoka mjini
  2. Mama ameenda mjini.
  3. Baba yako amerudi kazini?
  4. Baba amerudi kutoka kazini?

Kosa la tafsiri sisisi

Makosa yanatokana na tafsiri moja kwa moja na hivyo kusababisha makosa ya kisarufi katika lugha.

  • Mfano: aidha …….au

    • Mama aidha atakuwa mjini au kazini.
  • Osha uso wako badala ya nawa uso wako.

Makosa ya kimuundo

Makosa yanayojitokeza katika muundo, kwa kawaida miundo ya lugha ya Kiswahili huanza na nomino ya mtenda au mtendwa na kufuatwa na jambo analotendwa au analotenda yaani vitenzi.

Mfano: Sikuwa ninajua kuwa Grace ni dada yako

  • Sikujua kuwa Grace ni dada yako.

Makosa ya kimantiki

Mantiki ni utaratibu mzuri wa kufikiri.

Kwa mujibu wa kamusi ya Kiswahili sanifu toleo la pili (2004) inafasili mantiki kuwa ni mtiririko wa fikra zilizopangwa ili kujenga hoja yenye kukubalika.

Kutokana na fasihi hizi makosa ya kimantiki ni yake yanayoonesha kukosekana kwa utaratibu mzuri wa fikra au makosa yanayotokana na upotofu wa mawazo ya mzungumzaji.

Kwa maneno mengine ni makosa yanayotokana na kukosekana kwa mtiririko mzuri wa fikra zilizopangwa ili kujenga hoja zenye kukubadilika.

Kwa kawaida wazungumzaji na waandishi hufanya makosa ya kimantiki.

Mfano:

  1. Nyumba yangu imeingia siafu

    • Nyumba haiwezi kuingia siafu bali siafu huingia ndani ya nyumba
    • Siafu wameingia ndani ya nyumba yangu.
  2. Gari yangu imeibiwa

  3. Gari ndiyo imetedwa

  4. Gari yangu imeibwa

NB:

  1. Makosa ya kisarufi na ya kimantiki ni ya kawaida ambayo yapo na yataendelea kuwepo katika lugha.
  2. Jambo la msingi ni kuendelea kujazwa kabisa yasitumike katika taasisi rasmi kama vile shule, barua rasmi, na madhara na mikutano ya kitaaluma n.k
  3. Ni vizuri katika kutekeleza azima hii ya kuzuia makosa ya kimantiki na kisarufi mkazo wa marekebisho … Tangu kiwango cha awali.
  4. Hii itasaidia kupunguza makosa hayo kwa siku za baadaye.
  5. Kwa upande mwingine makosa haya husambazwa na vyombo vya habari na baadhi ya waalimu.
  6. Kwa hiyo ni vizuri walimu pamoja na vyombo vya habari kusisitiza matumizi sahihi ya lugha ya Kiswahili.

Utata katika matumizi ya lugha

Utata ni nini?

  1. Utata ni kitendo cha tungo kuwa na maana zaidi ya moja au kueleweka kwa namna mbili zaidi tofauti.
  2. Mara nyingi utata hujitokeza katika maana za maneno au maana za sentensi.

Sababu zinazosababisha utata

  1. Matumizi ya maneno yenye maana zaidi ya moja bila kuyapa muktadha wa kimatumizi. Mfano: Mama ana mbuzi Neno mbuzi lina maana mbili na hivyo hufanya sentensi zieleweke kuwa na namna mbili tofauti.

  2. Kutozingatiwa kwa taratibu za uandishi. Mfano: Nilimkuta Juma na rafiki yake George

  3. Mama John amekuja Katika lugha ya mazunguzo utata unaweza ukasababishwa na kutokuweka mkazo wa sauti mahali panapostahili katika neno. Mfano:

    • Mbuzi
    • Mbuni
  4. Utata unaweza ukasababishwa na matumizi ya mashina lugha ya picha au lugha ya mtaani au lugha iliyojificha. Mfano:

    • Juma anaua chumbani mwake anatoa uhai
    • Ana msichana mzuri chumbani mwake Ana maua chumbani mwake

Namna ya kuondoa utata

  1. Kuyapa maktadha wa kimatumizi maneno yenye maana zaidi ya moja. Mfano: Mama ana mbuzi wengi Mama ana mbuzi ya kukuna nazi.

  2. Kuweka mkazo wa sauti katika silabi stahiki katika neno. Mfano: Mbuni - Mbuni ni mzuri Mbuni – Mbuni ni mzuri

  3. Utata unaweza ukaondolewa kwa kuzingatia matumizi sahihi ya alama za uandishi. Mfano: Baba, John amefika Baba John, amefika

  4. Kuepuka matumizi ya lugha ya picha. Mfano: Juma anaua chumbani mwake Mzungumzaji aliyetumia sentensi hii akiwa anakusudia kuonesha kuwa Juma ana mchumba mzuri nyumbani kwake alipaswa kuepuka matumizi ya picha kwa kusema "Juma ana mchumba mzuri nyumbani kwake" Kwa kufanya hivyo angekuwa ameondoa utata uliokuwepo katika sentensi ya awali

NB: Wakati mwingine utata unaweza ukasababishwa na matumizi ya kutanguliza nomino ya mtendwa badala ya kutangulia nomino ya mtenda. Mfano: Simba ameuawa na askari pori Sentensi hii ni tata kwa sababu ina maana zaidi ya moja.

  1. Simba na askari pori wote wameuawa.
  2. Askari ndiye aliyemuua samba Kama nomino ya mtenda ingetangulia kusingegkuwa na utata. Askari pori ameua simba.

Mwalimu

Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.

Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.

Ingia ili kuuliza