Mada za sehemu hiiKuonesha Uelewa Wa Jambo Ulilolisikiliza Au KulisomaMada 6
Hali ya hewa ni jumla ya hali tofauti zinazomzunguka mwanadamu katika mazingira yake. Mfano upepo, baridi, joto, kipupwe, mvua n.k. kila hali ya hewa huweza kuoneshwa kwa dalili ambazo huleta athari fulani katika mazingira. Miongoni mwa hali hizo za hewa ni ukungu, upepo, joto, baridi na mvua
Shughuli za binadamu zinategemea hali ya hewa ya mahali. Kila kipengele cha hewa ni muhimu katika shughuli za binadamu. Vipengele vya hali ya hewa vinatakiwa viwe na uwiano sawa.
Mwalimu Ana anatufundisha somo la jiografia darasa la sita katika shule ya msingi uswaa huko mkoani Kilimanjaro. Siku moja alitufundishajuu ya hali ya hewa na majira ya hali hizo za hewa. Alianza kwa kusema.
Aina za majira ya mwaka hapa kwetu Tanzania ziko nne, kuna majira ya mvua za vuli, majira ya mvua za mwaka, majira ya baridi na majira ya joto.
Majira haya hutofautiana kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa sababu mbalimbali. Baadhi ya sababu hizo ni umbali kutoka usawa wa bahari, mwinuko kutoka usawa wa bahari na kuwapo kwa milima, misitu au majangwa.
Majira ya mvua yako ya aina mbili. Mvua za mwaka na mvua za vuli. Si kila sehemu nchini hupata aina zote mbili za majira ya mvua.
Majira yajoto hujulikana kama kiangazi. Mvua huadimika kabisa na ardhi inakuwa kame. Ni wakati ambapo vyito vya muda na visima vifupi hukauka na uhaba mkubwa wa maji hutokea.
Majira ya kipupwe ni kipindi cha baridi. Sehemu za pwani huwa na baridi kiasi lakini milimani huwa na baridi kali. Watu huvaa nguo nzito na usiku hujifunika gubigubi.
Faida za kuwa na majira mbalimbali ya mwaka ni nyingi. Wakati wa mvua watu hupanda mazao ya chakula na biashara. Wakati wajoto, watu hufanya kazi za ujenzi. Wakati wa baridi ni wakati wa kupata hewa nzuri.
Baadhi ya maneno ya Kiswahili yana maana zaidi ya moja kutegemeana na jinsi neno lilivyotumika au lilivyotamkwa. Maneno yenye maana zaidi ya moja huitwa maneno tata. Utata katika mawasiliano hutokea pale mtu anapotumia maneno yenye maana zaidi. Utata hutegemea muktadha mbalimbali pamoja na matamshi au hata mazingira ya neno linalohusika. Utata unaweza kujitokeza katika neno na wakati mwingine katika sentensi.
Mfano
Kaa - neno hili lina maana zifuatazo
i) Kaa la moto
Sentensi
Mtoto amekalia kaa la moto
ii) Kuweka makalio chini kitini
Sentensi
Wanafunzi wote wanatakiwa kukaa chini
iii) Mnyama wa majini
Sentensi
Tulipokwenda mtoni kuteka maji tulimwona kaa
Siku moja dada alimwomba mama amfundishe kupika samaki mbichi wa kuchemsha. Mama alimkubalia ombi lake. Alimwambia atamfundisha siku inayofuata.
Muda ulipowadia, mama alimwita dada ili amfundishe kupika samaki mbichi wa kuchemsha. Dada alikaa kwenye mkeka kisha akamsikiliza mama kwa makini.
Mama alimwambia, unachukua samaki na kumpaa. Unahakikisha magamba yote yametoka kisha unamwosha kwa maji safi, ukimaliza kumwosha unamwacha achuruzike maji. Baada ya hapo unampaka viungo kama vile chumvi, ndimu, kitunguu swaumu na tangawizi. Viungo husaidia kuondoa shombo na pia humfanya samaki awe na ladha nzuri.
Baada ya hapo unachukua mbuzi na kukuna nazi, kisha unachuja nazi. Tui zito la kwanza unaloweka pembeni kwani tui hili hutumika mwishoni pale samaki anapokua amekaribia kuiva. Unachuja tena tui jepesi na kuliweka kwenye sufuria ya kupikia samaki. Kisha unachukua karoti na vitunguu maji na kuvikata vipande vidogovidogo.
Bandika sufuria lenye tui jepesi jikoni na kisha weka karoti na vitunguu na ongeza chumvi kidogo. Acha tui jepesi lichemke kwa dakika tano kisha tumbukiza samaki mbichi. Mwache achemke akikaribia kuiva weka tui zito. Acha lichemke kwa dakika nane, tui litakua limeiva na samaki atakua ameiva. Ila unatakiwa kuangalia samaki asirojeke. Baada ya hapo epua samaki atakua tayari kwa kuliwa.
Samaki wa kuchemsha anaweza kuliwa na ugali, wali au chapati. Pia samaki hutupa protini ambayo ni muhimu katika miili yetu.
Mwalimu
Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.
Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.
Ingia ili kuuliza