Mada za sehemu hiiKuonesha Uelewa Wa Jambo Ulilolisikiliza Au KulisomaMada 6
MAZOEZI YA LUGHA
Kanusha sentensi zifuatazo
-
Fundi huyu ameshona nguo zangu vibaya Fundi huyu hajashona nguo zangu vibaya
-
Kiranja amewahi shuleni Kiranja hajawahi shuleni
-
Kiatu hiki ni kipya Kiatu hiki si kipya
-
Shule ina upungufu wa samani Shule haina upungufu wa samani
-
Shambani kwetu ni mbali na mjini Shambani kwetu si mbali na mjini
-
Kutembea gizani ni kuzuri Kutembea gizani si kuzuri
-
Shule yetu ina maktaba kubwa Shule yetu haina maktaba kubwa
-
Huyu ni daktari bingwa Huyu si daktari bingwa
-
Kazi ya kulima ina changamoto kubwa Kazi ya kulima haina changamoto kubwa
-
Mwajuma ni mtoro Mwajuma si mtoro
-
Mtoto mkorofi hupendwa na mwalimu Mtoto mkorofi hapendwi na mwalimu
-
Salumu aliishia darasa la sita Salumu hakuishia darasa la sita
-
Rushwa huwaathiri watu wenye fedha tuu Rushwa haiwaathiri watu wenye fedha tuu
-
Kwetu kuna milima mingi Kwetu hakuna milima mingi
Mwalimu
Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.
Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.
Ingia ili kuuliza