Sonzaschool
Rudi

Msingi · Darasa la Sita

Kiswahili

Uandishi Na Usikilizaji wa Habari

takriban dakika 5 kusoma

Mada za sehemu hiiKuonesha Uelewa Wa Jambo Ulilolisikiliza Au KulisomaMada 6

a) Kusikiliza habari na kujibu maswali yatokanayo na habari

Shujaa ni mtu mwenye moyo wa ujasiri katika kukabili mambo hata kama ni hatari.

Mambo ya kishujaa yanaweza kuwa ni kupigana vita na maadui: kupambana na majambazi hatari, kuokoa watu katika janga fulani, kupambana na wanyama wakali na kukomboa watu kutoka katika utawala wa kikandamizaji na katika unyonyaji.

Katika historia, Bara la Afrika liliwahi kuvamiwa na kutawaliwa na wakoloni. Waafrika wengi walipinga uvamizi wa wakoloni wakiongozwa na machifu wao.

Wakoloni walipokuja kulivamia Bara la Afrika, hapo hapo kuna machifu wajamii mbalimbali walikataa na kupinga uamuzi huo. Walipambana na wakoloni ili wasieneze utawala wao. Viongozi hao waliona hapana budi kutetea himaya zao. Miongoni mwa watawala hao ni mtwa mkwawa wa mtemi Mirambo katika Tanzania. Shaka Zulu wa Afrika kusini na kabaka Mutesa wa Uganda. Hawa walisimama kidete kuhakikisha wanapambana na wakoloni ili wasiwatawale maeneo yao na wananchi kuonewa.

Wakati Bara la Afrika lilipokuwa linatawaliwa na wakoloni,waliibuka wapigania uhuru wa nchi zao. Wao walipigania uhuru tuliokuwa tumenyanganywa na wageni. Mashujaa hao ni Kwame Nkurumah wa Ghana, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere wa Tanzania, Samora Masheli wa Msumbiji. Hao walipambana na ukoloni hadi waliporejesha uhuru wa nchi zao na wakoloni wakafunga virago vyao na kurudi makwao.

Baada ya uhuru wa nchi zao, mashujaa hao wamebakia kuwa watu muhimu wa kukumbukwa katika historia ya Bara la Afrika.

Wengi wao hawakuwa na tamaa ya madaraka. Mfano Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ni kiongozi aliyeamua kuachia madaraka akiwa na nguvu, anapendwa na watu na bado alikua na uwezo wa kuongoza. Nelson Mandela ni kiongozi mwingine ambaye baada ya kuikomboa Afrika kusini kutoka kwa makaburu, aliongoza kwa miaka mitano kisha akaachia madaraka.

UFAHAMU

1. Shujaa ni mtu wa namna gani?

Shujaa ni mtu mwenye moyo wa ujasiri katika kukabili mambo hata kama ni ya hatari.

2. Taja vitendo vya kishujaa

Vitendo vya kishujaa ni

  1. Kupigana vita na maadui
  2. Kupambana na majambazi hatari
  3. Kuokoa watu katika janga fulani
  4. Kukomboa watu katika utawala wa kikandamizaji

Katika historia Bara la Afrika liliwahi kuvamiwa na kutawaliwa na nani?

Katika historia Bara la Afrika liliwahi kuvamiwa na kutawaliwa na wakoloni

Taja machifu waliopambana ili ukoloni usienee ni

Machifu waliopambana ili ukoloni usienee ni:-

  1. Mtwa mkwawa wa Tanzania
  2. Mtemi mirambo wa Tanzania
  3. Shaka zulu wa Afrika kusini
  4. Kabaka mutesa wa Uganda

Kwame Nkurumah alipigania uhuru wa nchi gani?

Kwame Nkurumah alipigania uhuru wa Ghana

Viongozi gani ambao hawakuwa na uroho wa madaraka

Viongozi ambao hawakuwa na uroho wa madaraka ni Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Nelson Mandela wa Afrika ya kusini.

Badili sentensi zifuatazo kuwa kauli taarifa

  1. "Mtoto anaimba vizuri" dada amesema

Dada amesema kwamba mtoto anaimba vizuri

  1. Baba ametuambia "kaka amepewa zawadi baada ya kushinda mbio za marathoni"

Baba ametuambia kwamba kaka amepewa zawadi baada ya kushinda mbio za marathoni

  1. "Nitasafiri kesho asubuhi" mama alisisitiza

Mama alisisitiza kuwa atasafiri kesho asubuhi

  1. "Mwaka huu una mazao mengi" Mjomba amesema

Mjomba amesema kwamba mwaka huu una mazao mengi

  1. Mwalimu alitueleza, "Kiswahili kinafundishwa hadi nje ya nchi yetu"

Mwalimu alitueleza kwamba Kiswahili kinafundishwa hadi nje ya nchi yetu

  1. "Karanga zote zimeisha shambani" bibi alisema

Bibi alisema kwamba karanga zote zimeisha shambani

  1. "Mimi nitachezea timu ya Taifa" mwanafunzi alisema

Mwanafunzi alisema kwamba atachezea timu ya Taifa

  1. Dada aliniambia "Nitakuletea zawadi"

Dada aliniambia kwamba ataniletea zawadi

  1. Bibi alitueleza "sitahudhuria mkutano"

Bibi alitueleza kwamba hatahudhuria mkutano

  1. "Kesho tutakula pilau" Mama alisema

Mama alisema kwamba kesho tutakula pilau

  1. "Nitafua kesho jioni" Mtoto alisema

Mtoto alisema kwamba atafua kesho jioni

  1. Babu alisema, "Mwaka huu kilimo kimekubali sana"

Babu alisema kwamba mwaka huu kilimo kimekubali sana.

Kubaini makosa ya kiuandishi katika matini anuai

Lugha ndicho chombo kikuu cha mawasiliano baina ya watu. Hivyo ili watu waitumie lugha kwa kuelewana lazima itumike kwa usahihi. Mzungumzaji akikiuka kanuni za lugha, huzungumza lugha potofu.

Upotoshaji huu hujitokeza katika sarufi na kwenye mantiki. Makosa katika sehemu zote mbili husababisha kukatika kwa mawasiliano au kutoa ujumbe uliokusudiwa.

Soma habari ifuatayo kisha onesha maneno yenye makosa

Furaha ni madini ya thamani sana. Furaha ingaliuzwa ingalikua ghali mno, kwani ingalipatikana kwa rahisi ingalipoteza thamani yake.

Binadamu huanza kuonesha furaha tokea utotoni kwa kutabasamu na kucheka. Furaha ya kudumu haitokani na nasaba bora, elimu kubwa au mali nyingi, bali inatokana na mtu kuishi na wenzake kwa kujiamini, kufanya kazi kwa bidii na kuridhika.

Chozi lilivyokua na thamani kubwa limegawanyika tu kwa mtu kufiwa na wazazi, lakini humwagwa pia katika furaha. Dunia ingalikua nzuri zaidi walimwengu wangelitumia nia njema, maarifa na juhudi kutokomeza chuki, dhuluma, dhiki, na ubaguzi, wakajenga na kuimarisha udugu, haki na usawa.

MANENO YENYE MAKOSA

  1. Samani — thamani
  2. Gali — ghali
  3. Lahisi — rahisi
  4. Zuluma — dhuluma
  5. Ziki — dhiki
  6. Kulizika — kuridhika

Kusoma matangazo na kubaini taarifa muhimu

Tangazo ni taarifa inayotolewa hadharani ili ipate kuwafikia watu wanaohusika na taarifa hiyo. Taarifa inaweza kuwa ya mkutano, semina, msiba, masomo, nafasi za kazi, onyo au burasa. Taarifa huweza kutolewa kwenye vyombo vya habari kama vile redio, televisheni, magazeti. Pia kwenye mabango.

Mwalimu

Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.

Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.

Ingia ili kuuliza