Mada za sehemu hiiKuonesha Uelewa Wa Jambo Ulilolisikiliza Au KulisomaMada 6
Kamilisha methali zifuatazo
- Ada ya mja hunena, muungwana ni kitendo
- Avumae baharini papa, na wengine wamo
- Furaha ya mwenye meno, kibogovo hashiriki naiaii yaku iiaianiu &wa niwenzano
- Hapana siri ya watu wawili
- Hen kenda shika kuliko kumi nenda rudi
- Ivumayo haidumu
- Jembe halimtupi mkulima
- Kata pua uunge wajihi
- Kataa neno usikatae wito
- Kauli ni bora kuliko mali
- Heri umfadhili mbuzi bmadamu ataakuudhi
- Kipendacho roho, hula nyama mbichi
- Kitanda usichokilalia huwajui kungum wake
- Kuishi kwingi ni kuona mengi
- Kuku mgeni hakosi kamba mguuni
- Kuteleza siyo kuanguka
- Kuvuja kwa pakacha nafuu kwa mchukuzi
- La kuvunda halina ubani
- Leo ni leo asemaye kesho ni mwongo
- Macho havana pazia
- Maji hufuata mkondo
- Mali bila daftari hupotea bila habari
- Manahodha wengi chombo huenda mrama
- Mbio za sakafuni huishia ukingoni
- Mkataa pema pabaya panamuita
- Mkono mtupu haulambwi
- Mla mla leo mla jana kala nini?
Ni semi fupifupi ambazo hutumia lughamaneno ya kawaida lakini maneno hayo hutoa maana tofauti na ile iliyo kwenye maneno ya awali. Japokuwa nahau hutumia maneno ya kawaida lakini kauli yake ina undani kiasi kwamba kwa wageni wasioifahamu lugha hiyo hawawezi kuelewa maana.
Mfano
- Ana mkono mrefu - mwizi
- Kuzunguka mbuyu - kutoa rushwa
- Ana mkono wa birika - mtu bahili
Nahau kama zilivyo methali nazo zina maana. Maana ya nahau hujengwa na taswira za kimawazo zilizomo ndani yake.
Methali ni usemi mfupi wa mapokeo wenye mpangilio maalumu wa maneno unaodokeza lava muhtasari fikra au mafunzo mazito vatokanayo na uzoefu wa maisha yajamii husika.
Ni kauli fupi yenye pande mbili za fikra ambaye upande wa kwanza huanza na upande wa pili humaliza.
Mfano
Asiyesikia la mkuu huvunjika guu
Maana
Asiyefuata ushauri wa wakuuu wake mabaya humpata
Alive juu mngoje chini
Maana
Anayejitapa ameshafaulu maishani punde atafeli
Mzee Jangala ni mwenyekiti wa kijiji cha samaki maini. Wananchi wa kijiji cha samaki maini ni walevi kupindukia na hawapendi kufanya kazi kwa bidii. Pia hawana ushirikiano katika kazi za kijamii kama vile kutengeneza barabara, kuchimba mtaro.
Siku moja mzee Jangala aliita mkutano wa kijiji Mungu si athumani wanakijiji walijitokeza kwa wingi. Mzee Jangala alianza kwa kuwasalimu wanakijiji wenzake kisha akawaambia. Wanakijiji wenzangu msema kweli ni mpenzi wa Mungu na mficha uchi hazai hivyo lazima niwaeleze ukwelijuu ya hiki. Kijiji chetu hakina maendeleo nahii ni kwasababu hatuna ushirikiano. Tukikubaliana kufanyajambo wanaojitokeza huwa ni wachache sana. Mnasahau kwamba umoja ni nguvu utengano ni udhaifu. Kama tungejitokeza wote na kushirikiana wote barabara yetu ya kwenda hospitali tungemaliza kuitengeneza. Na ni barabara muhimu sana.
Mzee Jangala aliendelea kuwaambia wanakijiji wenzake kwamba. Kijiji chetu wananchi hamfanyi kazi kwa bidii. Na hii inapelekea badhi ya kaya kushindwa kuhudumia kava zao kwa kuzipatia mahitaji muhimu kama vile Chakula, hata wazee wa zamani walisema mgaa gaa na upwa hali wali mkavu na mkono mtupu haulambwi. Hivyo basi kama kila mtu atajishughulisha kwa bidii watoto hawatakufa njaa.
Hivyo wanakijiji wenzangu amkeni mfanye kazi kwa bidii.
Pia tabia ya ulevi wa kupindukia imekithiri sana hapa kijijini. Unakutana na mtu saa mbili asubuhi amelewa Chakari. Hivi tunawafundisha nini watoto wetu ambao ni Taifa la kesho? Watoto wetu wataiga ulevi. Maana mtoto wa nyoka ni nyoka na pia mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Hivi na hao watoto wakija kuwa walevi tutamlaumu nani? Jamani wanakijiji wenzangu tusiwalee watoto wetu kwenye misingi mibovu ya ulevi kupindukia.
Baada ya kusema hayo mwenyekiti aliwauliza wananchi wa kijiji cha samaki maini kama wana jambo la kuchangia. Mzee Juma alisimama na kuanza kumshukuru mwenyekiti wa kijiji kwa kuandaa mkutano. Alisema ni kweli kijiji chetu kinaongoza kwa ufukara. Na hili tatizo tumechangia sisi wenyewe kwani mchimba kisima hutumbukia mwenyewe.
Kuanzia sasa tutafanya kazi kwa bidii hasa kazi zetu za kilimo kwani jembe halimtupi mkulima. Tabia za ulevi nazo tutaziache. Mambo yote yanayopelekea kijiji chetu kuwa fukara tutayaache. Kwani mdharau mwiba mguu huota tende. Hatutakunywa pombe kwa kificho saa za kazi. Tunakuomba ndugu mwenyekiti wenye kuuza pombe wasiuze saa za kazi. Na kila mtu awe mlinzi wa mwenzie asitokee mtu yeyote atakavekunvwa pombe wakati wa saa za kazi. Maana mficha maradhi kifo humuumbua.
Mwenyekiti wa kijiji alifurahi kusikia kwamba wananchi wake watajirekebisha. Aliwaaga kwa kuwaambia asiyesikia la mkuu huvunjika guu. Hivyo kila mtu akatekeleze majukumu yake jinsi tulivyokubaliana ili kijiji chetu kiondokane na ufukara
Methali ni usemi mfupi wa mapokeo wenye mpangilio maalumu wa maneno unaodokeza lava muhtasari fikra au mafunzo mazito yatokanayo na uzoefu wa maisha yajamii husika.
Ni kauli fupi yenye pande mbili za fikra ambaye upande wa kwanza huanza na upande wa pili humalizia
Mfano
- Usimhukumu dobi, kaniki ndiyo rangi yake
- Tumikia kafiri, upate mradi wako
- Mpanda ovyo, hula ovyo
- Aliyekupa wewe kiti ndiye aliyenipa mimi kumbi
Baadhi ya methali huwa na maana zinazofanana, yaani hutoa ujumbe unaofanana.
Mfano
- Hasira za mkizi tijara ya mvuvi ina ujumbe unaofanana na ule wa methali ya "Vita vya panzi furaha ya kunguru." Methali hizi zinatuonya tuangalie matendo au uamuzi wetu usije ukatutia hasara na ukawanufaisha wengine.
- Ndondondo si chururu ina ujumbe unaofanana na ule wa methali ya "haba na haba hujaza kibaba." Methali hizi zina maana kwamba juhudi katika kutimiza kitu hata kama ni kidogo mwishowe huzaa matunda makubwa.
- Hakuna kama mama methali hii ina maana sawa na methali "Titi la mama litamu hata likiwa kama la mbwa."
- Heri kenda shika kuliko kumi nenda rudi
- Moja shika si kenda nenda urudi
- Jana hairudi tena
- Ujana ni moshi, uendapo haurudi
- Jembe halimtupi mkulima
- Mgaagaa na upwa hali wali mkavu
- Figa moja haliinjiki chungu
- Kidole kimoja hakivunji chawa
- Kanzu ya kuazima usiivae ijumaa
- Nguo ya kuazima haisitiri matako
- "Ndondondo si chururu"
- Haba na haba hujaza kibaba
- Kidogokidogo ndio mwendo
- Papo kwa papo kamba hukatajiwe
- Polepole ya kobe humfikisha mbali
- Udongo uwahi ungali maji
- Usipoziba ufa utajenga ukuta
- Mtoto mkanye angali mdogo
- Samaki mkunje angali mbichi
- Mchimba kisima huingia mwenyewe
- Sheria ni msumeno
- Kupanda mchongoma kushuka ndio ngoma
- Kinyozi hajinyoi na akijinyoa hujikata
- Milima haikutani lakini binadamu hukutana
- Mdharau mwiba mguu huota tende
- Mchelea haki hatendi ukweli
- Kidole kimoja hakivunji chawa
- Umoja ni nguvu utengani ni udhaifu
- Fimbo ya mbali haiui nyoka
- Kamba ya mbali haifungi kuni
Mwalimu
Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.
Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.
Ingia ili kuuliza