Mada za sehemu hiiKuonesha Uelewa Wa Jambo Ulilolisikiliza Au KulisomaMada 6
- Kubaini hoja Katika Majadiliano
- Kubaini taarifa Muhimu Kwenye Matangazo
- Methali na Nahau
- Uandishi Na Usikilizaji wa Habari
- Uchambuzi wa Habari
- Uchambuzi wa Hadithi
- Kutumia lugha inayoeleweka
- Kutumia maandishi yanayosomeka vizuri
- Kutumia picha na michoro inapowezekana
- Kutoa maelezo yanayojitosheleza ili tangazo lipate kueleweka
- Kama tangazo linatokea redioni au kwenye televisheni litolewe kwa kutumia sauti inayosikika vizuri
Mbuyeku Limited ni kampuni inayojishughulisha na uuzaji na usambazaji wa vifaa vya ujenzi kama vile mabati, simenti, nondo n.k. Kampuni inatoa nafasi mbili za kazi:
Mhasibu na Katibu Muhtasi
MHASIBU
Majukumu ya mhasibu ni kusimamia mahesabu ya kampuni, kuandaa ripoti za fedha, kufuatilia masuala ya kodi na kubuni mikakati ya kutumia vizuri rasilimali za kampuni.
ELIMU NA UZOEFU
- Shahada ya ACCA au CPA na Hali ya uthibitisho ya NBAA
- Ujuzi wa kanuni mbalimbali na sheria zinazohusiana na taaluma ya uhasibu
- Ujuzi wa kutumia kompyuta ya kiuhasibu
- Uzoefu wa miaka mitatu katika kusimamia mifumo ya uhasibu
- Uandaaji wa ripoti za uhasibu mahali pa kazi na shughuli nyingine za kitaaluma
KATIBU MUHTASI
Mwombaji anatarajiwa kuisaidia menejimenti katika shughuli mbalimbali za utawala na uendeshaji wa kampuni ikiwemo kupokea na kusambaza taarifa, kushughulikia barua zinazoingia na kutoka, kuandaa mikutano, kuweka mafaili katika mifumo na shughuli zingine za kiutawala.
ELIMU NA UZOEFU
- Mafunzo ya usekretari kutoka chuo kinachotambulika
- Ujuzi wa matumizi ya kompyuta
- Ujuzi wa kanuni na uelewa wa kuendesha ofisi
- Ujuzi na uzoefu wa mawasiliano na uandishi wa ripoti
- Uzoefu wa kazi ya usekretari wa miaka miwili
JINSI YA KUTUMA MAOMBI
Waombaji waandike barua za maombi, waambatanishe na wasifu binafsi (CV) na nakala za vyeti, namba za simu na anwani za barua pepe. Barua za maombi zinaweza kupelekwa jengo la Josam Mwenge, ofisi za Mbuyeku Limited au kutumwa kwa Meneja Mbuyeku Limited, S.L.P 2502, Dar es Salaam. Tarehe ya mwisho kupokea maombi ni tarehe 15.4.2020.
Watakaojibiwa ni wale tu watakaoorodheshwa kwa ajili ya kusailiwa
Tangazo hili linahusu nini?
- Tangazo hili linahusu nafasi za kazi ya uhasibu na katibu muhtasi.
Tangazo hili limetolewa na kampuni gani?
- Tangazo hili limetolewa na kampuni ya Mbuyeku Limited.
Kampuni hiyo inajishughulisha na nini?
- Kampuni hiyo inajishughulisha na uuzaji na usambazaji vifaa vya ujenzi.
Barua za maombi zinatakiwa kutumwa kwa nani?
- Barua za maombi zinatakiwa kutumwa kwa Meneja wa Mbuyeku Limited.
Barua za maombi zinatakiwa ziambatanishwe na vitu gani?
- Barua za maombi zinatakiwa ziambatanishwe na wasifu binafsi (CV) na nakala za vyeti, namba za simu na anwani za barua pepe.
Lini ni mwisho wa kupokea maombi?
- Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 15.4.2020
Tunakaribisha maombi ya kusafirisha kahawa kutoka Moshi, Kilimanjaro kwenda Congo. Magari yanayohitajika ni vile vinyenye uwezo wa kuchukua kuanzia uzito wa tani kumi (10).
Malipo mazuri na ya kuvutia yatatolewa.
Kuhusu hati za maombi na maelezo zaidi, mwone au mpigie simu:
Meneja Mkuu Mamlaka ya Kahawa (KNCU) S.L.P 21 Moshi - Kilimanjaro
Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 15.4.2020
Mwalimu
Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.
Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.
Ingia ili kuuliza