Mada za sehemu hiiKuwasiliana Katika Miktadha MbalimbaliMada 6
Uandishi wa barua
Chakupewa ni mwalimu anayefundisha katika shule ya msingi Kibaoni. Anafundisha somo la Kiswahili darasa la tano. Siku moja alituuliza kama kuna mwanafunzi amewahi kuandika kuiona barua ya kiofisi, wote tulimjibu hatujawahi kuandika wala kuiona. Mwalimu alituambia atatufundisha jinsi ya kuandika barua ya kiofisi. Sote tulifurahi.
Mwalimu alianza kwa kututajia vipengele vya uandishi wa barua na kutueleza vinavyotamkwa viwe katika mtiririko wake. Hivyo mwalimu alianza hivi:
i) Anwani ya mwandishi
Hii huandikwa kwenye pembe upande wa kulia wa karatasi.
ii) Tarehe
Hii huandikwa baada ya anwani ya mwandishi huandikwa chini ya anwani ya mwandishi.
iii) Anwani ya mwandikiwa
Hii huanza na cheo cha mwandikiwa na huandikwa upande wa kushoto mwa karatasi.
iv) Mwanzo wa barua
Huandikwa chini ya kichwa cha barua na mara nyingi neno ndugu hutumika kama salamu.
v) Barua yenyewe
Hapo huandikwa mambo yote muhimu yahusuyo dhumuni la barua hiyo. Hapa lazima barua ieleze mambo muhimu kwa ufupi.
vi) Mwisho wa barua
Huwa ni kimalizio cha barua. Mara nyingi maneno yanayotumika mwisho wa barua ni "wako mtiifu", "wako katika ujenzi wa Taifa.
vii) Saini na jina la mwandishi
Hapa mwandishi husaini kwanza na ndipo huandika jina lake.
viii) Cheo cha mwandishi
Kama mwandishi wa barua ana cheo basi huandika cheo chake chini baada ya jina lake.
Sote tulifurahi jinsi mwalimu Chakupewa alivyotuelekeza vipengele vyote vya uandishi wa barua ya kiofisi. Mwalimu alituambia kila mwanafunzi aandike barua ya kiofisi na tumpelekee ili aone kama tumeelewa. Kila mwanafunzi alichukua karatasi na kuanza kuandika barua ya kiofisi kwa kufuata mtiririko wa vipengele vyake.
Mwanafunzi aandike barua ya kiofisi na mwalimu aisahihishe. Mwanafunzi atachagua mwenyewe lengo la barua yake na ofisi anayoiandikia.
Barua ya kiofisi
MWALIMU ASHA MJUMBE S.L.P 10 DAR ES SALAAM
15.12.2018
MZAZI WA ASHA NGEDERE S.L.P 8 DAR ES SALAAM
YAH: WITO WA KUFIKA SHULENI TAREHE 18.12.2018
Ndugu mzazi,
Kichwa cha habari hapo juu chahusika. Unaombwa kufika hapa shuleni tarehe 15.12.2018, saa 4:30 asubuhi, mwanao Asha Ngedere amefanya uharibifu wa samani za shule. Hivyo kamati ya shule imekaa na kuamriwa ufike shuleni kwa ajili ya mazungumzo ya uharibifu alioufanya mwanao. Nitashukuru kama utaonesha ushirikiano.
Wako katika ujenzi wa taifa
Mwl Asha Mjumbe
Mwalimu wa darasa
Mwalimu
Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.
Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.
Ingia ili kuuliza