Mada za sehemu hiiKuwasiliana Katika Miktadha MbalimbaliMada 6
i) Nukta.
Hii huwekwa mwisho wa sentensi ni pumziko kubwa, hutumika katika kufupisha maneno, katika hesabu kuonyesha sehemu isiyo nzima, kuonyesha senti katika pesa.
ii) Mkato au koma
Hii ni pumziko dogo na pia hutumika pale unapo orodhesha vitu mfano karanga, mtama, mahindi, na njegere, hutumika kugawanya mawazo katika sentensi, kutoa maelezo zaidi na katika tarakimu, kugawa elfu.
iii) Mshangao !
Hii huonesha mshangao wajambo, mfano: Ah! Ehe! na kuigiza tanakali za sauti.
iv) Ulizo ?
v) Funga semi na fungia semi
Katika kuandaa matini mbalimbali
- Kuandika kifungu cha habari fupi kwa mpangilio wa sentensi unaoeleweka.
Mwanafunzi aandike habari fupi ya ugonjwa wa kipindupindu kwa mpangilio unaoeleweka.
Bwana Mkoi ni mwenyekiti wa kijiji cha Lokiri. Bwana Mkoi ni mchapakazi na mwenye kupenda maendeleo.
Mwaka mmoja kijiji hicho kilikumbwa na ugonjwa wa kipindupindu. Watu wengi walilazwa hospitalini. Hospitali ilifurika wagonjwa hadi wengine walilazimika kulala chini, watu wengi walipoteza maisha.
Bwana Mkoi aliitisha mkutano wa dharura na watu wengi wahfika kwenye mkutano.
Bwana Mkoi alianza kwa kuwasalimia na kuwaelezea madhumuni ya mkutano ule. Alianza kwa kuwaambia ugonjwa wa kipindupindu husababishwa na uchafu. Hivyo jamii inatakiwa kubadilika na kuacha kujisaidia hovyo, kila mtu achimbe choo na kukitumia. Pia aliwaasa wasile matunda bila ya kuvaosha, wahakikishe wananawa mikono kabla ya kula na baada ya kutoka msalani.
Wananchi wa kijiji walifurahi sana kwa kupata elimu hiyo. Kila mtu aliahidi atabadilika na atafuata kanuni za usafi pamoja na kuhakikisha kila kava ina choo.
Kwa kutumia nyingi, kidogo, mengi, chache.
Mwanafunzi achanganue vitu mbalimbali na kuvitofautisha kiasi chake kwa kutumia nyingi, kidogo, mengi, chache.
Maharage, kunde, vikombe, mayai, mchanga, sukari, chumvi, vibakuli, sahani, maji, vijiko.
i) Nyingi
- Sukari kilo moja ni nyingi kuliko sukari yenye ujazo wa nusu kilo.
- Mchanga wa baharini ni mwingi kuliko mchanga wa kwenye vidimbwi.
- Maharage ni mengi kuliko kunde.
- Maji ya baharini ni mengi kuliko ya kwenye kidimbwi.
ii) Kidogo
- Mvua za vuli ni kidogo kuliko za masika.
- Maji ya mferejini ni kidogo kuliko yale ya mtoni.
iii) Chache
- Vikombe ni vichache kuliko vibakuli.
- Vibakuli ni vichache kuliko sahani.
Lafu kubadili mpangilio wa herufi na silabi.
(Mila-lami, lima, mali) ili kukuza msamiati.
Kuunda maneno kutokana na neno "unda" yaani tengeneza, umbo kitu. Uundaji wa maneno ni kuzalisha maneno mapya. Uundaji huu hupanua msamiati wa lugha. Kuunda maneno huwezesha lugha kukidhi mahitaji ya mawasiliano. Uundaji wa maneno pia husababishwa na mabadiliko ya mandeleo na sayansi na teknolojia. Hivyo hufanya lugha kuhitaji maneno ili yaweze kutumiwa na jamii, mfano, laptop inaitwa kipakatalishi. Calculator - kikokotozi.
Njia mojawapo inayotumika kuunda maneno ni njia ya kubadili mpangilio wa herufi au silabi.
Maneno mengi hupatikana kwa kubadili mpangilio wa herufi au silabi, mfano:-
Lima - neno hili lina herufi nne na lina silabi mbili
Herufi za lima ni l-i-m-a
Silabi za lima ni li-ma
Lima - mali, mila, lami
Tiba - neno hili lina herufi nne na silabi mbili
Herufi za tiba ni t-i-b-a
Silabi za tiba ni ti-ba
Tiba - bati, bata
Mwalimu
Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.
Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.
Ingia ili kuuliza