Mada za sehemu hiiVitendawiliMada 3
- Muundo wa vitendawili
- Sifa za vitendawili
- Umuhimu wa vitendawili
Vitendawili
Vitendawili ni tungo au semi fupifupi zilizofumbwa na hutumia lugha ya picha kuelezea wazo lililofichika. Kitendawili uhusisha watu wawili yaani mtegaji na mteguaji.
Muundo wa vitendawili
- Kitendawili (mtegaji) — swali au kile anachosema mtegaji
- Tega (mteguaji) — jibu la kitendawili
Kwa mfano:
- Popo mbili zavuka mto — Kitendawili (mtegaji)
- Macho — Tega (mteguaji)
Ikiwa mteguaji amekosa jibu hupaswa kumchagua mji mtegaji na mtegaji akiridhika na mji aliopewa hutoa jibu la kitendawili alichotega.
Vitendawili huundwa kwa taswira na tamathali za semi
- SITIARI — Nyumba yangu ndogo lakini wapangaji wengi — kiberiti
- DHIHAKA — Kitu kidogo kimemtoa mfalme kitini — haja
- TANAKALI — Huku pi na kule pi — mkia wa kondoo anapotembea
- TASWIRA — Babu yangu kalala kaacha ndevu nje — muhindi
- TASHIHISi — Popo mbili zavuka mto — macho
Mwalimu
Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.
Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.
Ingia ili kuuliza