Sonzaschool
Rudi

Sekondari ya Juu · Kidato cha Tano

Kiswahili 1

Utumizi wa lugha

takriban dakika 3 kusoma

Mada za sehemu hiiMatumizi Ya LughaMada 5

Utumizi wa Lugha

  1. Matumizi ya lugha ni namna ya kutumia lugha kulingana na mila, desturi na taratibu zilizopo katika jamii husika.

  2. Ni jinsi ambavyo mzungumzaji anatunza lugha kwa kuzingatia uhusiano wake na yule anayezungumza naye.

  3. Matumizi ya lugha hutegemea mambo kadhaa kama vile:

    • Uhusiano baina ya wazungumzaji
    • Mada inayozungumzwa
    • Mazingira waliyemo wazungumzaji n.k

Umuhimu wa matumizi ya lugha

  1. Kuwasaidia watumiaji wa lugha kutumia lugha kwa ufasaha
  2. Kumsadia mzungumzaji kuweza kutambua kutofautiana na kutumia mitindo mbalimbali ya lugha

Mtindo wa lugha

  1. Mtindo wa lugha ni mabadiliko yanayojitokeza katika kutumia lugha, mabadiliko ya lugha katika mitindo mbalimbali yaani mitindo mbalimbali ya lugha.
  2. Kwa kawaida mtindo wa lugha / mabadiliko katika kutumia lugha ndiyo inayomwongoza mzungumzaji katika kuelewa maneno na mitindo ya tungo.

Matumizi katika lugha hutawaliwa na mambo yafuatayo:

  1. Uhusiano baina ya wazungumzaji
  2. Mada ya mazungumzo
  3. Lengo au madhumuni ya mazungumzo
  4. Sifa za wazungumzaji
  5. Jinsi mazungumzo yanavyofanywa
  6. Utanzu wa mawasiliano

Mazingira / Muktadha

  1. Ni wazi kwamba wazungumzaji huzungumza wakiwa katika mazingira fulani yanayotawala katika maisha yao ya kila siku.
  2. Mazingira hayo yanaweza yakawa ya hotelini, shuleni, ofisini, mahakamani na n.k

Uhusiano baina ya wahusika

  1. Uhusiano baina ya wahusika huathiri mtindo wa uzungumzaji katika lugha.

  2. Mzungumzaji atatumia lugha kwa kutegemea anaongea na nani, na kutokana na sababu hiyo tunapata:

    • Lugha ya baba na mtoto
    • Watu wa rika moja
    • Mtu na mpenzi wake
    • Mtu na mwanafunzi wake
    • Mfanyakazi wa kawaida na mkuu wake wa kazi n.k

Mada ya mazungumzo

  1. Kimsingi mada ya mazungumzo hutawala usemaji na namna ya uzungumzaji kwa ujumla

  2. Kutokana na mada ya mazungumzo tunapata lugha ya:

    • Kibiashara
    • Kitaalamu
    • Kitabibu
    • Kitaaluma
    • Kisiasa n.k

Madhumuni ya mazungumzo

  1. Wakati mwingine mitindo wa lugha hutawaliwa na madhumuni ya mazungumzo

  2. Kutokana na madhumuni ya mazungumzo, uzungumzaji utategemea:

    • Mazingira
    • Uhusiano baina ya wahusika
    • Mada ya mazungumzo

Jinsi mazungumzo / mawasiliano yanavyozungumzwa

  1. Namna mawasiliano yanavyofanyiwa inaweza kuathiri mtindo wa uzungumzaji

  2. Mawasiliano yanaweza kufanywa kwa njia ya:

    • Maandishi
    • Mazungumzo ya mdomo
    • Simu
    • Televisheni
    • Redio
  3. Njia hizi huathiri mtindo wa uzungumzaji

Utanzu wa mawasiliano

  1. Mtindo wa uzungumzaji unaweza kuathiriwa pia na utanzu wa mawasiliano

  2. Yaani kama ni:

    • Hotuba
    • Majadiliano
    • Masimulizi
    • Mazungumzo ya kawaida
    • Maelezo
  3. Vitathiri mtindo wa uzungumzaji

Sifa ya mzungumzaji

  1. Wakati mwingine mtindo wa lugha huathiriwa na sifa za wazungumzaji

  2. Sifa hizo zinaweza kuwa:

    • Kiwango cha elimu
    • Cheo
    • Uwezo wa kipato
    • Heshima ya mtu katika jamii n.k

Mwalimu

Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.

Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.

Ingia ili kuuliza