Mada za sehemu hiiMatumizi Ya LughaMada 5
Rejesta
Ni mtindo wa lugha ambayo hutumika mahali penye shughuli fulani, mf: hotelini, shuleni, hospitali, kanisani nk.
Aina za Rejesta
Kuna aina mbalimbali za rejesta kulingana na mahali au shughuli inapofanyika.
-
Rejesta za hotelini: Huu ni mtindo utumikao hotelini mf: Naniwali kuku? Chai moja chapati moja
-
Rejesta za mitaani Ni mazungumzo yatumiwayo na aina fulani ya watu katika magenge, vijiweni na hueleweka na watu au wahusika wenyewe. Mf: mshikaji-rafiki, Demu-msichana, umenoa- umekosa, dili maiti - mpango usiofanikiwa.
-
Rejesta za hospitalini Ni lugha itumiwayo na manesi, madaktari na wagonjwa hospitali. Lengo lake ni kupunguza muda kuwashughulikia wateja wengi. mf: kutwa mara tatu yaani kunywa kimoja asubuhi, mchana na jioni.
-
Rejesta kanisani Ni lugha ya mahubiri. Sifa yake kubwa haibadiliki. mf: Mapendo – daima, Bwana yesu asifiwe – Amina. Msikitini, mf: Asalam aleikum – Aleikum asalaam
-
Rejesta mahakamani Mtindo huu hutumika mahakamani. Mf: Mheshimiwa hakimu, Mtuhumiwa, kesi nk.
Dhima za Rejesta
-
Hutumika kama kitambulisho kwa wazungumzaji Mtu huweza kutambua shughuli baada ya kusikia lugha itumikayo. Mtindo wa sokoni ni tofauti na mahakamani hivyo hutambulisha wazungumzaji.
-
Hutumika kurahisisha mawasiliano kwa kupunguza muda wa kuhudumia mf: Hotelini kama wateja wengi, Naniwali samaki?, Chai wapi?
-
Hukuza lugha Msamiati wa lugha huongezeka kupitia rejesta. mf: dawa mpya – ikimaanisha dawa za kupunguza makali ya ukimwi.
-
Huficha jambo kwa wasiohusika mf: Daktari amuandikiapo majibu mgonjwa sio rahisi mtu asiye katika kada hiyo kuelewa. Mf: BS – kupima malaria Stool – kupima choo Inj – Sindano 5/7 – kunywa dawa kwa siku 5 katika wiki
-
Hupamba lugha Mikato ya maneno katika rejesta inapamba lugha. mf: Wali kuku, wapi mkia
-
Hutumika kupunguza ukali wa maneno mf: Kujifungua – kuzaa
Mwalimu
Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.
Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.
Ingia ili kuuliza