Mada za sehemu hiiMaendeleo Ya KiswahiliMada 3
- Nadharia kuhusu chimbuko la kiswahili
- ushahidi wa kihistoria
- Ukuaji na ueneaji wa kiswahili duniani
Chimbuko la Kiswahili
Nadharia hii inazungumzia kuhusu mahali hasa ambapo lugha ya Kiswahili ilichipukia. Wataalam wa lugha ya Kiswahili wanatofautiana kuelezea mahali hasa ambapo ndiyo chimbuko la lugha ya Kiswahili ilichipukia Kaskazini, Mashariki mwa Kenya na ilitokana na Kingozi na kuna wengine wanadai kuwa Kiswahili chimbuko lake ni Bagamoyo mpaka Mzizima, eneo lililojulikana kama Dar es Salaam hadi Kilwa. Wataalam hawa wanadai lugha ya Kiswahili ilienea kama Kishomvi. Madai ya wataalamu hawa hayajawahi kuthibitishwa kwa hoja makini na tafiti zinaonesha kwamba madai hayo hayana ukweli yanahitaji tafiti zaidi. Kwa ujumla madai haya yanaweza kuwekwa kwenye mchoro kama ifuatavyo:
| KIONGOZI | KISWAHILI | |
|---|---|---|
| KENYA | KIONGOZI | KISWAHILI |
| TANZANIA | KISHOMVI | KISWAHILI |
NB: Kuna kundi la wataalamu wengine linalodai kuwa chimbuko lake ni sehemu mbalimbali za Pwani ya Afrika Mashariki. Mfano mtaalamu Freeman Grenvill katika makala yake inayoitwa Medieval For Swahili (1959) anadai kuwa lugha ya Kiswahili ilianza na kuinuka katika upeo wote wa Afrika Mashariki kama ambavyo baadhi ya maneno, majina ya watawala na maofisa wa serikali yanavyojitokeza katika fasihi.
Madai ya mtaalamu huyu yanaashiria kwamba watu walioishi katika maeneo mbalimbali ya upande wa Afrika Mashariki walikuwa wakizungumza lugha zao mbalimbali. Lugha zote hizi zilikuwa za kibantu na hazikutofautiana sana.
Watu hawa katika kuwasaidia hasa katika biashara walilazimika kurahisisha lugha zao kwa kiasi fulani ili waweze kuwasiliana na miongoni mwao. Urahisishaji huo wa lugha na kuzuka kwa lugha hiyo kubwa ni jambo lililotokea katika sehemu zote za upwa wa Afrika Mashariki. Matokeo yake kulizuka lugha ambazo zilijulikana kama lahaja za Kiswahili. Lahaja hizo zilizungumzwa kutoka kusini mwa Somalia hadi Kaskazini-mashariki mwa Msumbiji.
Hapo tunapata lahaja kama vile kitikwa, Kiamu, Chichifundi, Kimvita, Kimombasa, Kimtang'ata, Kimakunduchi, Kihadimu, Kitumbata na Kipemba. Lahaja hizo zinafanana zaidi na lugha mbalimbali za kibantu kuliko zinavyofanana na Kiswahili sanifu kwa kuwa Kiswahili sanifu kina maneno mengi ya mkopo.
Maswali
- Kwa kutumia hoja madhubuti fafanua chimbuko la lugha ya Kiswahili.
- Wanadai kuwa Kiswahili ni Kiarabu, wanahoja kubwa kuu tatu. Fafanua hoja hizo.
- Kiswahili ni Kiarabu kwa jina lake, lakini ni Kibantu kwa asili yake, thibitisha kwa hoja za kiisimu.
Lugha Mama (Lugha ya Kwanza), Lugha Yapili na Lugha Rasmi
Lugha rasmi ni ipi?
Ni lugha inayoteuliwa na serikali ili itumike katika shughuli za kiserikali. Kiswahili Tanzania ni lugha ya taifa pia ni lugha rasmi.
Sifa za lugha rasmi
- Yaweza kuwa lugha sanifu au isiwe sanifu lakini pia yaweza kuwa fasaha au isiwe fasaha.
- Inaweza ikawa lugha ya taifa au isiwe lugha ya taifa.
- Huwa haifuati kabila wala mchanganyiko wa makabila yaliyopo nchini.
- Yaweza kuwa lugha ya kigeni kama vile kiingereza, Kifaransa, Kichina.
- Hutegemea utawala uliopo madakarani.
Lugha Mama (Lugha ya Kwanza)
Ni lugha ambayo mtu hujifunza utotoni baada tu ya kuzaliwa, kabla ya kujifunza lugha ya pili. Mtoto hujifunza lugha hii kwa kusikiliza kutoka kwa wazazi au majirani. Lugha hii ni rahisi kujifunza kulingana na ya pili kwa sababu zifuatazo:
- Mtoto huwa na muda mrefu wa kujifunza (usio koma)
- Mtoto hujifunza lugha katika mazingira halisi, mfano vile anavyojifunza vipo pale pale.
- Uhusiano wa mtoto na wanaomzunguka kuwa mzuri.
- Kuna kuwa na msaada wa kutosha katika kujifunza.
- Kuna kuwa na uzoefu katika lugha hiyo hiyo moja.
Dhima ya lugha ya kwanza
Kukidhi haja ya mawasiliano kwa watu wanaomzunguka mtoto.
NB: Lugha ya kwanza inaweza kuwa lugha ya pili kwa watu wengine na lugha ya pili inaweza kuwa ya kwanza kwa watu wengine. Mfano: Kiswahili ni lugha ya kwanza kwa Watanzania wote waliozaliwa mjini lakini yaweza kuwa lugha ya pili kwa Watanzania waliozaliwa vijijini.
Lugha ya pili
Ni lugha ambayo mwanadamu hujifunza baada ya kujifunza lugha ya kwanza. Mara nyingi lugha ya pili huwa na athari ya lugha ya kwanza kuhusishwa na mazingira ya lugha ya pili. Kwa Watanzania walio wengi hasa waliozaliwa kijijini Kiswahili ni lugha yao ya pili.
Matumizi ya lugha ya pili
- Kutaka kukidhi haja ya mawasiliano kwa jamii ambazo si wazungumzaji wa lugha ya kwanza.
- Kutaka kujihusisha na jamii inayozungumza lugha hiyo ya pili.
Mfano: tunajifunza Kiingereza ili kujihusisha na jamii nyingine.
Mwalimu
Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.
Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.
Ingia ili kuuliza