Mada za sehemu hiiMaendeleo Ya KiswahiliMada 3
- Nadharia kuhusu chimbuko la kiswahili
- ushahidi wa kihistoria
- Ukuaji na ueneaji wa kiswahili duniani
USHAHIDI WA KIHISTORIA
Licha ya ushahidi wa kiisimu, pia kuna ushahidi wa kihistoria unathibitisha kuwa Kiswahili ni Kibantu. Ushahidi huo unathibitishwa na wageni mbalimbali waliofika Afrika Mashariki na kudhihirisha kuwa Kiswahili kilizungumzwa Pwani ya Afrika Mashariki kabla ya ujio wa wageni.
Ushahidi huu ulitolewa na wageni mbalimbali waliofika Afrika ya Mashariki na kuthibitisha kuwa kabla ya kufika kwao, Kiswahili kilizungumzwa. Wageni hao ni kama wafuatao:
-
Ushahidi wa Marco Pollo Ni mwanataaluma wa Kizungu aliyejishughulisha na masuala mbalimbali ya Kijiogragia na kusafiri sehemu nyingine duniani. Katika moja ya maandiko yake, anasema hivi; "Zanzibar ni kisiwa kilicho kizuri ambacho kinamzunguko wa maili 200" Watu wake wanaabudu Mungu. Wana mfalme na wanatumia lugha yao na hawalipi ushuru kwa mtu. Nukuu hii imenukuliwa kutoka kitabu cha "SAFARI ZA MARCO POLLO" (1958 – 301). Pia katika kitabu chake cha Kijiografia ambacho hakikuchapishwa lakini kimetafsiriwa kwa Kirusi na Kifaransa lakini kina maneno kama vile; Ungudya ambako sasa ni Unguja. Zanguaba ambako sasa ni Zanzibar. Maneno mengine ni kama; kundi, firi, Omani, Murijani, na kisuka. Haya ni majina ya aina mbalimbali za ndizi zilizopatikana Zanzibar.
-
Ushahidi wa Al – Masoud (915 BK) Katika moja ya maandishi yake anazungumzia juu ya wakazi wa mwambao ambao walijulikana kwa jina la Waenji. Kwa dhana hii neno Zanzibar linatokana na neno Zanjibar, yaani pwani ya Zanji. Al – Masoud anaonesha kwamba, Wazanji walikuwa na watawala kwa nguvu za Mungu. Viongozi hawa walikuwa wacha Mungu, Huenda neno Wakitumia / ina maana ya wafalme. Anasisitiza kuwa walisema lugha fasaha na walikuwa na viongozi walio hutubia kwa lugha yao. Kutokana na neno Zanji inawezekana kabla ya kuja kwa waarabu, Kiswahili kilikuwa Kizaramo au Kizanji.
-
Historia ya Kilwa Kimsingi habari hizi zinaeleza historia ya Kilwa, karne ya 10 mpaka 16 BK na zinahusiana na kutaja majina ya utani kama vile Mkoma watu, Nguo nyingi n.k Ambayo walipewa Masultan wa kwanza wa Kilwa ambao ni Ali Ilbin Hussein na mwanawe. Mohamed Ibin Ali kutokana na habari hizi huenda lugha ya Kiswahili ilianza kuzungumzwa kuanzia karne ya 10 au 11. Maelezo ya kihistoria yanaeleza juu ya Sultani aliyeitwa Talt Ibin Al – Hussein aliyepewa jina la utani Hasha haefiki.
-
Ushahidi wa Ibin Batuta (14 BK) Mohamed Bin Abdallah Ibin Batuta ana asili ya kiarabu alifika Afrika Mashariki kunako mwaka 1331 BK, Katika maandishi yake anaeleza maisha ya watu wa nchi ya Afrika Mashariki ingawa yeye aliita nchi ya Waswahili. Anataja miji kama vile Mogadishu, na Kilwa. Alisema, "Basi nilianza kusafiri baharini kutoka Mogadisho kwenda nchi ya Waswahili na Kilwa ambao umo katika nchi ya Zanji. Tulifika Mombasa kisiwa kikubwa, mwendo wa siku mbili kutoka nchi ya waswahili, Watu hawajishughulishi na kilimo ingawa huagiza nafaka toka kwa waswahili."
-
Maandishi ya Morrice Maandishi haya yalijitokeza mwaka 1779, Katika maandishi hayo Morrice anawagawa watu wa Afrika Mashariki katika makundi matatu, ambayo ni waarabu, wasuriana na waafrika. Anasisitiza kuwa masuriana na waafrika walishakaa na kuwa kundi moja. Wakaelewana na kusema lugha moja ya kisuriana. Kuna kuwa huenda kisuriana ndicho Kiswahili cha leo.
-
Ugunduzi wa Ali Idris Ugunduzi huu ulifanywa huko Sicily mwaka 1100 mpaka 1166 BK kwenye mahakana ya mfalme Roger II, Katika ugunduzi huu ilisadikika Kiswahili kiliandikwa kabla ya karne ya 10 BK. Al Idrisi alikuwa wa kwanza kugundua jina la zamani la Zanzibar kuwa ni Ungudya. Katika maelezo yake anaandika pia majina ya aina za ndizi mbalimbali zilizopatikana huko Ungudya kama vile kikombe, mkono wa tembo, sukari, na muriani.
-
Vitabu vya Periplus na Yu – Yanga Tsa - Tsu:-
- Kitabu cha Periplus: Hiki kinahusu mwongozo wa bahari ya Hindi na inasadikika kuwa kiliandikwa karne I katika mji wa Alexander. Kitabu hiki kinataja habari za Azania yaani Afrika Mashariki na habari za vyombo vya baharini kama vile ngalawa, madema na mitepe. Kitabu hiki kinaeleza kuwa watu wageni hutozwa ushuru na wafanyabiashara wenyeji na wanaijua pia lugha ya wenyeji vizuri.
- Kitabu cha Yu- Yanga Tsa - Tsu: Kitabu hiki kinaeleza habari za upwa wa Afrika Mashariki na shughuli mbalimbali za Wachina hapa Afrika mashariki.
- Chu – Fan – Chi: Kilichapishwa 1226 na kinaeleza bahari za Zanzibar na shughuli mbalimbali za Wachina hapa Afrika Mashariki.
-
Ushairi wa Kiswahili
- Utenzi wa Fumo Lyongo: Hili ndilo shairi la zamani kabisa. Lilipata kuandikwa katika lugha ya Kiswahili na inasemekana liliandikwa karne ya 13 BK. Uwepo wa shairi hili unadhihirisha kuwepo kwa Kiswahili kabla ya hapo. Huenda kilitumika kabla ya karne ya 10 BK.
Mwalimu
Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.
Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.
Ingia ili kuuliza