Sonzaschool
Rudi

Sekondari ya Juu · Kidato cha Sita

Kiswahili 2

Nadharia kuhusu chimbuko la kiswahili

takriban dakika 10 kusoma

Mada za sehemu hiiMaendeleo Ya KiswahiliMada 3

Neno asili lina maana kuwa jinsi kitu au jambo lilivyotokea au lilivyoanza na tunapozungumzia asili ya lugha ya Kiswahili ina maanisha tunachunguza namna lugha hiyo ilivyoanza. Wataalamu mbalimbali wa lugha wamefanya uchunguzi juu ya asili ya lugha ya Kiswahili. Uchunguzi huo umejenga nadharia mbalimbali zinazoelezea chimbuko la lugha ya Kiswahili. Kwa ujumla historia kuhusu asili ya lugha ya Kiswahili ina matatizo mengi na ndiyo maana kuna nadharia mbalimbali zinazoelezea juu ya asili ya lugha ya Kiswahili.

Miongoni mwa matatizo yanayoikabili historia ya Kiswahili ni pamoja na:

  1. Hakuna uthibitisho kamili juu ya nadharia zinaelezea asili ya lugha ya Kiswahili na kuenea kwake.
  2. Uchunguzi wa asili ya Kiswahili ulifanywa na wataalamu wa kizungu ambao waliandika historia ya Kiswahili jinsi walivyoelewa wao baada ya kupata ushahidi kidogo tu.
  3. Wazawa hawakushirikishwa ipasavyo katika uchunguzi wa lugha ya Kiswahili.
  4. Hapakuwa na kumbukumbu za kutosha kwa sababu babu zetu hawakujua kusoma wala kuandika hivyo basi kuna upungufu wa kumbukumbu.

Kutokana na matatizo hayo yanayoikabili historia ya Kiswahili kuna nadharia mbalimbali zinazoelezea historia ya lugha ya Kiswahili. Nadharia hizo ni kama vile:-

  • Kiswahili asili yake Kongo
  • Kiswahili ni kundi au pijini
  • Kiswahili ni lugha ya vizalia
  • Kiswahili ni Kiarabu
  • Kiswahili ni Kibantu

Mwalimu

Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.

Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.

Ingia ili kuuliza