Sonzaschool
Rudi

Msingi · Darasa la Nne

Kiswahili

Matumizi ya Msamiati Katika Mazungumzo

takriban dakika 1 kusoma

Mada za sehemu hiiKuwasiliana Katika Miktadha MbalimbaliMada 4

Majina ya Vinywaji

Vinywaji visivyo na vilevi

Faida

  • Maji

    • Hukata kiu
    • Husaidia kuyeyusha chakula mwilini
    • Ni sehemu ya uhai
  • Maji ya matunda (juisi)

    • Hukata kiu
    • Hutibu magonjwa
    • Huwafaa watoto na wagonjwa
  • Soda

    • Hutuliza kiu
    • Huongeza sukari mwilini

Hasara

  • Vinywaji vyenye sukari nyingi vina madhara mwilini mwetu
  • Huongeza sukari isiyotakiwa mwilini

Tahadhari

Vinywaji vyenye sukari nyingi yatupasa kuvinywa kwa tahadhari

Vinywaji vyenye kilevi (Pombe)

(a) Pombe za kienyeji

  • Wanzuki
  • Mbege
  • Dengelua
  • Mnazi
  • Ulanzi

Faida

  1. Huwa na lishe kidogo
  2. Hutengenezwa na nafaka (baadhi)
  3. Hutuliza kiu
  4. Huwaburudisha wanywaji

Hasara

  1. Nyingi huwa chafu zikiandaliwa vibaya
  2. Husababisha magonjwa kama kuhara
  3. Hupoteza pesa kwa walevi
  4. Kudhoofisha afya ya mnywaji
  5. Mlevi huweza kupungua uzito akinywa sana gongo

(b) Pombe za viwandani

  • Bia
  • Wiski
  • Konyagi
  • Kilimanjaro

Faida

  1. Hutuliza kiu
  2. Hutumika kuburudisha wanywaji
  3. Hutumika kuwaweka watu pamoja

Hasara

  1. Hutumia pesa nyingi
  2. Hudhoofisha afya
  3. Huchangia kuongeza uzembe
  4. Walevi wanaweza kupata kisukari

Mimea katika Mazingira Yetu

  1. Miti ya matunda
  2. Miti ya mapambo na kivuli
  3. Mimea ya maua
  4. Mimea ya mbogamboga

Mti wa kivuli na mimea ya maua

Faida za mimea

  1. Hutupatia kivuli
  2. Hutupatia hewa safi
  3. Hutupatia dawa
  4. Hutupatia Chakula

Nyakati

Nyakati zimegawanyika katika sehemu kuu tatu ambazo ni:-

  1. Wakati uliopita
  2. Wakati uliopo
  3. Wakati ujao
WakatiSilabi ya wakatiTendo
Uliopita-li-Tulikula, Alikula
Uliopo-na-Tunakula, Wanakula
Ujao-ta-Tutakula, Watakula

Kutunga sentensi za wakati uliopita

Tutatumia —li-

  1. Juma alifundishwa kusoma
  2. Mama alipika pilau tamu sana
  3. Juzi tulikula wali na kisamvu
  4. Asubuhi niliamshwa mapema
  5. Babu alifurahi alipotafuna bisi
  6. Dada alinunua nyanya gengeni

Mwalimu

Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.

Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.

Ingia ili kuuliza