Sonzaschool
Rudi

Msingi · Darasa la Nne

Kiswahili

Matumizi Ya Msamiati Katika Maandishi

takriban dakika 3 kusoma

Mada za sehemu hiiKuwasiliana Katika Miktadha MbalimbaliMada 4

Hadithi ya ndege

Hapo kale ndege waliishi porini, ndege hao walioishi porini ni tausi, tai, flamingo, kangaroo, kanga, chiriku, mbuni na kasuku. Wote hao walikuwa wanaishi porini. Kuku, bata, njiwa na kware makazi yao yalikuwa kwenye vichaka, miti, nyasi na porini.

Siku zilipita maisha yakaanza kuwa magumu sana. Wadudu walianza kupungua, mazao shambani yakakauka, majani yakakauka kutokana na ukame. Ndege wengi walikufa waliobaki walidhoofu.

Siku moja kuku aliwakusanya ndege wote, akasema ndugu zangu ninashukuru kwa kuja. Lengo la wito ni kuwaasa kuwa kutokana na hali ilivyo inatubidi tukajisalimishe kwa binadamu. Huenda akatupa hifadhi, chakula na kuweza kutunusuru maisha yetu na watoto wetu.

Mbuni alidakia hoja we kuku vipi? Unataka twende kwa binadamu akatufanye kitoweo? Hapana siendi, bundi nave akadakia hata mimi siendi kunguru akacheka kwa! Kwa! Kwa! Yaani bundi huendi unaogopa nini wakati mimi na wewe hatumpati binadamu?

Bata, Kware na Njiwa wao wakasema wataenda hivyo hivyo kama kufa na tufe tu. Mabishano yaliendelea na mwisho kuku akatumwa aende akatafute kwanza kisha arudi kuwapa wenzake jibu. Kuku hakurudi, basi kanga akasema na mimi namfuata nitajua kama ametusaliti ama kunajanga limempata. Hivyo basi kanga alienda anamuita kuku wee! Kuku wee! Kuku wee! Mpaka leo. Ikafika zamu ya mwewe kumfuata akakuta watoto wa kuku wamenenepa mno! Loo! L'roho ukamshika akaanza kuwawinda mpaka leo.

Bundi akasema, nitakwenda usiku, nitakaa kwenye paa ya nyumba ya binadamu nimtishe akimbie mpaka leo bundi hajafanikiwa

Majina mengine ya ndege ni:

  1. Bata
  2. Bata mzinga
  3. Chiriku
  4. Bundi
  5. Kware
  6. Kuku
  7. Kunguru
  8. Mbuni
  9. Kasuku
  10. Tai
  11. Tausi
  12. Korongo
  13. Flamingo

Mwalimu

Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.

Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.

Ingia ili kuuliza