Mada za sehemu hiiMjengo Wa TungoMada 3
- Aina za tungo
- Virai
- vishazi
Kishazi ni tungo yenye kitenzi. Kitenzi hicho kinaweza kuwa kinachojitosheleza na hapo huitwa kishazi huru au kikuu, au inaweza kuwa kitenzi kinachojitegemea na hivyo huitwa kishazi tegemezi. Kishazi ni tungo yenye kitenzi ambacho kinaweza kujitosheleza na kukamilisha ujumbe uliokusudiwa na mzungumzaji au kuwa na kitenzi kisichoweza kutegemea kingine.
Kuna aina mbili za vishazi:
- Vishazi Huru
- Vishazi Tegemezi
Kishazi Huru
Ni kishazi kinachotawaliwa na kitenzi kikuu ambacho kwa kawaida hutoa ujumbe uliokamilika usiohitaji maelezo zaidi ya kukamilisha maana. Pia, maana kamili yaweza kupatikana hata kama vishazi tegemezi vikifutwa katika sentensi zinazohusika. Vishazi huru vyaweza kuwa kabla au baada ya vishazi tegemezi.
Mfano:
- Watoto wazuri wanakimbia.
- Mama anapika chakula.
- Asha naye mpumbavu.
Kishazi Tegemezi
Ni kishazi kinachotawaliwa na kitenzi kisaidizi ambacho kwa tabia yake hakikamilishi ujumbe uliokusudiwa bali hutegemea kitenzi kikuu kuweza kutoa ujumbe uliokusudiwa.
Mfano:
- Mzee aliyekuja jana.
- Mbwa aliyepata kichaa.
- Nyumbu aliyepigwa risasi.
-
Kishazi tegemezi hakitoi maana kamili ikiwa hakijaambatana na vishazi huru. Mfano: Somo lililoanza asubuhi. Mtoto aliyekuja jana.
-
Vishazi tegemezi vinaweza kufutwa katika sentensi bila ya kuharibu maana kamili ya sentensi nzima. Mfano: Mtoto aliyekuja jana amekwenda sokoni. (Kirai tegemezi 'aliyekuja jana' kinaweza kufutwa na sentensi kuendelea kama: Mtoto amekwenda sokoni.)
-
Vishazi tegemezi aghalabu vinaweza kutambulika kwa kuwa na viambishi rejeshi. Mfano: Aliyekuja jana ameondoka. Kitabu kilichopotea juzi kimeonekana.
-
Vishazi tegemezi vinaweza kutambulika kwa kuwepo vishazi tegemezi kama vile: kwamba, ingawa, ili, kwa sababu, mpaka na vingine vingi. Mfano: Hamisi anasema kwamba watoto wengi wamekuwa wahuni. Tumeingia shuleni ili tupate elimu.
-
Vishazi tegemezi vinaweza kutanguliwa au vikafuatiwa na vishazi huru. Mfano: Nilimuona Rehema nilipokwenda sokoni. Utakuja nyumbani leo, kufuatana na ndugu yako.
Vishazi tegemezi vinaweza vikawa na tungo kama hizi:
-
Tungo zenye viambishi rejeshi vya viwakilishi nafsi au viambishi ngeli vilivyoambatanishwa ndani ya kitenzi au mwisho Mfano: Anayevunja sheria lazima aadhibiwe haraka. Kilichopotea sikijui. Miti iliyoanguka imeibiwa pande hizi.
-
Tungo zenye kueleza mahali, wakati, masharti au kasoro, na sababu (Vishazi Tegemezi Vielezi - E) Mfano: Ninamolala mna kunguni wengi. Alipoondoka walifika wageni. Ukija nitakupa hicho kitu. Japokuwa inanyesha mvua nitatoka nje hivi punde.
-
Vishazi vyenye vitenzi vinavyoanza na kiambishi Ku- vilivyoambatana na maneno mengine Mfano: Saidi hataki kununua matunda sokoni. Kukaa tu, akatokea mjomba wangu. Kuulizwa tu, wakataka kuondoka.
-
Kishazi huru kina hadhi ya sentensi (sentensi sahihi), lakini kishazi tegemezi hakina hadhi hii.
-
Vishazi tegemezi ambavyo hutegemezwa kwenye vishazi vingine katika tungo, ambavyo huwa kwa kawaida ni dhima ya kikundi au neno.
-
Vishazi hivyo huvumisha nomino iliyoko kwenye tungo hiyo.
Mfano:
- Askari walioenda vitani wamepewa mshahara.
- Shule iliyofunguliwa kijijini imepata walimu.
Vishazi tegemezi vingine hufanya kazi ya vielezi viwapo katika tungo, sawa na vikundi vielezi.
Kutokana na hali hii, vishazi huru navyo huwa pia vimehusishwa hadhi, kwani vimeteremka daraja kutoka kishazi na kuwa sawa na kikundi ambacho kwa kawaida kina hadhi ndogo kuliko kishazi.
Mfano:
- Juma alipigwa, alipoiba mahindi.
- Watoto walikimbia alipowaona.
Mwalimu
Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.
Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.
Ingia ili kuuliza