Mada za sehemu hiiMjengo Wa TungoMada 3
- Aina za tungo
- Virai
- vishazi
Tungo kirai (kikundi)
- Kirai: ni tungo isiyo na muundo wa kiima na kiarifu, au ni kipashio cha kimuundo chenye neno moja na kuendelea lakini ambacho hakina muundo wa kiima na kiarifu.
- Kirai si lazima kiwe na kitenzi, na kwa kawaida kirai ni kikubwa kuliko neno, lakini ni kidogo zaidi ya kishazi.
- Katika kiwango hiki, miundo ya tungo huhusisha maneno mawili au zaidi, ambayo huwekwa pamoja katika mpangilio maalumu unaozingatia uhusiano uliopo baina ya neno kuu na maneno mengine.
Aina za virai
Kirai nomino (KN)
Kirai kinachotawaliwa na nomino au mahusiano ya nomino na neno au mafungu ya maneno.
Muundo wa kirai nomino ni kama ifuatavyo
- Nomino peke yake: Mfano: Baba analima. Juma anasoma.
- Nomino mbili au zaidi zinazounganishwa: Mfano: Juma na Ali wanacheza mpira. Kaka na dada wanaenda sokoni.
- Nomino na kivumishi (N + V): Mfano: Mwalimu hodari ameandaa somo. Mtoto mzuri anacheza.
- Kivumishi na nomino (V + N): Mfano: Wale wazee wameondoka.
- Kiwakilishi peke yake: Mfano: Mimi ninasoma kitabu. Wewe unaumwa malaria.
- Nomino na kitenzi jina: Mfano: Kilimo cha kufa na kupona kimezingatiwa. Kucheka kwa fisi hakunitishi.
Kirai kitenzi (KT)
Kirai ambacho kimekitwa katika kitenzi au katika uhusiano wa kitenzi na neno au mafungu mengine ya maneno. Kirai kitenzi kimeundwa na vipashio vifuatavyo:
Miundo ya kirai kitenzi:
- Kitenzi peke yake (T): Mfano: Analima, anapika.
- Kitenzi + jina na kielezi: Mfano: Anamfundisha mtoto vizuri. Wanasoma kivivu.
- Kitenzi kisaidizi kimoja au zaidi na kitenzi kikuu (Ts + Ts + T/Ts + T): Mfano: Alikuwa analima. Alikuwa anataka kulala.
- Kitenzi kishirikishi + Nomino (shamirisho): Mfano: Ni mpole. Ndiye shujaa.
Kirai kielezi (KE)
- Miundo yake hailekei kukitwa kwenye mahusiano baina ya neno kuu (kielezi) na neno au fungu la maneno linaloandamana nacho.
- Badala yake, miundo inayohusika hapa ni ya maneno ambayo hufanya kazi pamoja katika lugha.
Mfano ya kirai kielezi:
- Wanafunzi wanaandika vizuri.
- Alitembea polepole sana.
Kazi kubwa ya miundo hii katika sentensi:
- Kueleza wakati, mahali, jinsi na kinachofanya tendo lifanyike.
- Tofauti na virai vingine, nafasi yake ndani ya sentensi huwa ni ya kudumu.
- Virai vielezi huweza kushika nafasi mwanzoni mwa sentensi au baada ya kitenzi.
Mfano:
- Juma alikuja jana jioni.
- Jana jioni, Juma alikuja.
Kirai kihusishi (KH)
Kirai ambacho muundo wake umekitwa katika mahusiano baina vihusishi hivi; kwa, na, katika, au na fungu la maneno linaloandamana nalo. Katika kirai kihusishi, neno kuu ni kihusishi katika Kiswahili.
Muundo wa KH ni mmoja tu, nao ni kihusishi na kikundi nomino.
Mfano:
- Kwa amri ya jeshi.
- Mwizi amekamatwa na polisi.
- Amekwenda kwa kaka yake.
Mwalimu
Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.
Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.
Ingia ili kuuliza