Mada za sehemu hiiUhakiki Kazi Za Fasihi AndishiMada 3
- Uhakiki kazi za fasihi andishi
- Vipengele vya fani na maudhui katika kazi za fasihi andishi
- Vipengele vya fani
Maudhui katika kazi ya fasihi ni jumla ya mawazo yote yanayozungumziwa pamoja na mtazamo wa mwandishi juu ya mawazo hayo. Maudhui hujumlisha mawazo, pamoja na mafunzo mbali mbali yaliyomsukuma msanii hadi kutunga kazi fulani ya fasihi.
Hili ni wazo kuu au mawazo mbali mbali yanayojitokeza katika kazi ya fasihi ambayo mwandishi huyajengea hoja. Dhamira hutokana na jamii na zipodhamira kuu na dhamira ndogo ndogo. Dhamira kuu ni zile za kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni. Dhamira kuu ndicho kiini cha kazi ya fasihi na dhamira ndogo ndogo ni zile zinazoambatana na dhamira kuu.
Migogoro ni mivutano na misuguano mbali mbali ambayo huibuliwa na mwandishi katika kazi ya fasihi. Mgogoro kati ya wahusika ama vikundi vya wahusika, familia zao matabaka yao n.k. Migogoro hii mara nyingi hujikita katika mahusiano ya kijamii na ndipo tunapata migogoro ya:
- kisiasa
- kiuchumi
- kiutamaduni
- kinafsia (kifikra)
Ujumbe katika kazi ya fasihi ni mafunzo mbali mbali yapatikanayo baada ya kuisoma kazi ya fasihi. Ujumbe huwa sanjari na maadili mbali mbali ambayo mwandishi amekusudia jamii iyapate.
Ni hali ya kuyaona mambo katika maisha kwa kuzingatia mazingira aliyonayo msanii mwenyewe. Wasanii wana mitizamo ya aina mbili:
- Mtazamo wa kiyakinifu: mtazamo huu ni ule wa kuyaangalia mambo waziwazi na kuyaelezea kwa jamii kupitia kazi za kifasihi. Msanii anayeunga mkono mtazamo huu huutazama ulimwengu au mazingira yanayomzunguka binadamu kisayansi na hivyo huelezea mambo katika uhalisia wake.
- Mtazamo wa kidhanifu: msanii mwenye mtazamo wa kidhanifu hujadili mambo na kuyatolea masuluhisho yaliyoegemea katika kudhani tu pasipokuzingatia uhalisia wa mambo. Huchukulia ulimwengu kama kitukinachobadilika kulingana na matakwa ya Mungu.
- Falsafa: Huu ni mwelekeo wa imani ya msanii. Msanii anaweza kuamini kuwa, mwanamke si kiumbe duni kama wengine wanavyoamini au, kwa wale wapinga usawa, wanaweza kuwa na falsafa ya kumwona mwanamke kuwa kiumbe duni au chombo cha starehe. Hivyo falsafa inatakiwa ichambuliwe kwa kuzingatia jinsi kazi hiyo ilivyoutazama ulimwengu na kuueleza ukweli juu ya mambo mbali mbali na ukweli huo lazima uhusishwe na binadamu.
Msimamo ni hali ya mwandishi kuamua kushikilia na kutetea jambo fulani bila kujali kuwa jambo analolishikilia linakubalika au la. Misimamo ya mwandishi huweza kuwekwa katika makundi (kategoria) matatu:
- Msimamo wa kimapinduzi: Mwandishi mwenye msimamo huu huyajadili masuala/matatizo yanayoihusu jamii yake na kuonesha bayana mbinu (njia) za kuondokana na matatizo hayo. Mwandishi huyu hutumia kazi zake za kifasihi kama jukwaa la kupigania mabadiliko na mageuzi katika jamii. Anatoa mapendekezo au suluhisho la wazi la matatizo, akiwa na lengo la kuchochea mabadiliko makubwa na kuleta mabadiliko ya kijamii, kisiasa au kiuchumi.
- Msimamo usio wa kimapinduzi: Mwandishi mwenye msimamo huu huwa na asili ya woga inayomfanya kuyajadili mambo kwa kufichaficha na hivyo kushindwa kuleta athari chanya katika mapinduzi. Mwandishi huyu hutangaza matatizo au changamoto za kijamii lakini hakuwa wazi katika kutoa suluhisho halisi. Kwa hiyo, kazi yake hufaili katika kuleta mabadiliko ya kweli kwa jamii, kwani haibuni mbinu za moja kwa moja za kushughulikia masuala yaliyozungumziwa.
- Msimamo wa kiadilifu: Mwandishi mwenye msimamo huu hutetea maadili ya haki, usawa na utu kwa kujikita katika kuonesha umuhimu wa utu katika jamii. Anapinga unyanyasaji, ubaguzi na ukandamizaji katika jamii, lakini analenga kutoa suluhisho linalohusiana na kupigania haki za binadamu, bila kutafuta mapinduzi au changamoto kubwa kwa mfumo uliopo. Huu ni msimamo wa kukubalika na jamii nzima kwa sababu hauhitaji mabadiliko makubwa ya kijamii, bali unajikita katika kuboresha hali ya sasa kwa njia za amani na za kimaadili.
Fani katika fasihi ni ule ufundi wa kisanaa anaoutumia msanii katika kufikisha ujumbe wake kwa jamii inayohusika
Mwalimu
Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.
Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.
Ingia ili kuuliza