Mada za sehemu hiiKuonesha Uelewa Wa Jambo Ulilolisikiliza Au KulisomaMada 2
- Kusoma Sentensi
- Vifungu Vya Habari
Soma habari ifuatayo kisha jibu maswali
Mwalimu Kapesa ni mwalimu wa somo la Kiswahili darasa la tano. Mwalimu huyu ni mgeni: amehamia kutoka shule ya Uyole. Mwalimu Kapesa ni mchapakazi na anaipenda kazi yake ya ualimu.
Siku moja alituuliza kama kuna mwanafunzi yeyote amewahi kutembelea mbuga za wanyama. Sote tulimjibu hatujawahi kutembelea mbuga za wanyama. Alituuliza kama tumeshawahi kuona picha za wanyama. Asha alijibu kuwa aliwaona kwenye kitabu cha hadithi.
Mwalimu alitoa picha za wanyama mbalimbali, akatuonyesha kisha sisi akataja majina ya wanyama hao na sifa zao.
Picha za wanyama na sifa zao
i) Simba
SIFA ZA SIMBA:
- Chakula chao kikuu ni Nyama.
- Simba jike anaanza kuzaa akifika umri wa miaka 2-3
- Simba jike ndiye anayewinda na baada ya kuwinda simba dume ndio anayeanza kula nyama, hasa vitu vya ndani kama vile utumbo na maini.
ii) Chui
SIFA ZA CHUI:
- Ni mnyama mwindaji anayewinda kimya kimya.
- Wanaweza kuishi kwa umri wa zaidi miaka 21.
- Kiasili ni mnyama anayependa kuwinda usiku.
- Anaweza kukimbia kilomita 58 kwa saa.
iii) Mamba
SIFA ZA MAMBA:
- Wanaishi majini hasa kwenye maji baridi.
- Hupatikana maeneo mengi ya kitropiki katika Afrika, Asia na Amerika.
- Maumbile yake humfanya awe mwindaji hodari.
- Hula hasa wanyama wengi wenyi uti wa mgongo kama samaki.
iv) Fisi
- Urefu wake ni zaidi ya inchi 35.
- Huishi zaidi ya miaka 20.
- Fisijike ana nguvu kuliko fisi dume.
- Ni kiumbe asiyekuwa na mbio za kasi.
- Anajulikana kwa kuwa muoga na kula mizoga.
v) Mbwa
SIFA ZA MBWA:
- Anatumika kama mlinzi wa mali za binadamu.
- Akitoa (akibweka) sauti yake husikika.
- Huishi na binadamu.
vi) Tembo
SIFA ZA TEMBO:
- Ni mnyama mkubwa kuliko wote lakini sio mrefu kama Twiga.
- Tembo jike wanauwezo wakubeba mimba kwa miezi 18-20
- Tembo jike hunyonyesha watoto wake kwa takribani miaka 2-3
- Tembo huishi miaka 60-75 kwa sasa, lakini miaka ya zamani walikuwa na uwezo wa kuishi miaka 80-120.
vii) Twiga
SIFA ZA TWIGA:
- Ni miongoni mwa wanyama wenye mvuto.
- Ni mrefu na ana shingo ndefu kuliko mnyama yeyote duniani.
- Twiga hana ushindani mkubwa wa chakula na wanyama wengine kwa vile yeye hula majani ya juu zaidi.
- Ana urefu wa kati ya mita 4.8 na 5.5.
- Uzito wake ni kati ya kilo 700 mpaka 1500.
Mwalimu Kapesa alituambia simba, chui, mamba na fisi hawali majani, huwa wanakula nyama, huwinda wanyama kama sungura na kuwala.
Asha alimuuliza mwalimu, "Simba, chui, mamba hawawezi kufugwa nyumbani?" Mwalimu Kapesa alijibu, "Wanyama hao sio wa kufugwa nyumbani kwani ni wakali sana. Wanyama hawa huishia kwenye mbuga za wanyama. Wanyama hawa ni kivutio kwa watalii. Watalii hutoka ng'ambo kuja kuwaona wanyama hao. Hulipa fedha kwa ajili ya kiingilio cha kuwaona hivyo hutuingizia fedha za kigeni na kuongeza pato la Taifa."
Mwalimu Kapesa alionyesha kwamba mamba huishi majini. Mamba anayo faida, ngozi yake hutumika kutengeneza viatu.
Mwalimu Kapesa alimaliza somo lake kwa kutuambia kuwa mbwa hufugwa nyumbani. Mbwa hutusaidia kulinda nyumba zetu.
Kusoma kifungu cha habari na kubaini majina ya miti
Soma habari ifuatayo.
Mwalimu Masawe ni mwalimu mkuu katika shule ya Lokiri mkoani Kilimanjaro. Shule hiyo ina uwanja mkubwa wa michezo na shamba kubwa.
Mwaka uliopita mwalimu Masawe alianzisha mradi wa upandaji miti. Kwanza alianza kuwaelimisha walimu wenzake pamoja na wanafunzi faida za miti.
Alisema upandaji miti ni njia mojawapo ya kutunza mazingira na kuepuka na jangwa. Kila mtu anapaswa kujali: kutunza na kuyahifadhi mazingira yetu ili ukame usitokee.
Miti hutusaidia kupata hewa safi, mua za kutosha, kivuli, kuni, makaa, mbao kwa ajili ya kutengeneza samani kama vile meza, vitanda, madawati, n.k. Vilevile, miti ya matunda hutupatia matunda kama vile maembe, machungwa, malimau na mapapai ambayo ni muhimu kwa afya zetu.
Baada ya kuwaelimisha aligawa mti mmoja mmoja kwa kila mwanafunzi ili aoteshe na kutunza ipasavyo. Miti hiyo ilikuwa ni miti ya mikaratusi, miarobaini, mipingo, mipodo, miashoki, milonge, miheledi na miti ya matunda kama vile miembe, michungwa, mipapai, mizambarau, mitopetope,pera na mifenesi.
Mwalimu alituambia baada ya miaka mitatu tutafaidika na miti hiyo kwa kupata kivuli, hewa safi, matunda na madawati.
Mwalimu alisema mtu akikata mti mmoja inabidi apande miti mitano. Tutunze mazingira ili yatutunze.
Mwalimu
Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.
Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.
Ingia ili kuuliza