Sonzaschool
Rudi

Msingi · Darasa la Tano

Kiswahili

Kusoma Sentensi

takriban dakika 1 kusoma

Mada za sehemu hiiKuonesha Uelewa Wa Jambo Ulilolisikiliza Au KulisomaMada 2
  1. Kusoma Sentensi
  2. Vifungu Vya Habari

Kamilisha sentensi kwa kutumia maneno haya

"Kushinda", "Kuliko", "Kama", "Sawa", "Na", "Zaidi ya"

  1. Kamba hii ni ndefu kuliko ile.
  2. Asha ni hodari wa kupika kushinda Mery.
  3. Musa ni mjanaja kama Sungura.
  4. Asha ana umbo sawa na Rozi.
  5. Asha hutumia pesa nyingi zaidi ya Ana.

Tunga sentensi kwa kutumia maneno ya ulinganishi

Mithili ya, kama, zaidi ya, kuliko:

  1. Asha ni mweupe kama mzungu.
  2. Juma ni mnene kuliko Musa.
  3. Anatembea kwa madoido mithili ya Twiga.
  4. Juma ana mbio zaidi ya Hawa.

Kusoma sentensi: umiliki na kinyume

Kusoma sentensi na kubaini maneno yanayoonesha umiliki na kubadili sentensi hizo kuwa katika kinyume.

Umiliki huonesha kumilikiwa kwa vitu kihalali mfano kumiliki ardhi unakua na hati ya umiliki wa ardhi huwa kuna mizizi ya viwakilishi.

UMOJAWINGI
Nafsi ya kwanza-angu-etu
Nafsi ya pili-ako-enu
Nafsi ya tatu-ake-ao

Mfano wa sentensi:

  • Mtoto wangu ameanguka (nafsi ya kwanza umoja)
  • Watoto wetu wameanguka (nafsi ya kwanza wingi)
  • Nguo yako imechanika (nafsi ya pili umoja)
  • Nguo zenu zimechanika (nafsi ya pili wingi)
  • Kuku wake amekufa (nafsi ya tatu umoja)
  • Kuku zao zimekufa (nafsi ya tatu wingi)

Kinyume ni maneno ambayo huwa na maana inayopingana.

Mfano:

  • Rafiki - adui
  • Tengeneza - haribu
  • Bomoa - jenga
  • Ingia - toka

Mwalimu

Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.

Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.

Ingia ili kuuliza