Sonzaschool
Rudi

Msingi · Darasa la Saba

Kiswahili

Usomaji wa Matini Mbalimbali

takriban dakika 5 kusoma

Mada za sehemu hiiUsomaji Wa Matini MbalimbaliMada 1
  1. Usomaji wa Matini Mbalimbali

a) Kusoma matini teule kwa kuzingatia alama zote za uandishi na kueleza umuhimu wa matini hizo

Matini ni andiko au chapisho linalohusu maudhui zaidi kuliko fani. Kutokana na maana hii tunaweza kusema si matini zote huzingatia zaidi kipengele cha fani na kuacha maudhui. Zipo ambazo huweka usawa katika vipengele hivyo. Matini kama zile za kisiasa na zile za kisayansi, zinahusisha kipengele cha maudhui zaidi kuliko fani.

Matini ni wazo au mfululizo wa mawazo ambao unajitosheleza kimaana. Matini yaweza kuwa neno moja: kirai, kishazi, sentensi, aya au kifungu cha habari ambacho kinajitosheleza kimaana chenye ujumbe au wazo linalojitosheleza.

Soma matini teule ifuatayo kwa kuzingatia alama zote za uandishi kisha jibu maswali vanayofuata:

Maji ni moja kati ya vitu muhimu sana vinavyotuwezesha kuishi. Vitu vingine ni hewa na chakula. Hewa ndiyo ya kupewa kipaumbele kwani binadamu au wanyama akikosa hewa kwa dakika chache hufa.

Kusingelikua na maji, maisha ya binadamu na viumbe wengine yasingeliwezekana. Maji yanatamalaki maisha ya viumbe hai kwa kiasi kikubwa sana. Baadhi ya viumbe maskani yao ni kwenye maji, mfano samaki, mamba na nyangumi.

Binadamu hutumia maji kwa shughuli mbalimbali. Hutumia maji kwa kunywa; kuogea, kupikia, kuoshea vyombo na shughuli nyingine ndogondogo. Kuna sehemu nyingine watu hutumia maji kumwagilia bustani za mboga.

Kilimo cha umwagiliaji kinafaa kwani mkulima anakuwa na uhakika wa kuvuna wakati wote.

Maji ya mvua vanatuwezesha kulima na kupanda mazao ya chakula na biashara. Ingawaje hapa kwetu Tanzania kuna sehemu ambazo wakulima hutegemea kilimo cha mvua.

Bila maji hakuna uhai kwa sababu maji ni uhai. Uharibifu unaofanywa na binadamu unasababisha kuwepo kwa upungufu mkubwa wa maji. Binadamu ameharibu mazingira kwa njia nyingi sana. Baadhi ya njia hizo ni kulima kandokando ya vyanzo vya maji, ufugaji huria, ukataji misitu hovyo, kuchoma misitu ni mambo vanayochangia katika kuharibu mazingira na kupelekea upungufu wa maji.

Maji kwa upande mwingine yana hasara zake. Maji yanapokuwa mengi kupita kiasi, mathalani mvua kubwa sana zinaponyesha mfululizo, mafuriko hutokea. Watu huweza kupoteza maisha kwa kufa maji na mazao huharibika mashambani. Hata hivyo mafuriko hutokea kwa nadra sana.

Kusoma matini teule za kisiasa, kiuchumi na kijamii kubaini maneno mapya na kuvatumia katika miktadha mbalimbali.

Maneno mapya

Mabadiliko mengi yanatokea kila siku katika nyanja mbalimbali za kimaisha kama kiuchumi: kisiasa, sayansi na teknolojia. Watu huhitaji kuwasiliana.

Lugha huhitaji kuunda maneno mapya ili kuwasilisha dhana mpya zilizoibuka mfano maneno kama kompyuta, tarakilishi, udukuzi yameundwa ili kuwasilisha dhana za kiteknolojia kwa Kiswahili.

Mabadiliko ya kimaendeleo yanafanya lugha ihitaji maneno ya kuyafikisha na kutumiwa na jamii ili kukidhi mahitaji hayo.

Maneno hayo yanaweza kuwa katika fani mbalimbali kama vile sayansi na teknolojia, siasa, utamaduni na uchumi kulingana na mkondo wa maendeleo.

Soma habari ifuatayo

Tangu nchi yetu ipate uhuru tumeanzisha viwanda vingi. Kuanzishwa kwa viwanda hivyo kulikuwa na lengo la kuimarisha uchumi na kuwapa wananchi ajira. Baada ya uhuru viwanda vidogo na vikubwa vimekuwa vikijengwa katika mikoa mbalimbali nchini. Viwanda hivyo vilimilikiwa na serikali na vilijulikana kuwa ni mali ya umma. Miaka ya hivi karibuni viwanda ambavyo vimeshindwa kujiendesha kwa ufanisi vimebinafsishwa. Serikali inaruhusu makampuni ya ndani na nje ya nchi kuanzisha viwanda hapa nchini. Watu binafsi pia wenye uwezo wanaruhusiwa kuanzisha viwanda hapa nchini.

Humu nchini vipo viwanda vinavyozalisha mafuta ya kupikia yanavotokana na mbegu, mfano, mafuta ya alizeti. Mafuta haya yanazalishwa kwa wingi katika mikoa ya Dodoma na Singida, kwani mikoa hiyo hulima alizeti kwa wingi.

Pia vipo viwanda vinavyotengeneza vinywaji baridi kama vile soda, juisi (shurubati) na maji. Na viwanda vingine hutengeneza vinywaji vikali kama bia na konyagi. Vipo viwanda vya pembejeo za kilimo, vifaa vya majumbani na viwanda vingine vingi.

Kabla kiwanda hakijaanzishwa, ni lazima wataalamu wa mambo ya viwanda wafanye utafiti wa kutosha kuhusu kuanzishwa kwa kiwanda hicho. Ni lazima wajue kama kiwanda kitakapojengwa patakidhi masharti muhimu ya kuanzishwa kwa kiwanda hicho. Mfano, hakitawabugudhi wakaziwaliopo jirani na kiwanda au kama hakitaharibu mazingira. Wataalamu hao ni lazima wajue pia malighafi zitatoka wapi na zitafikaje kiwandani na ni wapi bidhaa zitakapotengenezwa zitauzwa. Kiwanda kikianzishwa bila kufanyiwa utafiti wowote kinaweza kufilisika haraka na kufungwa au kuendeshwa kwa gharama kubwa.

Viwanda vinapaswa kuinua uchumi wa nchi kwa kutoa ajira kwa wananchi na pia kulipa kodi kwa serikali. Kodi hiyo huiwezesha serikali kuhudumia hospitali, shule, miundombinu, na huduma nyingine za jamii.

Viwanda vingi vilivyomo nchini vimejengwa kwa kuzingatia masharti muhimu ya ujenzi wa viwanda. Mfano, viwanda vya kusindika minofu ya samaki vipo Mwanza kwa sababu kuna ziwa Victoria lenye samaki wakubwa na wenye minofu. Na pia kuna barabara, uwanja wa ndege, na reli kwa ajili ya kusafirishia bidhaa ndani na nje ya nchi.

Swali

Kwa nini hewa inapaswa kupewa kipaumbele kuliko vyingine?

Ingia ili kuwasilisha jibu lako na lihesabiwe katika umahiri wako.

Ingia ili kufanya mazoezi

Mwalimu

Umekwama? Niulize chochote kuhusu mada hii.

Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu swali hili.

Ingia ili kuuliza