Mada za sehemu hiiUfupisho Wa Habari Na HadithiMada 1
- Ufupisho wa Habari na hadithi
Ili ufupisho uwe mzuri hatua zifuatazo hazina budi kufuatwa:
- Kuisoma na kuisikiliza habari kwa makini ili kueleweka vizuri.
- Kutambua na kubaini mawazo makuu yanayojitokeza katika kila aya.
- Kuyaunganisha mawazo makuu na kuandika au kuelezea ufupisho wa habari hiyo kwa maneno yako mwenyewe bila kupotosha maana ya habari ya kwanza.
- Kuhesabu idadi ya maneno ya ufupisho ili kuyapunguza ikiwa yanazidi idadi inayotakiwa.
- Pitia tena habari ya mwanzo na pitia tena ufupisho ili kujiridhisha kuwa hujaacha taarifa yoyote ya muhimu.
- Ufupisho humwezesha mwanafunzi kufikiria waziwazi, kwani mazoezi hayo humtaka mwanafunzi asome kwa uangalifu ili aone habari muhimu.
- Ufupisho humfanya mwanafunzi aeleze kwa ufupi, usahaihi na atumie lugha ya mkato.
- Ufupisho humpa mwanafunzi mazoezi ya kupanga mawazo yake kwa uangalifu na katika sentensi zilizilonavu. Katika kufupisha huanza na vifungu vya maneno, kisha sentensi moja kabla ya kuelekezwa kuchambua habari ndefu.
- Hutumika wakati wa kutayarisha ripoti na kumbukumbu za mikutano
- Husaidia wakati wa kuandaa hoja kutokana na mihadhara au hotuba
- Hutumika katika kuandaa shajara au kumbukumbu za kila siku
- Husaidia katika uhariri wa habari
- Husaidia kuokoa gharama hasa katika uandishi wa simu ya maandishi
Palikuwepo na familia moja iitwayo familia ya Bwana Suka, aliyekuwa na mke na binti zake watatu. Mke wa Suka aliitwa Sara. Sara alikuwa hodari kwa kupika kitoweo kilichokuwa maridadi na kitamu sana.
Suka, baba wa watoto, alitamani kula kitoweo hicho hata kabla ya Chakula cha jioni. Katika harakati za kupakua hata kabla ya wakati kuwasili, mchana alisubiri wanae waende shuleni na mkewe aende shambani.
Alianza kuita, kila jina la mtu aliyeishi pale ili kuhakikisha kwamba wote wametoweka ili aingie ndani aibe kitoweo kilichoachwa kwa ajili ya kutumiwa katika Chakula cha jioni.
Mke wa Suka kila wakati anaporudi nyumbani hukuta kitoweo kimeliwa. Na hii humlazimu kuandaa kitoweo kingine japokuwa anakuwa amechoka kwa shughuli za shamba.
Panya aliyekula kitoweo alikuwa na nguvu za kunyanyua hata mfuniko kutoka kwenye sufuria. Familia ya Bwana Suka ilishangazwa na panya huyu alivyokuwa na nguvu tofauti na panya wengine.
Siku moja binti mkubwa aliwaambia wanafamilia kwamba, "Mimi panya huyu nitamkamata. Lakini sitasema ni lini wala kwa wakati gani nitakapofanya hili jambo, kwani panya huyu ametega masikio yake na amepanua macho yake kusikia na kuona tunayoyapanga."
Suka alimshukuru binti yake kwa hatua hiyo. Suka alifanya hivyo ili asijulikane kwani akijulikana itakuwa ni aibu kubwa mno.
Si mwingine bali ni Bwana Suka. Kwa bahati mbaya Bwana Suka alikuwa uchi wa mnyama. Hivyo alipochuchumaa karibu na mtego alibanwa sehemu zake za siri. Bwana Suka alihisi maumivu makali. Bwana mwizi alipiga kelele watu wa nyumbani kwake wakakurupuka kutoka usingizini kuona ni kitu gani kilichompata baba yao. Waliona damu zikitiririka na mtego ukining'inia kwenye sehemu zake za siri.
Familia ya mzee huyu ilishangazwa, wakamuokoa. Lakini kila mtoto aliyetoka usingizini wimbo ulikuwa "panya mtu, panya mtu."
Swali
Ni kipi kati ya vifuatavyo ni umuhimu wa ufupisho?
Ingia ili kuwasilisha jibu lako na lihesabiwe katika umahiri wako.
Ingia ili kufanya mazoeziMwalimu
Umekwama? Niulize chochote kuhusu mada hii.
Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu swali hili.
Ingia ili kuuliza