Mada za sehemu hiiHadithiMada 1
- Uchambuzi wa Hadithi
Hadithi
Hadithi ni masimulizi ambayo yanatumia lugha ya kawaida na mtiririko wake huwa ni mwepesi au sahili. Urefu wa hadithi hutofautiana kutoka tanzu au kipera kimoja hadi kingine. Kuna baadhi za kubuni na hadithi za kihistoria.
MAUDHUI
Haya ni yaliyomo au ni jumla ya masuala yanayozungumziwa katika kazi ya fasihi. Maudhui huibuka katika uendelezaji na ukuzaji wa dhamira au wazo kuu la kazi ya fasihi. Kwa ufupi dhamira hujitokeza kama sehemu ya maudhui. Katika kusoma na kuchambua maudhui katika hadithi fupi, msomaji achunguze lengo kuu na ujumbe wa mwandishi. Msomaji anaweza kuelekezwa kwenye lengo kuu au dhamira ya hadithi na kichwa cha hadithi yenyewe kisha msomaji atafute na kubainisha msimamo wa mwandishi pamoja na mwelekeo wake wa kimawazo na kifalsafa.
WAHUSIKA
Wahusika katika kazi yoyote ya sanaa itumiayo lugha ni watu, wanyama ama vitu. Wahusika husawiriwa kisanaa na mwandishi ili waweze kuwakilisha dhana mbalimbali za maisha katika jamii. Wahusika katika hadithi huwa ni binadamu na mazimwi ama binadamu hata miti. Huwezekana pia wahusika wakawa binadamu na viumbe visivyokuwa hai kama vile mawe.
Soma hadithi ifuatayo
Hapo zamani za kale alikuwepo mzee mmoja aliyeitwa Mtinga. Mzee huyo alikuwa maarufu sana pale kijijini kwao. Jina lake lilikuwa akilini mwa kila mtu, awe mdogo au mkubwa. Alikuwa na kipaji cha kusema na kuwashawishi watu. Mzee Mtinga hakuwa na choyo na aliwapenda watu wanaofanya juhudi katika kutafuta maendeleo. Hakupenda ugomvi wala kulipiza kisasi kwa watu japokuwa watu walimkosea kwa kuwa yeye alikuwa na moyo mweupe. Kila wakati alikuwa yupo tayari kumsaidia mtu yeyote hata kama alikuwa hamfahamu. Kamwe hakuwa mtu wa kujigamba. "Yeye alielewa vizuri methali isemayo, 'Tenda wema nenda zako usingoje shukrani'."
Siku moja Mzee Mtinga alikuwa akikagua shamba lake la miwa. Alipokuwa anaendelea na ukaguzi huo, walipita wanafunzi ambao walikuwa wanatoka shule. Wanafunzi hao walikuwa wanaongea. Mzee Mtinga alitega sikio ili asikie yale waliyokuwa wanayaongea.
Wale wanafunzi walikuwa wanajadiliana kuhusu faida za maji. Majadiliano ya wanafunzi wale yalimvuta sana mzee Mtinga. Akaamua kuwasalimia na kusema: "Wajukuu zangu, nimefurahi sana kusikia mkizungumza vizuri sana kuhusu faida za maji. Lakini kujua faida tu haitoshi. Ni lazima mjue na hasara zake pia kwani hakuna masika yasiyo na mbu."
Wale wanafunzi walipigwa na butwaa waliposikia Mzee Mtinga akisema kuwa maji yana hasara. Ndani yao, mmoja kati ya wale wanafunzi akauliza, "Hivi babu maji yanaweza kuwa na hasara?"
Mzee Mtinga alicheka kidogo kisha akajibu, "Oh! Maji yana hasara nyingi. Maji husababisha mafuriko yanapozidi kwa ajili ya mvua kuwa nyingi kupita kiasi. Mafuriko yanapotokea mimea vite humezwa na maji, barabara na zahanati na shule pia. Kadhalika, maji ya mivia husababisha makorongo ambayo huleta uharibifu mkubwa wa mazingira yetu."
Mwanafunzi mwingine aitwaye Nyamchele naye akauliza, "Babu tunajua kuwa hewa ina faida kubwa kwa viumbe. Je? Hewa nayo ina hasara?" Mzee Mtinga akacheka kidogo kisha akamwambia hewa chafu kama ile yenye moshi au vumbi ina hasara kwani huathiri mapafu. Pia hewa inayotoka viwandani huathiri mazingira yetu.
Baada ya wanafunzi kujibiwa maswali yao, walimshukuru Mzee Mtinga. Kabla hawajaondoka, Mzee Mtinga aliwaambia, "Wajukuu zangu: hakuna kitu kizuri duniani kama kuwa tajiri wa akili."
Wale wanafunzi walifurahi sana. Nyamchele alimpongeza Mzee Mtinga kwa kumshika mkono kisha akamuaga kwa niaba ya wenzake.
FAIDA ZA HADITHI
-
Kuburudisha: Hadithi huburudisha watu walichoka baada ya kufanya kazi mchana kutwa.
-
Hukuza ushirikiano: Hadithi husimulia mambo yanayohusu ushirikiano katika shughuli mbalimbali za kijamii mfano kilimo, misiba, ufugaji, uwindaji, harusi n.k.
-
Kurithisha amali za jamii kutoka kizazi kimoja kingine: Hadithi hurithisha mila na desturi zajamii fulani kutoka kizazi kimoja hadi nyingine.
-
Kuliwaza watu: Hadithi pia huweza kutumika kwa kuliwaza watuwaliopatwa na majonzi au wale ambao wapo katika hali ya kuchanganyikiwa kwa kuwasimulia hadithi au kusikiliza.
-
Kujenga jamii na kuipa mwelekeo: Lengo la kusimulia hadithi ni kuifanya jamii iwe na mwelekeo mzuri unaozingatia maadili katika jamii.
-
Kuelimisha: Katika hadithi kuna maadili na ujumbe unaotolewa kwa jamii. Hivyo kwa njia hii hadithi hutumika kama chombo cha kuelimisha jamii. Mfano hadithi husimulia tabia za uchoyo, uzembe, wizi, wivu, na matatizo yaliyowapata huwa funzo kwa jamii.
Soma hadithi ifuatayo
MTOTO ULEAVYO NDIVYO AKUAVYO
Kuzoea ni jambo la heri. Japo baadhi ya watu wengine husema kuzaa ni kuondoa maradhi maradhi tumboni. Mimi sikubaliani na usemi huo kwani ninaamini mtoto umleavyo ndivyo akuavyo. Sitofautiani sana na wanaotumia methali nyingine isemayo "mchelea mwana kulia hulia yeye".
Methali zote hizi mbili zisingeweza kutumika ndani ya familia ya mzee Masenza na mkewe kama wangekubali kufuata methali isemayo "samaki mkunje angali mbichi" au wengine wasemavyo "uwahi ungali maji".
Udokozi wa mtoto wao Nyakisagani ungeweza kukomesha mapema kabla yaOTA mizizi lakini haikua hivyo. Kwani udokozi uliendelea kwa kasi hadi ukashika hatamu. Nyakisagani amekua na mkono mrefu: wizi wake sasa umekubwa.
Laiti kama wazazi wake wangeemkanya mapema tangu Nyakisagani alivyoanza tabia ya kukwapuakwapua mtaani, hivi leo mzee Masenza asingalikuwapo kizimbani, akisubiri hukumu ya kulipa faini au kwenda jela. Ama kweli ama kweli uchungu wa mwana aujuae mzazi. Hivi hivi mtu asingelichukua dhamana ya kumdhamini Nyakisagani kutokana na jinsi alivyo mkatili. Kweli mchuma janga hula na wanaо.
Kutoroka kwa Nyakisagani kumeleta taharuki ndani ya familia. Watu walikosa chakula kutokana na visa alivyofanya Nyakisagani. Nyakisagani kurudi tena nyumbani ni ndogo, japokuwa Waswahili husema mwenda kwao si mtoro ila si kwa Nyakisagani. Hakuna la kufanya ni kushukuru tuu, kwani maji yakishamwagika hayazoleki.
Swali
Kati ya faida za hadithi zilizomo katika somo, ipi siyo faida ya hadithi?
Ingia ili kuwasilisha jibu lako na lihesabiwe katika umahiri wako.
Ingia ili kufanya mazoeziMwalimu
Umekwama? Niulize chochote kuhusu mada hii.
Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu swali hili.
Ingia ili kuuliza