Mada za sehemu hiiMisamiatiMada 1
- Misamiati Katika Matini Mbalimbali
MSAMIATI
Toa maana ya misamiati ifuatayo na kisha tunga sentensi:
-
Kiwanda
- Mahali panapotengenezwa bidhaa au vifaa
- Mahali mafundi wanapofanyia kazi zao
Sentensi: Baba yangu anafanya kazi kwenye kiwanda cha kutengeneza saruji.
-
Utafiti Uchunguzi wa kisayansi au kitaaluma ambao unalenga kugundua, kuunda, kufasiri, kuchanganua au utumiaji wa maarifa mapya, nadharia au kanuni fulani.
Sentensi: Mwalimu alitupa kazi mradi ya kufanya utafiti juu ya wadudu wanaoshambulia migomba.
-
Uchumi
- Mali ilivopatikana kutokana na mali za nchi au watu
- Taaluma ya mapato na matumizi ya watu
- Mfumo wa mapato na matumizi ya watu katika nchi
Sentensi: Dada yangu alipomaliza elimu ya sekondari alichaguliwa kujiunga na chuo cha uchumi.
Soma na jibu
Soma habari ifuatayo kasha bainisha misamiati iliyotumika:
Yapata miaka mitatu sasa tangu wazazi wa Nyambuli waage dunia. Miaka ile hiyo Nyambuli amekuwa akiishi maisha ya shida sana. Hakuwa na mbele wala nyumba. Hakika mtoto huyu alipata bahati mbaya isiyoelezeka.
Miaka mitatu iliyopita, Nyambuli alikuwa anasoma darasa la saba katika shule ya msingi Lawate. Shule hiyo ipo Wilaya ya Siha katika mkoa wa Kilimanjaro. Nyambuli aliishi na wazazi wake waliokuwa wafanyabiashara wakubwa mjini Moshi.
Wazazi wake walipata ajali mbaya ya gari na kupoteza maisha papo hapo. Huu ndio ukawa mwanzo wa Nyambuli kuanza maisha mapya bila ya wazazi wake. Nyambuli alikuwa mtoto wa pekee kwani dada yake alifariki kwa kugongwa na pikipiki akiwa na miaka tisa. Ooh! maskini Nyambuli aliachwa yatima.
Kwa kuwa wazazi wake walikuwa na ukwasi, kila ndugu alijifanya kuwa mlezi wa Nyambuli. Wakati wote wa msiba hali ilikuwa shwari. Baba yake mkubwa alijigamba kwamba yeye ndiye mwenye mamlaka ya kumtunza Nyambuli. Baada ya kuanua matanga likubaliwa baba mkubwa amlee Nyambuli kwani mtoto huyo ni yatima. Kwa kuwa mali zote za marehemu ziliandikwa jina la marehemu, baba yake mkubwa wa Nyambuli alifanya juu chini kubadili umiliki wa mali zile uwe kwa jina lake. Baada ya mwaka, mali za marehemu zilisajiliwa kwa jina la Sadoki Mariale.
Kwa upande wa Nyambuli maisha yalikuwa magumu kupindukia. Shule aliacha kwani baba yake mkubwa aliacha kumlipia ada. Mahitaji muhimu yalikuwa nadra kupatikana. Bwana Sadoki alitumia mali ile ovyo na kwa anasa. Baada ya muda mfupi mali zote za marehemu mdogo wake zikawa zimeyoyoma. Maisha yalizidi kuwa duni zaidi.
Nyambuli aliamua kutoroka na kwenda mjini kutafuta kibarua ili aweze kukidhi mahitaji yake. Huko nako hali haikuwa shwari. Hakupata kibarua katu. Hivyo ilimlazimu kuzurura mjini akiomba wasamaria wema wampe chochote. Maskini ya Mungu! Nyambuli mtoto wa aliyekuwa tajiri maarufu bwana Samweli Mariale sasa ni mtoto anayeishi katika mazingira magumu. Ama kweli hakuna msiba usiokuwa na mwenziwe.
Swali
Neno utafiti linamaanisha nini?
Ingia ili kuwasilisha jibu lako na lihesabiwe katika umahiri wako.
Ingia ili kufanya mazoeziMwalimu
Umekwama? Niulize chochote kuhusu mada hii.
Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu swali hili.
Ingia ili kuuliza