Sonzaschool
Rudi

Sekondari ya Juu · Kidato cha Sita

Kiswahili 2

Uhakiki wa tamthiliya

takriban dakika 27 kusoma

Mada za sehemu hiiUhakiki Wa Kazi Za Fasihi AndishiMada 4

UHAKIKI-TAMTHILIA KITABU: NGUZO MAMA

MWANDISHI: PENINA MHANDO

MWACHAPATI: DUP

MWAKA: 1982

Tamthiliya inazungumzia matatizo mbalimbali yanayowakabili wanawake katika jamii ya kitanzania na afrika kwa ujumla. Mwandishi anaonesha unyanyasaji na mateso ya wanawake kutoka kwa waume zao kutokana na mfumo dume uliojengeka katika jamii nyingi.ametumia mandhari ya patata kuyasawiri maisha ya mwanamke wa kiafrika.

Ukombozi wa Mwanamke

Ni tamthiliya inayochambua kwa undani matatizo mbalimbali yanayowakabili wanawake pamoja na jitihada zao ili kujikwamua katika minyororo ya utumwa kwa mwanaume na manyanyaso mengine mazito mengine wanayoyapata kutoka kwa jamii kwa ujumla. Ameyataja manyanyaso hayo kama vile: wanawake kupigwa, kufanyishwa kazi nyingi (kufua, kupika, kulea watoto, kuchota maji, kukusanya kuni n.k). Pia ameonesha mbinu mbalimbali zinazoweza kutumiwa na mwanamke kujikomboa. Mwandishi ameugawa ukombozi wa mwanamke, kama ifuatavyo

Ukombozi wa Kiuchumi

Mwandishi kwa kuwatumia wanawake wa patata ameonesha jinsi walivyoanzisha miradi ambayo ingewawezesha kujipatia fedha na kuwafanya wanawake wote wajitegemee, Wasiwe tegemezi.

"BI NNE Miradi tutatiliya mkaazo, Miradi Yakila aina, vilabu vya pombe, maduka Ya kanga, ushirika wa kushona, kupika Hotel na mengine mengi… "

BI PILI naye aliamua kuanzisha kilabu cha pombe ili aweze kujikwamua katika maisha magumu kiuchumi.

"BI MSIMULIZI Kaamua bi pili

Pombe kujipikia na kilabuni Kuiuza, pesa akipata, pesa msema Kweli. Na mauzo mama atasimama" Nukuu hii inonesha umuhimu wa pesa katika ukombozi wa mwanamke, kwani pesa ndiyo iletayo maendeleo stahiki.

Bi moja alijiunga na wenzake na kuanzisha viwanda vya kufuma mapambo ya nyumbani.

"BI MSIMULIZI katokea bi moja Na wazo lake jipya kiwanda Kuanzisha mapambo ya nyumbani Kufuma "

Ukombozi Kijamii

Kwa kutumia mhusika bi Nane mwandishi amonesha ukombozi wa kijamii kwani alianzisha umoja wa walimu wa kike, Lengo likiwa kutatua matatizo mbalimbali yanayowakabili katika ufundishaji.

"BI MSIMULIZI katokea bi nane na wenzake

Wengi makubwa hawakujitakia Vizuri walijishauri

Tuanze na yetu matatizo………..

Kazi yetu yakufunza vyema kuchapa Vingi vikitokomea

Vyema vijana watafunzika"

Mwandishi anaonesha kuwa elimu ni nyenzo mojawapo ya kumkomboa mwanamke, Katika kumkomboa mwanamke kijamii, mwandishi ameonesha jamii nzima lazima ishirikishwe, Mwanamke peke yake atoweza kujikomboa.

"BI NANE……tushirikishe wanaume pia

Nguzo mama inafaida kwa wote"

Mwandishi anaonesha mwanamke akikomboka ni faida kwa jamii nzima. Pia mwandishi anaonesha umoja na mshikamano kama njia itakayowawezesha wanawake kujikomboa.

Pia mwandishi anaonesha kupitia mikutano watu wengi wataelewa zaidi kuhusu ukombozi wa mwanamke na …, wayapatayo wanawake nahivyo kuwa rahisi kubadilika.

Ukombozi wa Kisiasa

Mwandishi anaonesha juhudi mbalimbali za wanawake wa patata ili kujikomboa kisiasa. Nafasi za uongozi kwa wanawake ni moja kati ya njia hizo ndiyo maana mwandishi anonesha jitihada mbalimbali zilizofanywa na wanawake wa patata ili kuchukua uongozi serikalini. Mwandishi anasema:

"BI NNE madaraka kwa akina mama Jambo hili tumetilia mkazo, Wakina mama watapewa vyeo Orodha tumeshapanga, tutapata Mawaziri, mameneja, mabalozi n.k Wengine tayari wameshapata kama Tunavyofahamu" Mwaandishi ameonesha umuhimu wa mwanamke kupewa uongozi kujikomboa kisiasa. Baadhi ya waliopata uongozi ni Bi Nne, mwenyekiti wa kamati ya vyeo. Bi Tatu, mwenyekiti wa kamati ya malezi bora. Bi Nane mwenyekiti wa umoja wa walimu.

Ukombozi wa Kifikra

Mwandishi ameonesha tatizo linalosumbua wanawake wengi, Wanawake wengi wamekuwa na fikra potofu. Kuwa baadhi ya mambo ni ya wanaume tu hayamuhusu mwanamke, mfano , uongozi , kufanya kazi , kumiliki njia za uzalishaji mali , kujitegemea wao wenyewe n.k kwa mfano bi Nne aliyekuwa mwenyekiti wa wanawake alishiriki kuyachunguza mashtaka ya bi Nane na akatoa hukumu kwa kusikiliza upande mmoja, jambo hili ni fikra potofu. Bi Nane licha ya kufahamu kuwa mashtaka yake ni ya uongo anakubali kila kitu alichoelezwa na bi Nne.

Kwa ujumla ukombozi wa kifikra juu ya wanawake na jamii kwa ujumla vinahitajika ili kufikia ukombozi wa kweli wa mwanamke.

Mwalimu

Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.

Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.

Ingia ili kuuliza