Mada za sehemu hiiUhakiki Wa Kazi Za Fasihi AndishiMada 4
- Uhakiki wa ushairi
- Uhakiki wa riwaya
- Uhakiki wa tamthiliya
- Uhakiki wa diwani
UHAKIKI WA RIWAYA YA "MFADHILI" WACHAPISHAJI: MACMILLAN AIDAN LTD MWANDISHI: HUSSEIN TUWA MWAKA: 2007 A.MAUDHUI UTANGULIZI Ni riwaya inayozungumzia mapenzi katika jamii pamoja na athari zake katika jamii. Ikizungumzia hasa mapenzi ya dhati nayale yasio ya dhati. DHAMIRA KUU MAPENZI NA NDOA Mwandishi anaonyesha mapenzi ya dhati na yasiyo ya dhati pamoja na ndoa. Mapenzi ya dhati
- Kati ya Gaddi na dada yake Bi Hanuna.
- Gaddi kwa Dania
- Gaddi kwa Junior
- Mama Mlole na wafanyakazi wake
- Nunu kwa Dania
- Nunu na Boaz
- Dk Virani na Gaddi
- Wazazi wa Dania na Dania mwenyewe
- Nunu na Gaddi
Mapenzi yasiyo yadhati
- Kati ya Jerry na Dania
- Rafiki yake Gaddi kwa Gaddi
Ndoa yenye mapenzi ya dhati
- Gaddi kwa Nyambuja
Ndoa isiyo ya mapenzi ya dhati
- Nyambuja kwa Gaddi
USALITI Msanii ameonyesha watu mbalimbali waliosalitiwa na athari za usaliti huo. Nyambuja alimsaliti Gaddi kwa kufanya mapenzi nje ya ndoa. Tena alimsaliti na rafiki wa Gaddi, athari yake, utendaji wa kazi wa Gaddi ulishuka na hatimaye alipoteza kazi. Mfano: Dania kwa Gaddi. Athari yake Gaddi kupata shinikizo la moyo kutokana na Jerry na Bi Hanuna kufungwa. Afisa uzalishaji na Gaddi, athari yake gaddi alishushwa cheo kazini. JerrykwaDania. Hakutokea siku ya harusi, pia katika kutoa ini kwa Dania alipokuwa anaumwa. USALITI MZURI. Daktari viiani kwa Gaddi Bulah. UONGOZI MZURI Mwandishi amemtumia mama Mlole kwani aliwasimamia vizuri wafanyakazi wake, alimsaidia Gaddi Bullah alipopata tatizo kazini Pia alimsaidia Dania wakati amepata matatizo. BIDII KATIKA KAZI Mwandishi anaonesha Dania na Gaddi kuwa na bidii katika kazi mpaka tu pale walipopata matatizo. Pia Daktari viran alimhudumia Gaddi Bullah kwa moyo. CHUKI Ameonyesha chuki mbalimbali kati ya wahusika,
- Bi Hanuna alikuwa na chuki na Nunu sababu ya Dania.
- Dania kwa Gaddi. ( mwanzoni)
- Dania kwa Jerry baada ya kuachwa.
- Nunu kwa Jerry kwani alimsaliti Dania
- Wazazi wa Dania kwa Jerry kwani alimtenda binti yao.
DHARAU Mwandishi amemtumia Nyambuja kama mwenye dharau. Mfano alisafiri safari za ghafla na kumtaarifu tu mumewe kwa simu. Vilevile alichelewa kurudi nyumbani. Nyambuja kufanya mapenzi na rafiki yake Gaddi ni dharau. Pia barua aliyomwandikia Gaddi ni kitendo cha dharau. Dania kwa Gaddi ofisini pia alipomfukuza mbele ya Junior. Vile vile baada ya kumwacha Gaddi na kurudi kwa Jerry. NAFASI YA MWANAMKE, Mwanamke ameonyeshwa/amechorwa kama ifuatavyo Kama kiumbe asiye na msimamo. Dania hakuwa na msimamo katika maamuzi yake. Mfano: Jerry- Gaddi- Jerry- Gaddi Kama mtu mwenye huruma na mshauri mzuri. Mfano mzuri ni Nunu aliyekuwa bega kwa bega na Dania. katika matatizo yote pia mama mlole kwawafanyakazi wenzie Kama mtu katili na msaliti. Mfano mzuri ni Dania na Nyambuja kwa jinsi walivyomtenda Gaddi. Kama kiumbe jasiri, Nunu aliyefanya kazi ya kumpatanisha Gaddi na Dania hata kumteka Bi Hanuna dada yake Gaddi. Mwenye upendo na moyo wa huruma. Bi Hanuna aliyempenda sana Gaddi na Mama fausta mlole aliyependa wafanya kazi wake. NAFASI YA MWANAUME
- Mtu mwenye mapenzi ya dhati kama vile Gaddi na Boaz.
- Kiumbe katili na msaliti kama Jerry na rafiki yake Gaddi.
- Mtu mwenye huruma mfano Gaddi Bulla.
- Asiyekuwa na msimamo kama vile Jerry.
- Mvumilivu na jasiri. Gaddi na Boaz
UJUMBE
- Rafiki wa kweli ni yule anayekusaidia wakati wa shida.
- Si kila king’aacho ni dhahabu
- Mtu akitenda kosa ni lazima akubali kutubu kosa.
- Ni vigumu kumpata mtu wa kukupenda kama unavyompenda wewe.
- Bidii na ufanisi katika kazi ni chachu ya maelendeleo
- Matatizo, chuki, majaribu na dharau ni lazima katika mapenzi na ndoa.
- Mwandishi ameonesha dhahiri kwamba uchungu wa mwana aujuaye mzazi.
FALSAFA Msanii anaamini kuwa katika mapenzi kuna kupenda na kupendwa, kuna kuoa na kuachwa, hivyo ni vigumu kumpata mtu mwenye mapenzi ya dhati. Mfano Gaddi, Bullah, Jerry, Dania, Nyambuja. MSIMAMO Msimamo wa mwandishi ni wa kimapinduzi, kwani anaonyesha wazi kuwa katika suala la mapenzi na ndoa kuna matatizo yake. Watu lazima tukubali kusameheana kwani hujui ni yupi atakayekusaidia wakati wa shida. MGOGORO
- Mgogoro kati ya Gaddi na Nyambuja (sababu ya usaliti ,kuachana)
- Mgogoro kati ya Gaddi na Dania(kurudiana na jerry, kutengana)
- Mgogoro kati ya Gaddi na Jerry(sababu ya Dania, kupigana)
- Jerry na wazazi wake Dania(jerry kuwa msaliti, alikataliwa)
- Nunu na Jerry.(Dania)
- Nunu, Boaz na Bi Hanuna (ugonjwa wa Dania, kumtoa Bi Hanuna)
- Dania na Jerry (usaliti, kurudiana)
- Mgogoro wa kinafsia (Gaddi, Dania)
FANI MUUNDO Mwandishi ametumia muundo changamano, Kuna muundo rejea (SURA YA I), Muundo wa Msago (SURA YA II – MWISHO). MTINDO Mtindo wa masimulizi umetumika kwa kiasi kikubwa na kiasi kidogo ametumia daolojia/majibizano, Mwandishi pia ametumia nafsi zote tatu, Ametumia pia barua (uk. 65)mazungumzo ya simu. (uk. 118, 72) MATUMIZI YA LUGHA Lugha ni rahisi iliyojaa misemo, methali, matusi na mbinu mbalimbali za kisanaa Lugha ya matusi.Mfano: Dania ni shwetwaani Misemo na nahau. Mfano: Jibu lile lilimkata maini Methali: Mfano:-
- Ukistaajabu ya musa utaona ya firauni
- Bora nusu shari kuliko shari kamili
- Hakuna marefu yasiyo na ncha
- Mkaidi hafaidi mpaka siku ya iddi
Matumizi ya kingereza. Mfano:-
- Boaz go! go! go! go! gooo!
- Nunu what the hell are you doing?
Tamathali za semi na mbinu mbalimbali za kisanaa Tashbisha Mfano:
- Paa lake
- Nunu alikuwa kama mtu aliyepagawa
- Kumfukuza kama mbwa kutoka katika nyumba ya marehemu mumewe.
Sitiari Mfano:
- Dania ni shwetwaani
- Kila mwanaume ni Jerry
Takriri, Mfano:-
- Hatua ndefu za harakaharaka
- Kwenda mwana kwenda
- Yaani alikuwa ni kimya moja kwa moja
Tanakali sauti, Mfano:-
- Sauti za Ko! Ko! Ko!
Mdokezo, mfano:-
- Ah! Ni kweli! Aunti.....lakini......
Tashtiti, Mfano:-
- Kamsubirie hukoooo! Siyo hapa kwangu, upo?
- Yaani alikuwa kimya moja kwa moja
- Yule
Mjalizo, Mfano:-
- Katili jeuri, masaliti na asiyestahili heshima hata kidogo
- Gaddi Bullah
- Ndiyo bwana
Nidaa, mfano:-
- Ee bwana we!
- Khah!
- Mnnh!
MANDHARI
- Ofisini
- Baa
- Nyumbani
- Barabarani
- Hospitalini
- Dar es salaam
- Arusha
- Pemba
- Chumbani
JINA LA KITABU Kwa kiasi kikubwa linasadifu yaliyomo:
- Mama mlole alimfadhili Gaddi dhidi ya kashfa
- Mama mlole alimfadhili Dania baada ya kurudia pombe
- Mama mlole alimfadhili Dania na Gaddi
- Gaddi alimfadhili Dania kwa kumpa ini ili asife
- Gaddi alimfadhili Junior
KUFAULU NA KUTOFAULU Kufaulu kimaudhui. Amefaulu kuonyesha matatizo mbalimbali yaliyopo katika jamii hasa swala la mapenzi na ndoa, kisha kutoa suluhisho la matatizo hayo. Kufaulu kifani Amefaulu kutumia lugha rahisi na inayoeleweka na amejenga wahusika wake vizuri Kutofaulu kifani Ametumia viswahili badala ya Kiswahili sanifu,Pia matumizi ya kingereza, Kutofaulu kimaudhui Ameangalia tu suala la mapenzi na kusahau matatizo mengi katika jamii. VUTA N'KUVUTE Adam Shafi Adam Vuta n'Kuvute ni riwaya ya Kiswahili iliyoandikwa na mwandishi mahiri na mkongwe Shafi Adam Shafi na kuchapishwa kwa mara ya kwanza na Mkuki na Nyota Publishers Dar es Salaam. Adam Shafi ni mwandishi wa Fasihi ya Kiswahili ambaye ameandika kazi nyingi na miongoni mwa kazi zake nzuri alizowahi kuandika ni Kuli na Kasri ya Mwinyi Fuad. Riwaya ya Vuta n'Kuvute imejikita juu ya Vuta ni Kuvute za kisiasa, kiutamaduni na kijamii.vuta n'kuvute hizi zimeweza kuibua dhamira mbalimbali ambazo mwandishi alikusudia ziifikie jamii aliyoiandikia. Pia mwandishi ametumia ufundi mkubwa wa kisanaa katika kuzielezea dhamira. Maudhui katika vuta n'kuvute VUTA NKUVUTE ZA KISIASA Miongoni mwa vuta ni kuvute alizozijadili msanii ni vuta nkuvute za kisiasa, Vuta ni kuvute hii imeibua dhamira zifuatazo: mapambano, kujitoa muhanga umoja na mshikamano, mbinu/mikakati ya kuyaendea mambo, uongozi mbaya, ubaguzi na ukiukwaji wa haki za binadamu. Mapambano Dhidi Ya Dhuluma (Ukoloni) Dhamira kuu inayojitokeza katika riwaya hii ni mapambano dhidi ya dhuluma. . Kama zilivyo kazi nyingi za fasihi ya Kiswahili na ya Afrika huzungumzia mapambano ya kuleta ukombozi kwa jamii kandamizwa kwa kuwa jamii ya Kiafrika imepitia katika la kukandamizwa kutawaliwa (ukoloni) na kuibiwa rasilimali yake ndio maana mwandishi ameibua dhamira hii ili kuishajihisha jamii isiendelee kukubali kudhulumiwa, ipambane ili kujikomboa kutokana na unyonge, kudhulumiwa na kulinda heshima na utu wao. Dhamira hii ya mapambano ameizungumzia pia katika riwaya yake ya Kuli ambapo mhusika Rashidi na Mwenzake walianzisha mapambano dhidi ya Wazungu walio wakiwadhulumu Waafrika. Dhamira ya mapambano imeonyeshwa kupitia mhusika Denge akishirikiana na kikundi chake cha akina Mambo, Sukutua, Chande, Huseni, Pazi na Salehe. Denge na kundi lake wanaanzisha mapambano dhidi ya Serikali ya kikoloni ya Kiingereza ili kuleta ukombozi wa kisiasa katika nchi za Zanzibar na Bara la Afrika kwa ujumla. Tazama maelezo haya: "Basi lazima tutumie njia za siri kwani mapambano yetu ni ya vuta n'kuvute. Wao wanavutia kule na sisi tunavutia huku na katika mvutano huo, hapana suluhisho. Linaloweza kupatikana isipokuwa kuwa huru" (uk. 113). Maelezo hapo juu yanaonyesha jinsi Denge alivyodhamiria kupambanua na serikali ya kikoloni mpaka uhuru upatikane na kuweza kujikomba kisiasa. Kuonyesha kwamba, mwandishi amekusudia kuonyesha dhamira ya mapambano, tazama maneno ya Denge: "Haya ni mapambano, mapambano ya vuta n'kuvute, ni vita, tena vita vikubwa kila mmoja anamwinda mwenzake. Wao au sisi, lakini ushindi ni wetu, tutashinda tu"(uk. 122) Maelezo hayo yanaonyesha Denge na kikundi chake walivyodhamiria kupambana na serikali dhalimu ya kikoloni na kuleta ukombozi kwa wananchi wa Zanzibar. Tena Denge amekusudia hasa kupambana na anajipa matumaini lazima ushindi upatikane dhidi ya wakoloni. Kwa hiyo msanii anakusudia kuiamsha jamii isikubali dhuluma ya aina yoyote na iwe tayari kupambana kwa hali na mali kuhakikisha dhuluma inaondoka na kuleta haki na usawa ndani ya jamii. Vile vile Denge na kundi lake wamepambana dhidi ya ubaguzi kwa kupanga kufanya fujo na vurumai katika ukumbi wa karimjee "Karimjee club" ukumbi uliokuwa unaendeshwa kwa misingi ya kibaguzi. Ni ukumbi uliokuwa ukitumiwa na watu wa asili ya Kihindi. Denge na kundi lake walioamua kufanya katika ukumbi huo ili kuonyesha hisia zao za kupinga ubaguzi. anasimulia: "Lilianza vurumai kubwa na hapo hapo ilirushwa chupa nyingine iliyofuatiwa na mawe kutoka katika kila pembe. Kizilizala kikubwa kiliingia densini mle, watu wakaanza kutimka bila ya kujua wanakwenda wapi"(uk 136). Kwa hiyo Denge na wenzake walionyesha juhudi ya mapambano ya dhuluma ili waweze kujikomboa Kujitoa Muhanga kwa manufaa ya umma katika jamii Dhamira ya kujitoa muhanga imegusiwa sana na wasanii wa fasihi ya Kiswahili ili kuishajiisha jamii iwe tayari kujitolea kwa manufaa ya umma. Kwa mfano Mtolewa wa "Kivuli Kinaishi" alijitoa muhanga kupambana na uongozi dhalimu wa Bi - Kirembwe ili kukomboa wananchi wa Giningi. Vile vile Rashidi wa Kuli alijitolea muhanga kuwaongoza makuli kupambana na uongozi ukoloni uliokuwa ukiongoza bandari. Hiyo ni mifano michache katika fasihi ya Kiswahili. Hali kadhalika, msanii wa Vuta n'kuvute ameishughulikia dhamira hii ya kujitoa mhanga. Denge, Yasmin, Mambo na Zanga ni wahusika ambao wamejitoa muhanga kuendesha harakati za kupambana na wakoloni wa Kiingereza huko Zanzibar. Denge alijitoa muhanga kuendesha mapambano dhidi ya wakoloni wa Kiingereza. Serikali ya kikoloni ilikuwa na nguvu katika harakati zake. Denge alisafiri safari za hatari usiku kutoka Unguja kwenda Dar es Salaam kwa mashua, kwa ajili ya kusafirisha karatasi na vitabu vilivyokuwa vinawahamasisha wandugu waunge mkono mapambano ya kuing'oa serikali ya kikoloni. safari zao zilikuwa na mashaka makubwa, dhoruba, mawimbi makubwa lakini yote hayo Denge hakujali, alilokuwa anataka ni kupambana na kuikomboa jamii yake. Mfano Denge alisafiri safari ya kwenda Dar es Salaam kuchukua mashine ya kuchapia ambapo baada ya kurudi Unguja walikamatwa na askari wa kikoloni, Kabla ya kukamatwa Denge alisema" "Hii inaonekana madhubuti, sasa watatutambua, ikafika tu tutaanza kutoa gazeti" "Mtaliitaje" Kimbunga (uk. 224). Maelezo hayo yanaonyesha jinsi Denge alivyokuwa tayari kwa lolote, amejitolea muhanga kupambana mpaka uhuru upatikane. Mwandishi anaonyesha safari ya kutoka Dar es Salaam kurudi Unguja ilivyokuwa na misukosuko. “...Lakini kitaacha wapi kwenda mrama na mawimbi yalikuwa yakijizonga na Kujizongoa, yakajitandaza juu ya uso wa Bahari kwa kishindo; wakilipita wimbi hili Jingine liko tayari mbele yao. Safari yote Ikawa ya msukosuko mtupu usiku kucha"(uk. 225.) Msanii anataka kuonyesha jamii, katika harakati zozote kuna misukosuko kwa hiyo hakuna budi watu kujitoa mhanga ili kufanikisha harakati hizo, kama watu watarudi nyuma wakishindwa kujitoa basi mafanikio hayawezi kupatikana. Pia, Denge alijitoa muhanga kwa kupanga mipango na kwenda kwenye nyumba ya inspekta Wright kupekua na kuchuka data muhimu jambo ambalo liliichanganya serikali ya kikoloni na lnspekta Wright. Tazama mazungumzo kati ya Denge na Yasmini kuonyesha kwamba Denge amedhamiria kujitoa mhanga. Denge anamwambia Yasmini: " Hii ni kazi ngumu, ina matatizo mengi na inahitaji kujitolea muhanga na mimi ni miongoni mwa hao waliojitolea mhanga, kufa kupona, potelea mbali..." (uk. 145) Yasmini pia ameonyesha dhamira ya kujitoa mhanga kutokana na vuta n'kuvute ya kisiasa. Yasmini alikuwa ameshawishiwa na Koplo Matata shirikiane na polisi ili kumkata Denge. Koplo Matata alimpa karatasi yaliyoandikwa uchochezi iii ayaweke kwenye chumba cha Denge ili iwe njia ya kumkata. Makaratasi hayo yaliandikwa hivi: "Sisi makomonisti wa visiwa hivi tunaapa kupindua serikali na siku hiyo tutamuua sultani" (uk. 154). Yasmini badala ya kuweka karatasi hizo kwenye chumba denge kwa kificho bila Denge kujua ili polisi wa kikoloni wamkate,Yasmini alimkabidhi karatasi hizo Denge na kumwambia mambo yote waliyozungumza na Koplo Matata, na Denge akachukua tahadhari. "Waliingia ndani na baada ya kuingia tu Yasmini alimkabidhi Denge yale makaratasi. "Koplo Matata kaniambia niyalete kwako lakini wewe usijue kama nimeyaleta" (uk. 154). Kitendo alichokifanya Yasmini ni cha kujitoa mhanga kunusuru maisha ya Denge na kunusuru harakati za mapambano.kusaliti Makubaliano na polisi tena wa kikoloni ni kujiota mhanga Ina maana Yasmini alikuwa tayari kwa lolote kutoka kwa polisi maana hakujali kukamatwa au kuchukuliwa hatua yeyote na polisi Ikizingatia wanamjua kwa kila kitu. Mambo naye alijitoa mhanga kupeleka karatasi bandarini ili zisafirishwe kwenda Pemba kwa ajili ya kuwahamasisha wananchi wapiganie na kudai uhuru wao. Karatasi zenyewe zilikuwazimeandikwa hivi; "Kufa au kupona tunataka uhuru" "Ndiyo, kufa au kupona tunataka uhuru..." (uk. 186) Karatasi hizo zilitakiwa zibandikwe nchi nzima, Unguja na Pemba. Mambo alichukua karatasi hizo bila kuogopa ili kuzipeleka melini kwa kijana mmoja ambaye alizisafirisha kwenda Pemba. Mambo alifanya kazi ya hatari, maana bandarini kulikuwa na ulinzi na angeweza kushikwa na kuchukuliwa hatua, lakini alisukumwa na moyo wa uzalendo kuendesha mapambano hadi uhuru upatikane. Msanii anasimulia: "Ilipofika saa mbili za usiku Mambo akawa yumo safarini anakwenda gatini, wasiwasi umemjaa lakini kila akifikiri imani aliyekuwa nayo kwa Denge wasiwasi ulimpungua."(k. 187). Maelezo hayo yanayoonyesha namna gani Mambo alikua amejitolea kufanya kazi ya hatari alimradi harakati za mapambano zisonge mbele. Ushirikiano katika harakati za kudai uhuru kwenye jamii Kushirikiana katika harakati za kudai uhuru dhidi ya dhuluma ni dhamira iliyoshughulikiwa na msanii katika kuijenga dhamira kuu ya mapambano. Dhamira hii imeshughulikiwa na wasanii mbalimbali katika fasihi ya Kiswahili na Afrika kwa ujumla Kwa mfano msanii mkongwe Marehemu Saadani Kandoro katika diwani yake ya "Mashairi ya Saadan" katika harakati za kudai uhuru wa Tanganyika alitunga mashairi yaliyokuwa yakiwataka wananchi wawe na umoja na mshikamano katika kupigania uhuru, mfano shairi la "Waafrika Njooni." Liliwataka wananchi wajitokeze kukiunga mkono chama cha TANU katika kupigania uhuru. Wanyonge na wanaodhulumiwa wanatakiwa waungane pamoja wawe na nguvu moja katika kupigania haki zao. Shafi Adamu Shafi katika Vuta n'kute ameishughulikia dhamira hii kwa kumuonyesha Denge na kikundi chake jinsi walivyookuwa na ushirikiano katika harakati zao za kupambana na wakoloni wa Kiingereza. Denge , Mambo, Sikutuwa, Chande, Husein, Mwajuma, Yasmini, Zanga, Pazi wameonyesha umoja na mshikamano wa hali ya juu katika kuendesha harakati zakupambana na ukoloni. Wameshirikiana katika kusafirisha na kusambaza karatasi za kuwamasisha wananchi kudai uhuru (uk. 187), Wameonyesha ushirikiano kumuokoa Denge asikamatwe na polisi kutokana na mtego uliowekwa na polisi wa kumtumia Yasmini kuweka karatasi za uchochezi ndani ya chumba cha Denge. Mambo, Chande na yasmini walishirikiana wakazichoma moto zile karatasi za uchochezi, Denge akaondoka na Chande akaenda kulala kwenye chumba cha Denge, ambapo polisi walipofika katika chumba hicho Denge walikosa kidhibiti na kuondoka zao (uk. 159). Katika kuonyesha vijana hawa walikuwa wana umoja na mshikamano tazama mazungumzo kati ya Chande na Denge. "Wakifiri hivyo n'do barabara, lazima wajue kwamba hakuna hata mtu mmoja katika nchi hii ambaye yuko pamoja nao, lazima sasa waelewe kwamba Denge huko peke yako." (uk.156) Maelezo yanaonyesha Denge katika harakati za kupambana na wakoloni hayuko peke yake, kuna watu wengie wanashirikiana na ndio ushirikiano unaotakiwa katika kuendesha mapambano ya dhuluma. Pia ameizungumzia dhamira hii kwa kuonyesha ushirikiano waliokuwanao wafanyakazi katika kulaani ukoloni. Siku ya Mei mosi walibeba vitambaa na mabango yaliyoandikwa kwa maneno ya kuhimiza kuungana kwa wafanyakazi kulaani ukoloni (uk. 139). Kwa hiyo msanii anasisitiza umoja unahitajika katika makundi yote ya kijamii ili kufanikisha mapambano dhidi ya dhuluma. Msanii anaonyesha wanyonge kokote walipo, lazima waungane na washirikianekupinga dhuluma. Tazama mazungumzo denge "Mia moja" Denge alishangaa, "Vijana kama mimi na zaidi yangu mimi wapo zaidi ya alfu moja, wapo ndani ya Zanzibar na nje ya Zanzibar. Kila mmoja wao ana mchango wake anaotoa katika kufanikisha mapambano yetu. " (uk.113). Maelezo hayo yanaonyesha kuwa akina Denge walifanya harakati zao kwa umoja na ushirikiano mkubwa ndani na nje ya Zanzibar. Na huo ndio umoja na ushirikiano anaouonyesha msanii katika riwaya yake hii. Mbinu/Mikakati ya Kuyaendea Mambo katika jamii Suala la mbinu, mikakati, mipango kwa ajili ya kuyaendea mambo mbalimbali, mfano mapambano limeshughulikiwa na msanii. Shafi A. Shafi anaelimisha jamii kuwa utekelezaji wa jambo lolote lazima lipangiwe mikakati na sio kujiendea ovyo. Denge na kikundi chake wameonesha mbinu na mikakati mbalimbali waliokuwa wakiipanga na kuifanya katika harakati zao za kupambana na ukoloni wa Kiingereza. Katika harakati zao za mapambano, akina Denge walitumia mbinu mbalimbali, miongoni mwao ni: Kusambaza karatasi vitabu vya kuihamasisha jamii kupigania uhuru. Walifanikiwa kusafirisha na kusambaza na kuyabandika karatasi katika Unguja na Pemba kwa siku moja, jambo ambalo liliichanganya serikali ya kikoloni chini ya Inspekta Wright (uk.189). Chande na Hussein walipanga mbinu ya kumuokoa Denge asikamatwe na polisi baada ya polisi kumuwekea mtego Denge kumuingizia karatasi ya uchochezi chumbani mwake ili akamatwe. Denge alipangiwa mpango akaondoka, chumba cha Denge kikasafishwa, siku hiyo Chande alilala katika chumba cha Denge, Polisi walipofika kumkamata (Denge) hawakumkuta badala yake walimkuta Chande na karatasi walizozitarajia hawakuziona chumbani mle. (uk. 159). Bukheti, Mambo, Yasmini na Fikirini walipanga mbinu ya kumtoa gerezani Denge alikokuwa amefungwa na wakafanikiwa. na Bukheti na Mambo wakafanikiwa kumtoa Denge toka gerezani kumsafirisha ughaibuni ambako alikwenda kuendelea na harakati za kudai uhuru (uk. 240 - 244). Mwandishi ametuonyesha mbinu nyingine aliyotumia katika harakati zao za kupambana na ukoloni ni Denge alijibadili sura ili kukwepa kukamatwa na polisi. "Denge hakuwa na wasiwasi wowote, kwani alikuwa na hakika kwamba hakuna mtu yoyote atakayeweza kumtambua kwa jinsi alivyobadilika.Uso wake ulizungukwa na sharafa ya ndevu zilizoungana na nywele kubwa zilizochanwa vizuri zikapasuliwa njia upande wa kushoto. Miwani myeusi iliyofunika macho yake yakawa hayaonekani..." (uk. 173) Mbinu hii ilimfanya Denge aweze kutua uwanja wa ndege Zanzibar akitokea ughaibuni bila kujulikana na hakuweza kukamatwa mpaka akafika nyumbani kwake, na akaendelea na harakati za kudai uhuru. Katika ukurasa 113 msanii anaonesha ni jinsi gani kina Denge waliendesha mapambano yao kwa kutumia mbinu mbalimbali ambazo ziliwasumbua na kuwanyima raha wakoloni. Tazama maelezo haya: "Siku tunaleta magazeti au vitabu hawawezi kutugundua hata kidogo, kwani wana mbinu gani zilizokuwa za ubingwa zaidi hata tusiweze kuzipiku? Tushaingiza vitu vingapi bila ya kukamatwa navyo? tushatorosha vijana wangapi waliokataa kuwapa paspoti na sasa wako nje wanasoma? (uk. 113) Maelezo hayo yanayoonyesha kwamba katika harakati za kupigania au kupambana na dhuluma lazima wapambanaji wawe na mbinu na mikakati mbalimbali katika kuziendea hizo haraka iwezekanavyo hawatafanikiwa. Uongozi mbaya katika jamii Suala la uongozi mbaya limeshughulikiwa na Shafi Adam Shafi kama ambavyo waandishi wengi wa fasihi ya Kiswahili wanavyolizungumzia katika mitazamo mbalimbali. Mara nyingi uongozi mbaya huelezewa kuwa ni ule unaokandamiza, kunyanyasa, kudhulumu na unajihusisha na ufisadi na ulaji rushwa. Mwandishi wa Vuta n'kuvute amelishughulikia suala hili kwa kuonyesha uongozi mbaya wa serikali ya kikoloni dhidi ya wananchi wa Zanzibar na Bara zima la Afrika. Mwandishi ameonyesha pamoja na dhulurna nyengine ambazo hufanywa na uongozi mbaya, amegusia jambo moja ambalo uongozi wowote mbaya huwa unalifanya ambalo ni hila na visingizio kwa raia. Shafi Adam Shafi ameonyesha jinsi uongozi mbaya unavyoweza kuongoza kwa kutumia hila na uongo kwa kuwazushia raia ili iweze kuwaadhibu.Katika riwaya hii, serikali ya kikoloni kupitia jeshi la polisi inatumia hila kumsingizia Denge kuwa ni komonist, hamjui Mungu na anataka kumuua sultani, ili waweze kumkamata Denge na kumtia gerezani asiendelee na harakati za kupigania uhuru. Tazamamaelezo haya: “furaha ilioje aliyokuwa nayo Inspekta siku ile, kwani kwa visingizio tu, yeye alikuwa navyo vingi na kisingiziocha kumkamata Denge yeye hakitompa shida (uk. 153). Maelezo hayo ya Inspekta Wright yanathibitisha ni kwa jinsi gani uongozi mbaya na wa kidhalimu huongoza kwa hila na wasingizia raia wema mambo mbalimbali ili kuweza kuwatisha na kuwadhibiti. Uongozi mbovu kama huu ndio unaoifanya dunia leo kuwepo na machafuko ya mara kwa mara. Dunia haina amani kutokana na uongozi unaoongoza kwa hila na visingizio. Inspekta Wright alimzuishia Denge kwa kuandika vikaratasi vya uchochezi na kumpa Koplo Matata avipeleke nyumbani kwa Denge bila yeye (Denge) kuwa na habari halafu askari wafanye upekuzi kwenye hicho chumba na Denge akamatwe.vikaratasi alivyokuwa ameviandika Inspekta Wright kwa ajili ya kumsingizia Denge viliandikwa hivi: "Sisi makomonist wa visiwa hivi tunaapa kuipindua serikali na siku hiyo tutamuua Sultani" (uk. 154). Maneno yaliyoandikwa kwenye vikaratasi hivyo vilivyoandikwa na Inspekta Wright yalikuwa ya kumchonganisha Denge na serikali na jamii kwa ujumla. Denge aonekane mtu mbaya, muuaji na anayetaka kupindua serikali hivyo iwe halali vyombo vya dola kumdhibiti na jamii inayomzunguka isimuhurumie na kumuona hafai. Tazama maelezo haya yaDenge: "Ukisema kweli wewe komonist. Ukipinga kutawaliwa wewe koministi. Lolote utakalolifanya madhali halina maslahi kwao basi wewe kominist. Mau Mau wa Kenya wameitwa komonisti, wapigania uhuru wa Algeria wameitwa makominist. Kila anayedai haki kwao ni koministi, na sumu yao kubwa wanayoitumia ya kutaka kuwiitenganisha watu kama hao na wananchi wenzao ni kusema kwamba watu hao wanaowaita makomunist hawaamini Mungu" (uk. 68). Maelezo hayo yanaonesha namna gani uongozi mbaya unavyoweza kuzua visingizio kwa raia wake kwa lengo unavyoweza kuwatenganisha raia wanaowazulia visingizio na raia wenzao na wasiweze kupata msaada toka kwa raia wenzao na waonekane hawafai ndani ya jamii ili serikali itakapowadhibiti raia iliyowawekea visingizio raia wengine waone ni sawa kwa wenzio kutendewa hivyo. Kwa hiyo mwandishi anaitahadharisha jamii iwe macho na uongozi wa namna hii, wachunguze kwa makini kila kauli ilivyotolewa na serikali dhidi ya raia au kundi fulani ndani ya jamii,, vinginevyo uongozi wenye hila na visingizio utakuwa unasingizia raia wema na jamii ikawaona raia hao hawafai kumbe ni kwa maslaihi ya uongozi ni si kwa wananchi. Ubaguzi katika huduma za jamii ndani ya nchi Dhamira nyingine inayotokana na vuta n'kuvute za kisasa aliyeshughalikia msanii ni ubaguzi. Siasa za kikoloni chini ya inspecta Wright zilikuwa zinatofautiana na siasa za akina Denge na raia wa Unguja waliokuwa wanapinga na kupambanana ukoloni. Kutokana na mvutano huo, serikali ya kikoloni iliwabagua waafrika na kuweka sera za kibaguzi. Ubaguzi ulionyeshwa katika huduma za kijamii na sehemu za starehe. Kulikuwa na kumbi starehe ambazo ziliendeshwa kwa misingi ya ubaguzi. Ukumbi wa english Club ulikuwa ukitumiwa na Wazungu na watu watu wa hadhiya juu. "Karimjee Club' ni ukumbi uliokuwa unatumika na watu wenye asili ya Kihindi, na sehemu zote hizo Waafrika hawakuruhusiwakuingia kwenda kustarehe kwenye kumbi hizo. Kumbi za Waafrika walizokuwa wakitumia kustarehe ni kama mwewembetanga, kwa Mzee Kiroboto, sehemu ambazo zilikuwa duni kukiuzwa pombe za kienyeji na fujo nyingi. Pia kuna ubaguzi katika ajira. Denge anabaguliwakutokana na kwamba yeye (Denge) amesomea Urusi nchi ya kikomunist ambayo inapingana kiitikadi na siasa za Uingeleza serikaliya kikoloni ya Kiingereza ilimbagua Denge katika ajira kwa kumuona ni komunisti hivyo haendani na itikadi za kibepali matokeo yake Denge alikosa ajira pamoja na elimu aliyokuwa nayo abaki akiishi katika hali ngumu. Hata katika jeshi la polisi la koloni kulikuwa na ubaguzi. Wazungu ndio waliokuwa na vyeo a juu mfano Inspekta Wright na Waafrika walikuwa katika azi za chini mfano Koplo Matata. Uvunjaji wa Haki za Binadamu katika jamii Suala la uvunjaji wa haki za binadamu limeshughulikiwa na Shafi Adamu Shafi. Mwandishi ameonyesha ni jinsi gani serikali kupitia vyombo vya dola kama polisi na magereza zinavyo dhalilisha utu wa binadamu. Polisi na Magereza zina kanuni na sheria azowaongoza katika kukamata wahalifu na kuchunguza wafungwa wakiwa gerezani. Lakini vyombo hivi vimekuwa mstari wa mbele katika kuvunja haki za binadamu. Kwa mfano, Denge alivamiwa usiku nyumbani kwake askari wakiongozwa na Inspekta Wright, ambapo askari aliusukuma mlango, Denge alipofungua mlango, akiwa amevaa chupi tu akapigwa kofi na Inspekta, kabla hajakaa sawa akapigwa kofi jingine akabebwa kitikiti na kutupwa ndani ya gari (uk. 191). jambo hili ni uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu. Denge alipofikishwa kituo cha polisi aliamrishwa avue nguo. "Vua nguo!" askari mmoja alimwamrisha Denge. "Nakwambia vua nguo" aliamrisha tena yule askari" denge ikabidi atii ale amri, akavua chupi na kubaki uchi. Yule askari alimgeuza geuza akamwambia tena "Vaa nguo zako" (uk. 191) Kumkamata mtu akiwa na nguo ya ndani tu ni kuvunja haki zabinadamu. Kitendo cha askari wawili kumpiga makofi Denge ni uvunjaji wa haki za binadamu. Kitendo cha askari kumuamuru denge avue nguo na kubaki uchi kama alivyozaliwa ni udhalilishaji mkubwa na uvunjaji mkubwa wa haki za binadamu. mwandishi anaionyesha jamii ni jinsi gani vyombo vya dola vinavyokiuka haki binadamu. Vile vile mwandishi ameonyesha jinsi gani walinzi wa (askari magereza) wanavyokiuka sheria na kuvunja haki za binadamu Tazama jinsi walinzi wa jela walivyomdhalilis mfungwa mmoja ndani ya jela: "Wakaingia walinzi wa jela wanne waliombeba mfungwa mmoja kitikiti na marungu yao mkononi. Walimtupa chini wakaanza kumpiga marungu bila yahuruma wala kujali kama yule wamtesae ni kiumbe mwenzao. Mlinzi mmoja alimpiga teke la kiunoni, mwingine akamkanyaga shingoni, mwingine akamtandika rungu tumboni. Mfungwa yule alipiga kelele mpaka nguvu zikamuishia akabaki kukoroma kama anayekata roho (uk.234) Maelezo hayo yanazidi kuthibitisha uvunjifu wa haki za binadamuunufanywa na vyombo vya dola. Sidhani kama kuna sheria ya askari wanne kwa pamoja kumshambulia kwa marungu na mateke mfungwa hasa akiwa chini ya himaya yao. Huo ni uvunjaji wa haki za binadamu. Binadamu hastahili kushambuliwa namna ile, pia anaonyesha mazingira wanayoishi wafungwa ndani ya magereza ni ya udhalilishaji na uvunjaji wa haki za binadamu, Mwandishi anasimulia mazingira wanayoishi wafungwa "Chumbani mle mhjaa harufu ya uvundo. Mlikuwa na virago vilivyokunjwa upande mmoja vitano na upande mwingine vitano au pembeni kabisa palikuwa na ndoo.... lakini alipoikaribia harufu ya uvundo ilizidi na ndoo ile ilikuwa tupu (uk. 192) Maelezo hayo yanaonyesha namna gani wafungwa Wailopokuwa gerezani wanaiShi katika mazingira mabovu, hakuna Vitanda wala magodoro, sehemu ya kujisaidia ni humo humo wanamolala Huku ni kuvunja haki za binadamu. Pia Denge alipokuwa gerezani aliingizwa kwenye chumba chenye giza akavuliwa nguo zote akawa uchi, chumba hicho kina.joto mchana kutwa na baridi kali sana wakati wa usiku jambo lililomfanya Denge aishi katika hali ngumu sana (uk. 236). Kwa ujumla msanii anataka kuonyesha jamii ni jinsi gani vyombo vya dola vinavyotumia mamlaka yao vibaya kuvunja haki za binadamu. VUTA N'KUVUTE ZA KIJAMII Katika riwaya hii vuta n'kuvute za kijamii zimeshughulikiwa na msanii. Mambo ya kijamii ni yale yanayohusu mahusiano, ndoa, mapenzi, urafiki, ujirani n.k. Msanii kaonyesha vuta n'kuvute ya marafiki..wawili, Yasmini na Mwajuma, vuta n'kutuve kati wanandoa Mzee Raza na Yasmini, Vuta n'kuvute kati ya Shihabu Yasmini na Vuta n'kuvute kati ya wapenzi wawili Bukheti na yasmini; Pia msomaji anaweza kufanya utafiti na kupata vuta n'kuvute nyingine za kijamii. Katika vuta n'kuvute hizi za kijamii zinazoelezea ndani ya kitabu, zimeweza kualibua dhamira zifuatazo: ndoa za lazima / Mapenzi ya lazima, Mapenzi ya dhati, Wivu katikandoa, Ukandamizaji wa mwanamke na Usaliti katika ndoa. Ndoa za Lazima katika jamii Suala la ndoa za kulazimisha limeshughulikiwa na mwadishi kwa kuonyesha ndoa kati ya Yasmini na Mzee Raza. ni alilazimishwa na wazazi wake aolewe na Mzee Raza. Ndio a ndani ya ndoa yao hakukuwa na amani, ndoa yao haikuwa na kila siku ndani ya nyumba kulikuwa na malumbano. Ndoa yao kulazimishwa ilikuwa ya vuta n'kuvute. Tazama jinsi ndoa hii ya ilivyokuwa ya vuta n'kuvute.
- "Usinikere Bwana mimi nataka kulala" "Mbona unalala mapema? N'do kwanza saa mbili. Amka tuzungumze, "Bwana Raza alinguruma, Yasmini alimpuuza akalala" (uk.3).
- Kutokumpenda Bwana Raza pamoja na utumishi wa kutwa dukani pake kulimfanya Yasmini ayachukie maisha ya unyumba na mumewe" (uk. 2)
- "Bwana Raza hakuwa na raha ya kuwa na mke na Yasmini ya kuwa na mume. Maisha ya watu wawili hawa yalikuwa ya bahati nasibu na hakuwa mmoja kati yao aliyekuwa na raha " (uk.4)
Maelezo yote hayo yanaonyesha ndoa kati ya Yasmini na bwana raza haikuwa na amani, raha wala starehe. Na hii yote ni kwasababu bwana Raza alilazimisha kumuoa Yasmini, binti mdogo mwenye umri wa miaka 15 ambaye hakumpenda kabisa bwana raza aliyekuwa na umri wa miaka 52. Mapenzl ya Dhati katika jamii Suala la mapenzi ya dhati limeshughulikiwa pia na Shafi adamu Shafi, Yasmini alikuwa na mapenzi ya dhati kwa Denge alimpenda sana Denge kwa kuwa alikuwa kijana mwenzie, mchapakazi na mpambanaji. Hakujali hali ya kimaisha aliyokuwa kuwanayo denge alikuwa masikini, hana kazi, anaishi katika chumba kimoja ambacho kila siku kilikuwa kichafu. Yote haya Yasmini haku hakujali bali alionyesha mapenzi ya ukweli kwa Denge. Malumbano hatimaye kupigana kati ya Yasmini na rafiki yake Mwajuma.kuonyesha jinsi gani Yasmini alivyokuwa na mapenzi ya dhati kwa Denge. Mwajuma alijaribu kumshawishi Yasmini akukubali kuolewa na shilab bin antar na hapo ugomvi ndipo ulipo ibuka maneno ya Mwajuma. "Aaam babu we! Denge, Denge, unafikiri Denge atakupa nini, mtu mwenyewe hohe hahe, matatizo matupu, heshi kuandamwa na maaskari utafikiri mwizi." (uk.169) Maelezo hayo ni maneno ya Mwajuma akimshawishi yasmini aachane na Denge na akubali kuolewa na Shihab.sikiliza majibu ya Yasmini: "Lakini si mwizi"Yasmini aliyadakia maneno. "Wanamwonea tu, na mimi mwenyewe nimehakikisha kama wanamwonea." (uk.169) Maelezo hayo yanaonyesha jinsi Yasmini alivyokuwa na huruma na Denge na jinsi anavyompenda Yasmini anaendelea: "Mwajuma usikasirike,tuombe Mungu anijaaliye niijifungue salama na hata wakati huo naamini Denge atakuwa amekwisharudi, popote pale atakapokwenda, nitamshauri nimsikilize ataniambia nini (uk. 170). Tazama majibu ya Mwajuma: "Na weye nawe na Denge wako, kila uambiwalo,Denge, Denge, unafikiri Denge atakupa nini?Yeye mwenyewe hana mbele hana nyuma,riziki inakuja hivi hivi unaipiga teke,na kama hukuolewa sasa unafikiri utaolewa lini?Mwajuma alimkaripia utafikiri mtoto mdogo." (uk.170) Mwajuma anamkasirikia Yasmini kwa kuonyesha msimamo wake wa kumpenda kwa dhati Denge hivyo kwa nini akatae kuolewa na bahati imefika? Kwa upande mwingine, hata Mwajuma anaonesha ana mapenzi ya dhati kwa Yasmini. Mwajuma anaumia, anamuonea huruma Yasmini, bahati ya kuolewa imepatikana kwa nini rafiki yake kipenzi asiolewe akaondokana na ujane na dhiki alizokuwa nazo? tazama maneno ya Mwajuma: "Yasmini utaishi mjane mpaka lini? kupata mwanamume akataka kukuoa si rahisi siku hizi. Unafikiri mimi! mwenyewe napenda kuishi kama hivi ninavyoishi? Natamani na mimi ningelikuwa na mume wangu. (uk.170). Maelezo hayo yanaonyesha Mwajuma alikuwa akimuhurumia rafiki yake, hakutaka rafiki yake aendelee kuishi maisha ya ujane na dhiki kama zile, ndio maana alikasirika kwa uchungu kuona rafiki yake amepata bahati na kutaka kuichezea. Pamoja na malumbano hayo marafiki hawa walipatana na kuonesha kuwa wana mapenzi ya dhati na baadaye Yasmin akaolewa na Shihab. Hata Yasmini alipoolewa na Shibah alikuwa bado anamkumbuka Denge. Mapenzi ya dhati mengine yameonyeshwa kwa Denge na kundi lake kuipenda nchi yao na kuanza harakati za kupambana na wakoloni ili kupatikane uhuru wa kweli wa wananchi wa Zanzibar pia vuta n`kuvute kati ya Bakheti na Yasmini inaonyesha mapenzi ya dhati ya yasmini kwa denge(uk231) Pia Bukheti alikuwa na mapenzi ya dhati kwa yasmini bukheti alisafiri mara mbili toka Mombasa kwenda Unganda kumfatilia Yasmini. Bukheti alikubali masharti yote aliyopewa na yasmini ili amuoe likiwemo la kumtoa Denge gerezani, wakati alikuwa akijua yasmini na Denge walikuwa na uhusiano. Wivu katika Ndoa kwenye jamii Mwandishi pia amezungumzia suala la wivu katika ndoa Wivu katika ndoa ni chachu ya ndoa lakini wivu ukizidi sana huleta madhala ndani ya ndoa. Ndoa ya Shihab na Yasmini imetawaliwa na wivu wa kupindukia kiasi ambacho raha ya ndoa miongoni mwa wana ndoa hawa ikakosekana. Shihabu mume wa Yasmini alikuwa na wivu sana. Mwandishi anasema: "Wivu wa Shihab ulikuwa ni ila yake kubwa aliyoijua kila mwanamke mjini Tanga na kwa sababu ya wivu wake huo, alikwisha waacha wanawake watatu na Yasmini sasa ni mke wake wa nne. Alimpa kila starehe ila uhuru wa kutoka, na starehe zake ziliishia ndani ya nyumba yake kubwa iliyokuwa na kila aina ya anasa ndani yake, zote asizione kitu, kubwa akawa aning'inia madirishani. "(uk. 197). Maelezo hayo yanaonyesha Shihab alivyokuwa na wivu wa kupindikia na tabia yake hiyo ilimfanya ashindwe kuishi na nawake, alikwisha aachana na wanawake watatu kutokana na tabia yake ya wivu. Kutokana na wivu wa kupindukia wa Shihab, yasmini alinyimwa uhuru wa kutoka nje hadi akakumbuka maisha yake ujane aliyokuwa akiishi na Mwajuma. Kuhusiana na wivu aliokuwa nao Shihab: "Nisikonde! Mwanaume yule! Ana wivu, ana gubu, ana nongwa kama mwanamke" Yasmini alilalamika." Nakwambia kaniweka ndani kama mwari, hata huyo mwali ana afadhali, sina shoga , sina jirani, sina jamaa, mimi na ndani na ndani na mimi, siendi sirudi (uk. 211) Maelezo hayo yanaonyesha Shihab alikuwa mume mwenye wivu sana ambapo uliwanyima uhuru wake aliowaoa. Wivu wa kupindukia wa Shihab ndio ilikuwa chanzo cha kifo chake. (Uk. 15). Ukandamizaji wa Haki za Wanawake katika jamii Suala la ukiukwaji na ukandamizaji wa haki za wanawake ndani ya jamii limeshughulikiwa na msanii kupitia ndoa mbili, ambazo ni ndoa kati ya Bwana Raza na Yasmini na nyingine. shlhab na Yasmini. Suala la ukandamizaji haki za wanawake limezungumziwa sana na wanafasihi wa Kiswahili Ikiziingatiwa jamii imepitia na bado imo katika mfumo dume. Shafi Adamu Shafi ameonyesha namna gani mwanamke aliyenyimwa haki kwa Yasmini kulazimishwa kuolewa na Raza , Yasmini hakupewa nafasi na uhuru wa kuolewa na mwanaume aliyempenda kwa dhati yake (uk. 1). Pia bwana Raza kama mwanaume ndani ya nyumba alimtumikisha mkewe (Yasmini) kama mashine Jambo ambalo jamii nyingi za Kiafrika humfanya mwanamke ni chombo ulizalisliaji mall, na mwanaume ni mtu wa kufaidi matunda yallyozalisliwa na mke katika familia. Hali hii ni kumkandamiza Mwanamke. Yasmini alikuwa anatumika kutwa nzima dukani jambo ambalo hakulifurahia na kupelekea kuzidi kuichukia ndoa yao. "Kutompenda Bwana Raza pamoja na uturnishi wa kutwa dukani pale kulimfanya Yasmini ayachukia maisha ya unyumba wake" (Uk.2) Bwana Raza alimfanya Yasmini ni mtumishi wa kwake, na si mke mwenye hadhi. Ndoa kati ya Shihab na Yasmini nayo inaonyesha jinsi mfumo dume unavyokandamiza kunyima haki za wanawake ndani ya familia. Shihab kama mume alimnyima uhuru mkewe wa kutoka nje ya nyumba, kuwasalimia watu wengine na hata kujishughulisha na shughuli nyingi kijiongezea kipato katika familia. Shihab alimlazimisha Yasmin akae ndani tu na hakuna ruhusa ya kutoka nje na alijisifia kitendoo hicho. Kumnyima uhuru mwanamke wa kutoka nje ya nyumba au kumfungia mwanamke asitoke ndani ya nyumba au kufungia mwanamke ndani ya nyumba ni ukiukaji wa haki wanawake ndani ya familia. Yasmini pamoja na kuwa kwenye nyumba nzuri na inakila kitu, lakini alinyimwa uhuru, jambo ambalo lilimhuzunisha Soma maelezo haya: “Alijiona kama ndege aliyefungiwa tunduni akapewa kila kitu isipokuwa uhuru wake wa kuruka hewani alihisi Shihab alikuwa kama aliyemtupia mshipi, akaumeza pamoja na ndoana, chambo na chubwi. Sasa amenasa, ni mahabusu wake, si huru tena wa kwenda apendako, na nyimbo za taarabu ambazo alikuwa bingwa wa kuziimba kwenye tafrija za chama cha Cheusi Dawa sasa akawa anaziimba chumbani tu na badala ya kumletea furaha na msisimko sasa zikawa zinamletea mawazo na simanzi..." (uk. 197). Maelezo hayo yanaonyesha jinsi Shihab alivyomnyima uhuru mke wake hata akajiona kama mfungwa ndani ya mahabusu hali hiyo ilimfanya Yasmini aishi kwa majonzi makubwa. Jambo la kujiuliza kwa nini mwanamke ndio afungiwe ndani tu. Pamoja hayo Yasmini aliyazoea maisha hayo ya kifungo: "Taratibu Yasmini aliyazoea maisha ya utawa, akawa mke wa nyumbani aliyewekwa akakaa, akatulia na Shihabu akawa anajisifu kwa rafiki zake wote" Safari hii nimepata mke" (uk. 198) Shihab kujisifu kuwa amepata mke hali anamfungia ndani na kunyima uhuru wa kutoka nje ni kumdhalilisha na kumkandamiza mkewe. Usaliti katika Ndoa kwenye jamii Usaliti katika ndoa ni dhamira iliyoshughulikiwa na mwandishi. Jambo hii linajitokeza sana katika jamii tunamoishi. wanandoa katika jamii tunamoishi baadhi yao si waaminifu hivyo huzisaliti ndoa zao. Na usaliti katika ndoa unaweza kusababishwa na mambo mbalimbali, inawezekana miongoni mwa mambo hayo wa wivu. Yasmini mke wa Shihab anasaliti ndoa yake, kumuaga mewe (Shihab) anakwenda Unguja kuwaangalia wazazi wake kumbe alikuwa anataka kwenda kumuona Denge mzazi mwenzie. “Yasmini alimshawishi mumewe akashawishika, akawashika akalaghaika, akawa kama aliyezugwa akaamini kabisa kwamba anakwenda Unguja mara moja kuwaangalia wazee wake" (Uk. 210). Maelezo hayo yanaonyesha kuwa Yasmini alifanya usaliti kwa kumlaghaimume wake. Yasmini alipofika Unguja na kumkuta Denge, akahamia kabisa kwa Denge akaishi miezi miwili wakati ruhusa aliomba kwenda unguja mara moja na kurudi kwake tanga. Mwandishi anaeleza: siku ni usiku ule, usiku aliyolala na kuamka na Denge. Siku ya pili akahamia kwake akawa ni wa kupika na kupakua" (uk.214). Maelezo hayo yanaonyesha ni namna gani Yasmini alifanya usaliti ndani ya ndoa. Kumuacha mume wake Tanga alifika Unguja anaishi kinyumba na mume mwingine. Hata kama alikuwa na mapenzi ya kweli kwa Denge, maadamu aliolewa na mume mwingine (Shihab) hakuruhusiwa kufanya hivyo katika ndoa, jambo ambalo lilisababisha kifo cha mume wake bwana Shihab ambaye alifariki kwa kihoro. VUTA N'KUVUTE ZA KIUTAMADUNI Kuna vuta n'kuvute za kiutamaduni ambazo zinaonyeshwa migongano baina ya tamaduni moja na tamaduni nyingine. mgongano kati ya utamaduni wa Kiafrika na wa Kihindi ,migongano kati ya utamaduni wa vijana na utamaduni wa …, mfano kuna vuta n'kuvute kati ya Yasmini na wazazi wake. Vuta n'kuvute kati ya Bukheti na Bashiri. Vuta n'kuvute za kiutamaduni zimeweza kuibua dhamira zifuatazo: Kuchaguliwa mme Ubaguzi wa rangi na utii kwa wazazi. Kuchaguliwa Mme/Mke katika jamii. Suala la vijana kuchaguliwa mke wa kuoa au mume wa kuolewa limeshughulikiwa na msanii wa riwaya hii. Utamaduni ulioje katika jamii nyingi hasa za Kiafrika ni wazazi kuwachagulia watoto wao wake au waume kwa ajili ya ndoa. Utamaduni huu ulishazoeleka lakini kwa sasa umeshapitwa na wakati na hivyo kusababisha migogoro ya kifamilia. Wazazi wa Yasmini walimchagulia binti yao mume wa kumuoa, mume mwenyewe alikuwa na umri mkubwa ukilinganisha umri wa Yasmini. Yasmini hakuridhika na mume aliyechaguliwa na wazazi wake ndio maana ndoa yenyewe haikudumu. Yasmini aliondoka kwa Mzee Raza. Msanii anaeleza: "Mara tu baada ya kuvunja ungo, Yasmini aliozwa mume. Alikuwa mume wa jamii yake ya lthanaashiria ambaye alikuwa akiishi jirani naye hapo Mtendeni."(uk.1) Maelezo hayo yanaonyesha wazazi wa Yasmini kutokana utamaduni uliojengeka walimchagulia binti yao mume ambaye yeye mwolewaji hakumpenda wala hakuridhika naye. Yasmini baada a kushindwa kuishi na Bwana Raza na kurudi kwa wazazi wake, walimfukuza kwa kuwa alionekana amevunja mila na utamaduni wao. Tazama jinsi mjomba wake Yasmini alipomfukuza Yasmini nyumbani kwake baada ya kurudi unguja toka kwa Mzee Raza: "hapa palikuwa kwenu kabla hujaolewa.Sisi tulikupa mume ili tupungukiwe na mzigo. Sasa madhali umemkimbia mumeo, tafuta pa kwenda" (uk. 18). Maelezo hayo yanaonyesha jinsi wazazi walivyong'ang'ania utamaduni wa kuwachagulia watoto waume wa kuwaoa hata wao hawakuridhika. Yasmini hakuridhika kuchaguliwa mchumba. "Yasmini hakupenda hata kidogo kuolewa na mume kama yule kwani yeye mwenyewe angelipenda sana kupata mume kijana kama yeye mwenyewe" uk.1) Bashiri ami yake Bukheti anafuata utamaduni wa wazazi kuwachagulia watoto wake wa kuoa. Bukheti alikuwa amevutiwa na kumpenda yasmini hivyo aliamua kumchumbia na kumuoa awe mke wake Bukheti alipomwambia ami yake Bashiri kwamba amepata mchumba na anataka kumuoa, Bashiri alimkatalia nakumchagulia somoye ndiye awe mke wake. Kwa hiyo Bashiri na Bukheti walikuwa katika mgongano.Sikiliza majibu ya Bashiri kwa bukheti: “Ndugu yako somoye yupo hapa kama mke kweli tutakuoza Somoye. Wacha mambo ya kwenda kutafuta maponjoro.." (uk.254) Maelezo hayo yanaonyesha utamaduni uliojengeka wa wazazi kuwachagulia wachumba watoto wao. Matar anapingana na mawazo ya Bashiri na Gulam, mjomba wake Yasmini, yeye wasichaguliwe wachumba. Tazama maneno ya matar; “huyu ami yako mpuuzi, hayajui mambo leo Bashiri.Hajui kama siku hizi vijana wanatafutana wenyewe.Kijana anatafuta wake. N'do mnamwitaje vile siku hizi,gali frendi sijui (uk. 259) Maelezo hayo ya Matar yanaonyesha kuwa utamaduni wa wazazi kuwachagulia watoto wao wake wa kuoa au waume wa kuwaoa umepitwa na wakati, hivyo wazazi wawape uhuru vijana wao bukheti hakukubaliana na wazo la ami yake na akamchumbia yasmini na kumuoa. Ubaguzi wa Rangi katika jamii Ubaguzi wa rangi ni dhamira iliyoshughulikiwa na mwandishi Kutokana na tofauti za kiutamaduni na rangi za watu ndani ya jamii wanaweza kubaguana. Jamii ya Wahindi na jamii ya waafrika wana mtuzamo wa kubaguana. Kwa mfano, Bashiri alitaka kumzuia Bukheti asimuoe Yasmini kwa kuwa Yasmini ni mhindi (mwenye asili ya Kihindi) ila amuoe Somoye ambaye ni ndugu yake na Mwafrika mwenzake. Tazama maelezo ya Bashiri: "Ya nini kwenda kutafuta Wahindi mwanangu. Wewe una jamaa zako chungu nzima, kuukeni na kuumeni. Badala ya kumchukua jamaa yako ukamsitiri wewe unakwenda kutafuta Wahindi" (uk. 254). Maelezo hayo yanaonyesha ubaguzi, Bashiri anambagua yasmini kwa kuwa Yasmini ana asili ya Kihindi na Bashiri na nduguye ni Waafrika. Mama yake Yasmini anaonesha ubaguzi wa rangi a kumshutumu Yasmini kuwa anaishi na kushirikiana na aafrika. Kwa Mama Yasmini, mwanae kuishi na Waafrika ni kosa ni aibu kwa jamii ya Kihindi. Maneno ya mama Yasmini kwa mwanae: "Umekujisha kufenza nini hapa wewe mwanaharamuUmeacha Raza Mombasa umekujisha Zanzibar kufunzauhuni kutilisha sisi aibu, jamatini vatu ote nazungumza habari yako,nasema veve siku hizi nafuatana na golo. Toka toka kwenda zako..."(uk. 43). Maelezo hayo yanaonesha ubaguzi wa rangi waliyokuwa nayo jamii ya Kihindi dhidi ya jamii ya Kiafrika. Mama Yasmini na Jamatini wanamuona Yasmini amefanya jambo la aibu kabisa la kufuatana na "golo" yaani Waafrika. Huu ni ubaguzi. Suluhisho la tatizo hili mwandishi ameonyesha jamii inatakiwa iishi bila kubaguana kama alivyoonyesha kwa Yasmini muhindi kuishi na Mwajuma na kuwa na uhusiano na Denge pia aliolewa na Bukheti ambao wote hao ni Waafrika na hakuna tatizo lolote lililotokea. Pia Mzee Gulam, mjomba wake Yasmini alioa mke wa Kiafrika na hakukua na ubaya wowote. Utii kwa Wazazi katika jamii Jambo la kuwatii na kuheshimu wazazi limeshughulikiwa na mwandishi . Mwandishi anawataka watoto wawe na utii kwa wazazi wao wasionyeshe dharau kwa wazazi, hata kama kutotokosea mzazi, kafanya kosa basi mtoto anatakiwa awe mvumilivu na asionyeshe aina yoyote ile ya dharau mbele ya wazazi. Yasmini ni binti aliyeonyesha utii naheshima kwa wazazi wake, hakupinga mbele ya wazazi kuolewa na Mzee Raza mume aliyechaguliwa nao Yasmini anaonyesha hakumpenda wala hakumridhia mzee Raza kuwa mumewe bali hakutaka kuwaudhi wazazi wake. Tazama maneno haya: “kukubali kwake kuolewa ilikuwa ni kwa sababu ya kuwaridhi wazazi wake tu. Yeye mwenyewe hakuona fahari yoyote kuolewa na mzee anayeweza kumzaa. "(uk.1) “ah Yule alikuwa si mume wa kumtaka Mimi mwenyewe, niliozeshwa tu na wazee na mimi sikuweza kuwavunja…”(uk.23) Maelezo hayo yanaonyesha jinsi Yasmini alivyokuwa na heshima kwa wazazi wake. Hakutaka kubishana na kuonyesha utovu wa nidhamu mbele ya wazazi. Hivyo, mwandishi kupitia yasmini anasisitizavijana kuwa na heshima kwa wazazi na watu wazima Kukosa adabu mbele ya wazazi kunasababisha na mmomonyoko wa maadili ambapo inaweza kuzalisha viongozi wasio na adabu na utii kwa wanaowaongoza. Msomaji anaweza kufanya utafitina kupata dhamira nyingine kama vile umasikini na hali ngumu ya maisha na nyinginezo. MIGOGORO KATIKA VUTA N'KUVUTE. Migogoro lmeonyeshwa mingi ndani ya riwaya hii, na hapo tutaeleza kwa ufupi migogoro michache tu: kwanza, ni mgogoro kati ya Denge na serikali ya kikoloni chini ya idara ya polisi iliyokuwa ikiongozwa na Inspekta Wright. Denge pamoja na wenzake walikuwa wanapinga serikali ya kikoloni iliyokuwa chini ya Mwingereza katika visiwa vya Zanzibar yaani unguja na Pemba. Kwa mfano; mwandishi anadhihirisha mgogoro huu anaposema:- Denge alikuwa ametulia kimya, ananisikiliza kwa makini kabisa kabisa. "Yasimini mimi najua kuwa unanipenda, na mimi nakupenda vile vile, lakini kuna kitu kimoja napenda uelewa, kuna mapenzi na wajibu wa mtu katika jamii. Kila mtu ana wajibu fulani katika jamii na mimi wajibu wangu mkubwa ni kufanya kila niwezalo kwa kushirkiana na wenzangu ambao wengine unawajua na wengine huwajui kuona nchi hii inakuwa huru. Hii ni kazi ngumu Ina matatizo mengi na inahitaji kujitolea muhanga kufa, kupona potelea mbali" uk 145. Pili, mgogoro kati ya Yasimini na wazazi wake (mjomba mama yake). Mgogoro huu ni wa kijamii ambapo wazazi wake yasmini walimlazimisha kuolewa na mzee Raza mwenye umri wa miaka 52. Yasmini alikubali kuolewa kwa sababu ya kulazimishwa na mwandishi anavyoeleza:- "Ah, yule alikuwa si mume wa kumtaka mimi mwenyewe niliozeshwa tu na wazee wangu na mimi sikuweza kuwa vunja" alisema Yasimini uk 23 Tatu, mgogoro kati ya Yasimini na mzee Raza. Huu, pia ni mgogoro wa kijamii juu ya ndoa ya Yasimini na mume wake mzee raza kwa sababu Yasimini hakumpenda mume wake. Kwa hiyo ndoa hiyo ilikuwa katika mvutano na hatimaye ilivunjika. Kwa mfano mwandishi anasema:- usinikere bwana mimi nataka kulala" mbona unalala mapema? Ndo kwanza sasa mbili Amka tungumze" bwana Raza aliunguruma Yasmini alimpuuzana kulala uk 3. Nne mgogoro kati ya Mwajuma na Yasimini. Mgogoro huu ulitokea pale Mwajuma alipokuwa akimshawishi Yasimini achane na Denge na aolewe na Shihab kijana wa Tanga. kwa mfano mwandishi anaeleza; Na weye na Denge wako kila uambiwalo, Denge. Denge, unafikiri Denge kakupa nini? " Yeye mwenyewe hana mbele h ana nyuma, riziki inakuja hivi hivi unaipiga teke, na kama hukuolewa sasa unafikiri utaolewa lini? Mwajuma alimkaripia utafikiri mtoto mdogo. Uk 170 Tano, mgogoro kati ya Yasimini na Shihab mume wake wa pili baada ya Raza. Mgogoro huu ulitokea kwa sababu ndoa ya Shihabu na Yasmini ilitawaliwa na wivu wa kupindukia kiasi kwamba Yasmini hakufurahia maisha ya ndoa kama ilivyotegemea. Kwa mfano; mwandishi anaeleza:- “nisikonde! Mwanaume Yule ana wivu ana gubu, ana nongwa kama mwanamke” Yasmini alilalamika; nakwambia kaniweka ndani kama mwari sina jirani,sina jamaa, mimi na ndani na ndani na mimi siendi sirudi Uk 211. Sita ni Mgogoro kati ya Waafrika na Wahindi. Mgogoro huuvile vile ni wa kijamii kwa sababu Waafrika (waswahili) na wahindi wana mtazamo wa kubaguana kutokana na tofauti za kiutamaduni na rangi za watu ndani ya jamii inayoishi katika nchi moja. Kutokana na mgogoro huo wa kiubaguzi, wahindi wanawaita waswahili (wanfrika) GOLO na waswahili nao wanawaita wahindi MAPONJORO kwa mfano, juu ya wahindi mwandishi anasema; Umekujisha kufenza nini hapa wewe mwenaharamu, umeacha Raza Mombasa umekujisha Zanzibar kufenza uhuni kutilisha sisi aibu ote nzungumza habari yako, nasema veve siku hizi nafatana na golo uk. 43 Pia kwa upande wa Waswahili (Waafrika) mwandishi anasema:Badala ya kurnchukua jamaa yako ukamsitiri wewe unakwenda kutafuta wahindi" Bashiri aliweka kikombe cha kahawa barazaniameshangaa anamtazama Bukheti. Ndugu yako Somoye yupo ha pa. pia unataka mkwe kweli tutakuoza Somoye. Wacha mambo ya kwenda kutafuta Maponjoro. Unasemaje? uk. 254 Na saba ni mgogoro wa kinafsi waliokuwa nao Denge, Yasmini, Bukheti na Mwajuma. Kwa mfano, Yasmini ana mgogoro wa kinafsi kuhusiana na mambo kadhaa yanayomkabili. Yasmini ana mawazo kichwani kwake kuhusu mtafaruku aliokuwa nao wazazi wake, ana mawazo juu ya kifo cha mume wake Shihabu na amezongwa na majonzi ya kukamatwa mpenzi wake Denge,amezongwa na mapenzi ya dhati aliyokuwa nayo juu ya Denge naye sasa yuko mikononi mwa vyombo vya dola na mwisho amezongwa na hamu kubwa ya kumnusuru Denge. Huo ni mgogoro wa kinafsi aliokuwa nao Yasmini. Ujumbe Baada ya kusoma riwaya hii unaweza kutoka na mafunzo mengi, baadhi ya mafunzo hayo ni:
- Ushirikiano wenye upendo ambao umejikita katika misingi ya haki na usawa kwa kila mhusika ni jambo la msingi kabisa katika harakati za kuleta mabadiliko ndani ya jamii.
- Ndoa ya lazima mara nyingi haiwezi kudumu. Utamaduni wa wazazi kuwachagulia wachumba watoto wao umeshapitwa na wakati katika ulimwengu huu wa sayansi na teknolojia.
- Popote palipo na dhuluma na ukandamizaji mapambano nilazima yachukue nafasi ili kuondoa dhuluma hizo.
- Ndoa huweza kudumu kwa watu waliochaguana na kuridhiana.
- Penye nia daima pana njia
- Suala la mapenzi ya kweli halichagui rangi, kabila au mali. Falsafa Ya Mwandishi Mtazamo na msimamo wa mwandishi ni kuleta mabadiliko ndani ya jamii ambapo mabadiliko hayo yatafanikiwa kwa mapambano kama vile Denge alivyopambana, Yasmini alivyopambana na Bukheti alivyopambana.
MATUMIZI YA VIPENGELE VYA FANI KATIKA VUTA N’KUVUTE Shafi Adam Shafi katumia sanaa ya hali ya juu katika kuijenga kazi hii. Ndio maana riwaya hii ilipata tuzo wakati ba do ni mswada wa riwaya ya Kiswahili kabla hata haijachapishwa kwenye tamasha la vitabu la dar es salaam mwaka 1998. Kutokana na sanaa iliyotumika,inatia mvuto kwa msomaji anapoanza kukisoma asikiweke chini mpaka akimalize. Vipengele vya fani vitakavyo shughulikiwa ni: muundo, mtindo, wahusika mandhari na matumizi ya lugha.
- Muundo Muundo tunaangalia kwa kuona jinsi gani mwandishi alivyosuka visa na matukio na namna gani kazipanga sura katika kitabu chake. muundo uliotumika katika riwaya hii kwa upande wa mfululizo wa visa namatukio ni wa moja kwa moja. Mwandishi anaanza kusimulia kisa cha Yasmini binti mwenye umri wa miaka 15 kuozeshwa kwa mzee mwenye umri wa miaka 52 kwa jina Mzee Raza. Binti anaamua kumkimbia Mzee Raza, anarudi nyumbani kwa wazazi wake, wazazi wake wanamfukuza, anaamua kwenda kuishi kwa rafiki yake Mwajuma huko anakutana na kijana mwenzake Denge ambaye alikuwa akiongoza harakakati za kupambana na wakoloni wa Kiingereza na kupendana naye hatimaye wakaazaanaye mtoto. Denge kutukana na harakati zake alifungwa gerezeni yasmini akafunga ndoa na Shihab ambayo ilikuwa ndoa yake ya pili ndoa hii Ilitawaliwa na wivu wa kupindukia uliosababisha yasmini anyimwe uhuru na mumewe na kutokana na wivu shihab alifariki kwa kihoro. Mwisho Yasmini anafunga ndoa yake ya tatu kijana Mwafrika toka Mombasa na kuishi naye unguja kwa raha na starehe. kwa upande wa mpangilio wa sura, riwaya imejengwa kwa sura kumi na nnekuanzia sura ya kwanza hadi sura ya kumi na nane na katika sura ya kumi na nane (18) mwisho kabisa kuna kishilizio alichokiita tamati katika ukurasa wa 274.
- Mtindo Mwandishi ametumia mtindo wa masimulizi ambao utumiwa takriban na waandishi wengi wa kazi za fasihi ya kiswahili. Katika mtindo huu mwandishi ndiye anayejua na simulia hadhira visa na matukio yote, kama vile anavyotusimulia visa na matukio yote yaliyofanywa na Yasmini na wahusika wengine. Pamoja na mtindo huu wa masimulizi (Monolojia). Pia, mtindo wa barua ameutumia mwandishi pale Shihab alipomwandikia barua Yasmini ya kumueleza nia yake ya kutaka muoa (uk. 168). Barua nyingine ni ile iliyoandikwa na Yasmini kwenda kwa Denge iliyokuwa inaonyesha masikitiko aliyokuwa nayo Yasmini ya kuondoka Unguja na kumwacha Denge (uk.184).Vile vile mtindo wa dayalojia umetumika pale mwandishi powapa nafasi wahusika wenyewe wazungumze kwa Thizana. Kwa mfano mazungumzo kati ya Mwajuma na Yasmini, mazungumzo kati ya Yasmini na Koplo Matata, Mazungumzo kati Denge na Yasmini, mazungumzo kati ya Denge na Mambo, mazungumzo kati ya Denge na Inspekta Wright, Mazungumzo kati Bukheti na Bashiri, mazungumzo kati ya Yasmini na Kalmar na zungumzo mengine mengi. Mazungumzo hayo yaliyofanywa wahusika ili kutajirisha maudhui. Zaidi ni kwamba, kuna mtindo wa nyimbo. Mwandishi amemtumia Mwajuma; akifua huku akiimba:- Jamani ujana unanitoka, Mfano wa jua linapotoweka, Sasa wako wapi, walionitaka, Uzuri hakika, kitu cha kukopa Hakika ni kweli, nilibahashika Kuringia kitu, kisichoenzika, Mithili ya ua, ukishalikata Uzuri hakika kitu cha kukopa. (uk. 85 - 86)
- wahusika
Mwandish amewatumia wahusika wengi kupaza sana yake hapo tutawadondoa wahusika wachache muhimu.
- Yasmini Binti wa kihindi kutoka jamii ya lthnashiria, aliyeku na umri wa miaka kumi na tano (15) wakati alipoolewa na Mzee raza alichaguliwa mume na wazazi wake aliyekuwa mzee mwenye umri wa miaka 52 na kuolewa naye. Alionyesha utii kwa wazizi wake kama binti mwenye maadili, heshima na adabu. Hakuridhika kuishi katika ndoa yake ya lazima, ambapo aliamua kuondoka kwa mzee raza na kuishikwa Mwajuma. Anaonyesha mapenzi ya dhati kwa Denge. Anapinga mila na utamaduni wa kuchaguliwa mume. Anapinga mila na utamaduni na ubaguzi wa rangi ndio maana aliamua kuishi kwa Mwajuma ambapo ni mwafrika, pia alikuwa na mapenzi ya dhati kwa Denge ambaye ni mwafrika na pia aliolewa na Bukheti ambaye alikuwa Mwafrika ni mwanamapinduzi ambaye alishirikiana na akina Denge kupambana katika harakati za kupambana na wakoloni wa Kiingereza huko Unguja ni mvumilivu na asiyekata tamaa. Ni mhusika mviringo ambaye alimsaliti mume wake Shibab na kwenda kwa Denge mpenzi wakati alifunga ndoa na wanaume watatu kwa nyakati tofauti
- Denge kijana aliyeishi maisha ya ukapera. Alipata elimu ya juu katika nchi ya Urusi (nchi ya Kikomunisti). Pamoja na elimu yake ya juu aliyokuwa nayo alikosa ajira katika serikali ya kikoloni kutokana na chuki, Alikuwa mpenzi wa Yasmini hadi wakazaa mtoto Denge ni kijana shupavu ambaye aliongoza harakati na mapambano dhidi ya serikali ya kikoloni. Alifungwa gerezani na kupata mateso makubwa kutokanana kuongoza harakati, za kudai uhuru kutoka kwa wakoloni wa Kiingereza. Ni mchapakakazi mvumilivu na hakuwa mtu wa kukata tamaa. Alijitolea muhanga kwa hali na nafasi yake kupambana na wakoloni wa Kiingereza.
- Mzee Raza Mzee mwenye umri wa miaka 52 ambaye aliamua kumuoa binti mdogo mwenye umri wa miaka 15 sawa na mjukuu wake. Alikuwa mfanyabiashara. Alihamishia biashara zake toka Unguja kwenda Mombasa. Alitawaliwa na mfumo dume kwa kumtumikisha mkewe Yasmini. Kutokana na umri aliokuwa nao, alikimbiwa na mke wake.
- Gulam Mjomba wake Yasmini. Anatoka katika jamii ya lthnashiria. Alishirikiana na wazazi wa Yasmini kumuoza binti yao kwa Mzee Raza. Alimfukuza Yasmini nyumbani kwake kwa karaha kwakuwa Yasinini aliondoka kwa mume wake (Raza) kutokana na kushindwa kuishi na mume asiyempenda. Anafuata utamaduni wa kikale wa wazazi kuwachagulia watoto wao waume.
- Mama Yasmini Mama wa Kihindi kutoka jamii ya Ithnashiria Mama mzazi wa Yasmini. Anashiriki kumuozesha binti yake kwa Mzee Raza. Alimfukuza binti yake (Yasmini) nyumbani kwake kwa kuwa ondoka kwa mumewe Mzee Raza, Mume ambaye hakumpenda tokana na kuwa halikuwa chaguo lake. Ni
- mbaguzi wa rangi - alimshutumu na kumlaumu mwanae (Yasmini) kwa nini anaishi a Waafrika. Hafai kuigwa na jamii.
- Matar Jina lake maarufu aliitwa Bwana Mashuguli. Alikuwa fanya biashara wa chupa tupu, pia alikuwa muuza genge Darajani. alifuatwa na Bukheti iii amsaidie kumshawishi Bashiri (baba yake dogo Buketi) amkubali kumuoa Yasmini na apeleke posa kwa Gulam ya kumuoa Yasmini. Alimkabili na kumweleza kweli. Anapingana na mawazo ya kale ya wazazi kuwachagulia achumba watoto wao. Anakubaliana kuwa vijana wapewe uhuru wa kuchagua wake wa kuwaoa au waume wa kuolewa nao.
- Koplo matata Mwafrika aliyekuwa anatumikia jeshi la polisi la kikolo anaunga mkono juhudi za wakoloni kuwakandamiza Waafrika wenzie anashirika kupanga njama za kumkamata Denge asiendeleze harakatiza kupambana na ukoloni. Ni msaliti wa kiafrika.
- Inspekta wright Ni mzungu kutoka Uingereza. Kiongozi wa ngazi za juu wa jeshi la kikoloni. Alikuwa jeuri, mkatili na muonezi ni hodari wa kupanga njama na kuwasingizia raia wasio na hatia ili wakamatwe na kutiwa nguvuni na jeshi la polisi. Alishirikiana kumwekea visingizio Denge kuwa kuchapisha vikarata vya uchochezi ili akamatwe na jeshi la polisi. Alishiriki kufuatilia harakati za akina denge hadi akamkata Denge na kupelekwa kufungwa gerezani Alitaka kumrubuni na kumshawishi Denge aachane na harakati za kudai uhuru kwa kumuahidi kumpatia cheo.
- Mwajuma mwanamke wa Kiafrika aliyeishi Unguja katika chumba chake bila mume Alikuwa rafiki kipenzi wa Yasmini. Alikuwa mwimbaji maarufu katika kikundi cha Cheusi Dawa. Alimpokea yasmini na kuish naye nyumbani kwake baada ya Yasmini kufukuzwa na wazazi wake kutokana na kuondoka kwa mume wake mzee raza. Anapenda starehe, hasa kunywa pombe na kucheza dansi Ana mapenzi ya dhati kwa Yasmini. Ni mvumilia na mwenye huruma. Alishiriki harakati za mapambano dhidi ya ukoloni , kwa kushirikiana na akina Denge na Mambo. Wahusika wengine walioshiriki ni Mambo, Chande, Sefu, Sikutua, Karma Hussein na wengine wengi ambao wametumika kutajirisha maudhui.
Mandhari Mandhari iliyo tumika kujenga riwaya hii ni mandhari inayopatikana ukanda wa juu wa afrika mashariki ambayo ni unguja Mombasa tanga na dare s salaam pia kumetajwa urusi mahali alikosomea Denge. Pamoja na miji hiyo, pia kuna mandhari ndogondogo ambazo zinaonyesha uhalisia wa maisha mwanadamu ya kila siku. Kuna mandhari ya chumba cha Denge, mandhari ya chumba cha Mwajuma, mandhari ya Darajani, mandhari ya gerezani, mandhari ya nyumba ya Matar, mandhari ya nyumbani kwa Inspekta Wright, mandhari ya Karimjee "club" mandhari ya English club, mandhari ya nyumbani kwa mzee Kiroboto, mandhari zote hizo kazitumia msanii katika kutajirisha maudhui yake. MATUMIZI YA LUGHA Lugha ndiyo zana inayotumika kujengea sanaa ya fasihi. wa upande wa lugha mwandishi ametumia utaalamu na ufundi wa hali ya juu kiasi ambacho kuna mvuto wa hali ya juu kwa msomaji. mwandishi anajua namna ya kuyateua maneno na yakaendana na husika wake aliowapa wayaseme yakiambatana na vitendo. Kwa ujumla kuna matumizi ya aina zote za lugha ndani riwaya hii. Kuna matumizi ya lugha sanifu, lugha isiyo sanifu, lugha ya mtaani, matone ya lahaja ya Kiunguja, lugha ya ucheshi, lugha kali (matusi) na matumizi ya tamathali za,semi, misemo na methali kadhaa, pia kuchanganya ndimi (amechanganya lugha). 'Lugha Sanifu LUGHA SANIFU Riwaya imetumia lugha sanifu ambayo inajulikana kwa watumiaji wote wa lugha ya Kiswahili. LUGHA ISIYO SANIFU Katika kurembesha na kuboresha kazi yake baadhi sehemu kuna matumizi ya lugha isiyo sanifu, yaani lugha inayokiuka kanuni za sarufi ya Kiswahili. Matumizi ya lugha isiyo sanifu wamepewa wahusika ambao si Waswahili asilia na wenye asili ya kigeni ili kutajirisha maudhui. Mfano tazama lugha yotumia mama yake na Yasmini. "Umekujisha kufenza nini papa wewe mwenaharamu, Umeacha Raza Mombasa umekujisha Zanzibar kufenza uhuni katilisha sisi aibu. Jamatini vatu ote na zungumza habari yako..." (uk.43) maelezo hayo yote yanaonesha upoteshaji wa Sarufi ya Kiswahili kwa hiyo ni lugha isiyo sanifu. Tazama mfano mwingine toka kwa inspekta wright ambaye ni mzungu “wewe iko hakika denge ndiyo naleta material hizi?” Eleza mimi progress ya investigation yako kwa denge(uk.76) inspecka wright anaongea Kiswahili kisicho sanifu. Msanii amefanya hivi ilikuleta msisimko na kutajirisha maudhui yake. Msomaji anaweza kufanya utafiti na kugundua mahali pengine ambapo lugha isiyo sanifu imetumika. LUGHA YA MTAANI. Kuna matumizi ya maneno ya mtaani mfano barobaro(uk.13) alikuwa kijana barorbaro mwenye umbo…………… “ tazama ulivyokongoroka umebaki fremu tu”(uk.32) “kijana mmoja aliyekuwa na “nishai” changachanga….”(uk.61) Ubela-ubela (uk.220) Wacha mambo ya kwenda kutafuta “maponoro”(uk.254) Mkweche wa kutupwa(uk.79) MATONE YA LAHAJA YA KIUNGUJA “chombo kikateremshwa pwani”(uk.225) Akamkalia dagi (uk.257) Amle,mbiza amle mboza?(uk.104) Mkoko n`do kwanza ulikuwa ukichanua maua(uk.85) Nabahashuka na wewe?(uk.170) Lugha kali Baadhi ya sehemu mwandishi katumia lugha kali isiyo na kificho Mfano: tazama maelezo haya: "Alikuwa mtoto mrefu mwembamba mwenye nywele ndefu nyeusi ambazo alizitimua zikateremka mpaka matakoni..." (uk. 135). Neno, 'matakoni' ni lugha kali, ilihitaji kutumika tafsida lugha kali Nyingine mwenye laana weye kahaba mkubwa" (uk. 170). MATUMIZI YA TAMATHALI ZA SEMI Shafi Adamu Shafi ametumia tamathali za semi mbalimbali katika riwaya yake ya Vuta n'kuvute iii kutajirisha maudhui yake kwa jamii husika. Kutokana na wingi wa tamathali za semi zilizotumika, sisi tunabainisha ni wajibu wa walimu na wanafunzi kubainisha tamathali nyingine za semi kama vile tashihisi,takriri, tabaini, mubalagha na kejeli Tashbiha ni mfananisho wa vitu viwili au zaidi. Mara nyingi tamathali hii hutambuliwa kutokana na matumizi ya maneno kama mwandishi wa vuta n'kuvute ametumia tashibiha mbalimbali. baadhi ya tashbiha zilizotumika katika riwaya ya vuta n'kuvute Jumamosi ikapeperuka kama kishada kilicho katika orjojo (uk14 ), Yasimini amechachamaa, amekuja juu kama moto wa kifuu (uk.15), Nimekwenda kwa mjomba, nimetimuliwa kama mbuzi. 19), Walibaki chumbani mle kimya kama mabubu (uk 25), salumu mbele Roger nyuma anafuata tu kama mkia (uk. 27), Pale pembeni amesimama kama mlingoti (uk 37), na watu wa nchi hiyo wafupi kama Athumani Kafupi (uk 53) Pia mwandishi ametumia tashbiha zifuatazo;- Yasimini alichana nywele zake vizuri akazizongazonga na kuzifungia juu akawa kama sega la nyuki (uk 61), Jua liliwaka likawa kama moto 66), Alikuwa bado amekamatana kama aliyepakwa ulimbo (uk.75), Moyo wake ulikuwa kama uliotiwa kitanzi (uk 96). Kwa mbali mwanga wa taa za jiji la Dar es salaam ulianza onekana kama jua la alfajiri linapoibuka kutoka baharini (uk 4), lnspekta Wright alikuwa mkali kama moto (uk 151) na alinong'ona peke yake kama mwendawazimu (uk 159). Vile vile msanii ametumia tashibiha kama vile, komamanga ilikuwa inaelea, mpera kama bua (uk 272), Alizichana nywele zake zikawa kama mawimbi madogo madogo (uk 164), Alikuwa kama mwizi na wasi wasi ukamjaa, akahisi kama watu wote wanamshangilia yeye (uk 270), Alikurupuka kutoka ofisini kwake kama mtu aliyepandwa na pepo (uk 189),Wafungwa walitimka kutoka vyumbani mwao kama mbuzi waliofunguliwa kutoka zizini (uk. 263) walikuwa wanatazama tu kama majogoo walio kwenye Mapigano (uk 190), na ananukia kama jini (uk 249) Zaidi ni kwamba mtunzi wa vuta n'kuvute ametumia tashibiha kama vile wafungwa wakawazongea kama inzi wanapouzonga mzoga (uk 195), Kwa ghafla ikaibuka kwa mbali kutoka mawinguni kidogo kama mwewe aliyechanua mbawa zake (uk.215)Maruirui tu yaliyozagaa mbele yake kama umande uliotanda (uk. 210)Unaendesha baiskeli kama mwendawazimu (uk.229) ukabaki kukoroma kama aliyekata roho (uk, 234) METHALI pia msanii ametumia methali nyingi, miongoni mwake ni
- Mwisho wa dhiki ni faraja (uk. 43)
- umdhaniaye ndiye kumbe siye (uk.59)
- Wagombanao hupatana (uk. 172)
- Maji ukiyavulia nguo, sasa lazima ayakoge (uk. 193)
- Kelele za mpangaji hazimkeri mwenye nyumba (uk.229) Methali hizo na nyingine nyingi zimetumika kupamba kazi na kutajirisha maudhui
KUCHANGANYA NDIMI/KUCHANGANYA LUGHA Mwandishi kachanganya lugha katika kazi hii. Baadhi. ya sehemu katumia lugha ya Kiingereza kutokana na mhusika wake aliyempa kutumia lugha hiyo ili kutajirisha maudhui. Pia mahali ametumia lugha ya Kiarabu. Mfano Matumizi ya lugha ya Kiarabu: Yasmini na Mwajuma walipokuwa wanazungumza kuhusiana na askari kumtafuta Denge.Mwajuma alitumia maneno ya Kiarabu " Allahu yaall (uk.66) ikiwa na maana Mungu ndiye anayejua kisa cha askari kumtafuta mtu huyo. Mahali pengine palipotumika lugha ya kiarabu "alhamdu lillahi rabbi-el - alamin" (uk. 81) "La tamsak, mall n-nas" (uk. 212) Pia lugha ya Kiingereza imetumika, kwa kuwa baadhi ya wahusika ni Wazungu wa Kiingereza ambao walikuwa wanatawala zanzibar. Tazama mazungumzo kati ya kamishna wa polisi inspekta Wright. "Well" Alisema Kamishna na kuvunja kimya kilichokuwa ofisini mle "The Situation is very grave!" "Indeed Sir!, alijibu inspekta Wright. "We must inform the British Resident" We must Sir" (uk. 190) Pia mazungumzo ya inspekta Wright na Koplo Matata. inspekta Wright anasema: "Right now sit down" The communies, we shall give them hell, inspekta Wright alisema (uk. 76) Matumizi haya ya lugha ya Kiingereza yametumika kana na wahusika walivyojengwa na kutaka kufikisha dhui yaliyokusudiwa, mfano jeuri na dharau waliyokuwa o wakoloni wa Kizungu dhidi ya Waafrika. JINA LA KITABU Jina la kitabu, Vuta n'Kuvute linasadifu na yale ambayo yameshughulikiwa na kusimuliwa ndani ya riwaya hii. Visa na matukio yaliyomo yanaonesha Vuta n'kuvute. Kua Vuta n'kuvute kisiasa baina ya wakoloni na wananchi, kuna Vuta n'kuvute mapenzi na ndoa, vuta n'kuvute za vijana (watoto) na wazazi nyinginezo nyingi. Kwa ujumla riwaya hii ina vuta n'kuvute za kisiasa, vuta n'kuvute za kijamii na vuta n'kuvute za kiutamaduni kama zilivyojadiliwa katika kipengele cha maudhui ya kitabu hiki. KUFAULU KWA MWANDISHI Mwandishi amefaulu kwa kiwango cha hali ya juu katika kuijenga kazi yake kifani na kimaudhui. KIMAUDHUI Mwandishi amefaulu kufikisha ujumbe katika jamii dhamira yake kuu ya mapambano ili kuleta ukombozi. Wapambanaji wake wote wamefaulu . yasmini amefaulu mapambamo dhidi ya ubaguzi wa rangi ambapo ameweza kuishi na Waafrika wakati yeye ana asili ya kihindi pia kaolewa na Mwafrika ambaye ni Bukheti; pia Gulum mwenye asili ya kihindi ameoa Mwafrika na alimkubalia mpwawe yasmin aolewe na bukheti ambaye ni Mwafrika. Yasmini amefaulu mapambano ya ndoa za lazima baada ya kuondoka kwa Mzee Raza mumewe na kuolewa na mume asiyempenda. Denge amefaulu kwa kiasi fulani mapambano ya haraka dhidi ya ukoloni kwa kutikisa serikali ya kikoloni mpaka inspekta wright akataka urafiki na Denge na kutaka kumrubuni kumuahaidi cheo kikubwa. haya ni mafanikio katika harakati za mapambano. Mwandishi ametafuta katika kuijenga fani ya kazi ameteuwa na kuyapanga maneno vizuri, amewapanga wahusika wake vizuri na kuwapa maneno stahiki ya kusema na kutenda kulingana na uhusika wao. Kuwatumia baadhi ya wahusika na kuwapa lugha waliyoitumia isiyo sanifu ndiko kuliko ongeza mvuto katika kazi hii. Wahusika Wanazungumza kwakupangilia lugha ile waliyoitumia ni kuongeza ladha katika fani. kosa la kiufundi lilifanyika kwa upande wa fani ni kule kutumia lugha kali (matusi)badala ya kutumia tafsida. KUTOFAULU KWA MWANDISHI Kwa upande wa maudhui, mwandishi hakufaulu katika kumjenga Mhusika Yasmini kufanya usaliti katika ndoa.hakutakiwa kuchezewa. Kumfanya mhusika wake awe msaliti katika ndoa ni kufeli kwa mwandishi, kwani haikupata funzo zuri kutokana na kitendo hicho. MASWALI
- Miongoni mwa maudhui yanayoibushwa katika riwaya ni machungu ya wanawake dhidi ya kani kinzani na kasheshe wanazofanyiwa katika mikakati yao ya kutaka kujinasua. Toa maoni yako ukitumia riwaya ya Vuta n'kuvute.
- "Kuwepo kwa fasihi katika jamii ni tarajio la kimsingi; inapokosekana jamii hupata mapungufu katika ukamilifu wake...". Kwa kutumia riwaya ya Vuta n'kuvute kataa au kubali hoja hiyo.
- "Ukombozi si jambo rahisi". Hakiki kauli hiyo ukihusisha riwaya ya vuta n'kuvute. Toa hoja tano (5).
- Ujenzi mzuri wa fani husaidia uwasilishaji wa maudhui katika kazi ya fasihi. jadili usemi huu kwa hoja tano (5) madh'ubuti ukitumia Vuta n'kuvute.
- Muhusika mkuu ni kipaza sauti cha msanii wakati muhusika mdogo ni mjenzi wa muhusika mkuu" Fafanua kauli hii kwa hoja tano (5) ukitumia vuta n'kuvute.
Mwalimu
Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.
Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.
Ingia ili kuuliza