Risala
Ni taarifa fupi inayosomwa mbele ya kiongozi mgeni rasmi kwa niaba ya kundi fulani la watu ili kutoa maelezo au kuonesha msimamo wa kundi hilo kwa kiongozi. Ni aina ya taarifa ambayo hupelekwa kwa mtu au watu fulani inayoeleza haja inayotakiwa.
Muundo wa Risala
Risala imegawanyika katika sehemu tatu:
Mwanzo
Hapa panahusu sana salamu: ukaribisho na lengo la risala
Kati
Hapa ndipo kiini cha risala ambacho huonesha mafanikio, matatizo, mapendekezo n.k
Mwisho
Hueleza msisitizo au shukrani
Soma risala ifuatayo kisha jibu maswali
RISALA YA WANAFUNZI WA SHULE YA MSINGI FUKA KWA MGENI RASMI JUU YA SHUGHULI ZA UZALISHAJI MALI
Ndugu mgeni rasmi: wazazi, walimu na wanafunzi.
Tunayo furaha kubwa kukukaribisha katika shule ya msingi Fuka, ili uweze kuona na kusikia shughuli za uzalishaji mali.
Ndugu mgeni rasmi shule yetu ina wanafunzi mia tao (500), wavulana mia mbili na hamsini (250) na wasichana mia mbili na hamsini (250). Walimu ishirini pamoja na shughuli za kitaalamu, shughuli za uzalishaji mali pia zinatiliwa mkazo.
Ndugu mgeni rasmi shule yetu ina miradi mbalimbali ambayo ni shamba la migomba na mboga za majani. Shamba la Migomba na mboga za majani kwa kipindi cha mwaka mmoja ziliingiza faida ya shilingi laki tano elfu ishirini.
Ndugu mgeni rasmi pamoja na mafanikio hayo tuna matatizo kadhaa yanayohusu shughuli za uzalishaji mali. Tuna tatizo la pembejeo, bado tunatumia majambe ya mkono katika ulimaji. Hii husababisha wanafunzi watumie muda mrefu.
Ndugu mgeni rasmi tatizo jingine ni tatizo la maji. Kutokana na tatizo hili, shule imeshindwa kupanua shamba la mboga za majani na kukosesha shule mapato.
Ndugu mgeni rasmi tunaomba wizara yako itusaidie ili tuweze kupata mkopo na hatimae tuweze kununua zana za kilimo zilizobora kama trekta na plau. Vilevile itusaidie kufikisha ombi letu la maji kwa Wizara husika ili tuweze kupata maji.
Ndugu mgeni rasmi, tunatumaini utapeleka maombi yetu kunakohusika. Asante
Mwalimu
Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.
Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.
Ingia ili kuuliza