Sonzaschool
Rudi

Sekondari ya Kawaida · Kidato cha Pili

Kiswahili

Mofimu

takriban dakika 2 kusoma

Mada za sehemu hiiUundaji Wa ManenoMada 3

Uundaji wa maneno

  1. Uundaji wa maneno ni shughuli ya kuunganisha viambajengo (vipashio) mbalimbali ili kupata maneno tofauti yenye maana mbalimbali ambazo ni kamili.
  2. Maendeleo ya jamii hubadilika, hukua, na kuongezeka, hivyo lugha nayo hukua na kubadilika ili kukidhi haja ya mawasiliano.
  3. Ili msamiati uongezeke, maneno yaundwe kwa lengo la kuboresha mawasiliano kulingana na wakati uliopo.

Umuhimu wa uundaji wa maneno

  1. Kupata msamiati wa kutosha katika lugha husika ili kukidhi mabadiliko yanayojitokeza.
  2. Kukabiliana na suala la maendeleo ya sayansi na teknolojia katika ongezeko la maneno mapya.
  3. Ubunifu wa maneno hutokana na njia mbalimbali kama vile:
    1. Uambishaji wa maneno
    2. Kubadili mpangilio wa herufi
    3. Kutohoa maneno ya lugha nyingine
    4. Kuambatanisha maneno
    5. Kufananisha sauti, umbo, mlio.

Uundaji wa maneno kwa kutumia mofimu

Mofimu ni kipashio kidogo zaidi cha lugha chenye maana ya kisarufi au kileksika (msamiati). Hiki ni kipande cha neno ambacho hakiwezi kugawanyika zaidi bila kupoteza maana yake ya awali.

Mwalimu

Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.

Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.

Ingia ili kuuliza