Mada za sehemu hiiTungoMada 2
- Sentensi
- Kuchanganua Sentensi
Uchanganuzi wa Sentensi
Kuchanganua sentensi ni mbinu ya kuigawa sentensi katika sehemu mbalimbali ambazo huunda sentensi hiyo.
-
Kutaja aina ya sentensi yaani kama ni sentensi sahili, ambatano au changamano.
-
Taja sehemu zake kuu yaani; kiima na kiarifu (kishazi) au KN na KT (kimuundo)
-
Kama ni sentensi sahili onyesha vipashio vya kiima na kiarifu; yaani jina, vivumishi, vitenzi, shamirisho na chagizo n.k
Kama ni sentensi changamano taja vishazi vyake na kazi ya kila kishazi tegemezi katika hiyo sentensi changamano yaani taja: kama kishazi tegemezi kinavyovumisha jina au KN kilicho katika kiima au KN cha kishazi huru. Mfano; Mzee uliyemwona jana ni baba yangu.
"uliyemwona jana" ni kishazi tegemezi kivumishi kinachovumisha jina "mzee" lililo kiima cha kishazi huru (K/H) "mzee ni baba yangu"
-
Kutaja aina za maneno yote yaliyomo katika sentensi hiyo.
Mfano; Baba na mama wanakula ugali
N t N T N
-
Kuandika tena sentensi
Kuna njia kuu nne za uchanganuzi wa sentensi
- Matawi/ ngawe/ michoroti
- Jedwali/ visanduku
- Mishale/ mistari
- Sentensi/ maelezo/ maneno
Mfano;
Mwalimu mwema amemsaidia mwanafunzi
Mbuzi aliyenunuliwa juzi amechinjwa leo asubuh

Mfano;
Gari lililopinduka jina limeinuliwa na dereva wake amefariki dunia
S. ambatano
Wanafunzi waliimba wimbo wao vizuri sana

Mfano;
Shangazi anasoma kitabu polepole
Shangazi anasoma kitabu polepole
Mbwa aliyepata kichaa mwogope
Mbwa aliyepata kichaa mwogope
Juma anacheza mpira na Damasi anasoma kitabu
- Hii ni sentensi ambatano.
- Sentensi hii ina sentensi mbili na kiunganishi.
Sentensi ya kwanza ina kiima na kiarifu:
- Kiima kina jina.
- Jina ni Juma.
- Kiarifu kina kitenzi na nomino.
- Kitenzi ni anacheza.
- Nomino ni mpira.
- Kiunganishi ni na.
Sentensi ya pili ina kiima na kiarifu:
- Kiima kina jina.
- Jina ni Damasi.
- Kiarifu kina kitenzi na jina.
- Kitenzi ni anasoma.
- Jina ni kitabu.
Balozi wetu ni mtu jasiri sana
Hii ni sentensi sahili.
Sentensi ina kiima na kiarifu:
- Kiima kina jina na kivumishi.
- Jina ni balozi na kivumishi ni wetu.
- Kiarifu kinakitenzi kishirikishi + Kirai nomino.
- Kirai kielezi
- Kitenzi kishirikishi ni ni.
- Kirai nomino kina jina na kivumishi:
- Jina ni mtu na kivumishi ni sana.
Mwalimu
Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.
Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.
Ingia ili kuuliza