Mada za sehemu hiiKutathmini ukoloni kama nguvu laini (soft power) ya kujenga mwelekeo mpya wa jamiiMada 4
- Kueleza dhana ya ukoloni kama nguvu laini (soft power) na nguvu ngumu (hard power)
- Kueleza chimbuko la ukoloni na kuenea kwake Tanzania
- Kuchambua athari za ukoloni kisiasa, kiuchumi, kijamii, kiutamaduni na maadili
- Kujadili uzalendo na ujasiri wa Watanzania waliopinga mfumo wa ukoloni na maadili ya utamaduni
Ukoloni ni hali ya taifa moja kutoka nje ya mipaka yake na kutawala kwa mabavu taifa lingine katika nyanja zote, yaani uchumi, utamaduni, siasa na jamii. Katika kuitawala Tanzania, wakoloni walitumia mbinu mbili kuu: nguvu laini (soft power) na nguvu ngumu (hard power). Mbinu hizi mbili zilisaidia kujenga mweleweko mpya wa jamii ya Kitanzania wakati wa ukoloni.
Maana ya nguvu laini
Nguvu laini ni ule uwezo wa upande mmoja kutumia ushawishi na mbinu za kidiplomasia kutimiza malengo maalum dhidi ya upande wa pili. Nguvu laini haitumii mabavu, bali inatumia ushawishi wa kiutamaduni, miliko na maadili ya kisiasa kufanya mabadiliko. Pia, ni uwezo wa taifa moja kuishawishi na kuibadilisha tabia ya mataifa mengine ili kupata kile ambacho taifa hilo linakitafuta.
Mifano ya nguvu laini iliyotumiwa na wakoloni Tanzania
Mikataka ya Kilaghai
Moja ya nguvu laini iliyoitumiwa na watawala wa Kijerumani ilikuwa kusaini mikataka ya kilaghai na jamii za Kitanzania. Mkataba maarufu ulikuwa ule uliosainiwa kati ya Karl Peters na Chifu Mangungo wa Msovero, Usagara mwaka 1884 katika wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro.
Mkataba huu ulisomeka kwamba Chifu Mangungo alikubali kuikabidhi ardhi yake pamoja na watu wake kwa Wajerumani na wao kugeuzwa kuwa watawalwa. Karl Peters alifanikisha mkataba huu kwa kutumia lugha ngeni ambayo Chifu Mangungo alikuwa haifahamu. Pia, Mangungo hakufahamu kanuni za mikataka ya kimataifa. Ni kupitia mkataba huu ardhi ya watu wa Msovero na Ujerumani ya Afrika Mashariki ilikabidhiwa kwa utawala wa Wajerumani mwaka 1885.
Imani ya Dini
Dini ilitumika kama nguvu laini ya kueneza ukoloni katika jamii za Kitanzania kupitia wamisionari kwa kukuza maadili ya utamaduni wa Magharibi na imani ya dini ya Kikristo. Wamisionari walitumia dini ya Kikristo kuzianzisha jamii za Kitanzania kuwa waumini wazuri wa Ukristo, dini mpya kutoka Ulaya. Ukristo uliwafundisha wanajamii wa Kitanzania kuwa wenye kevu kwa wageni na watu wote, pamoja na kuti na kuheshimu mamlaka za kanisa na serikali. Hali hii ilifanya uvamizi wa wakoloni kuwa rahisi na kukubalika haraka.
Elimu
Elimu ya kikoloni ilitumika kama nguvu laini katika kutawala jamii za Kitanzania. Elimu ilitumika katika kupandikiza utamaduni wa Magharibi, yaani utamaduni wa Kizungu, ambao uliathiri mtazamo, kujiamini, uzalendo na tabia za jamii za Kitanzania. Elimu ya kikoloni ilitumia mitaala ya kikoloni iliyoandaliwa ili kuwaandaa wanafunzi wa jamii za Kitanzania kurithi utamaduni wa Magharibi na kuachana na utamaduni wao.
Maana ya nguvu ngumu
Nguvu ngumu ni matumizi ya nguvu za kijeshi au mabavu au nguvu za kiuchumi kushawishi na kubadilisha tabia au mtazamo au maslahi ya nchi au jamii zingine. Mara nyingi mfumo huu unatumia mabavu na hufanikiwa pale unapotumiwa na upande wenye nguvu ya kiuchumi na kijeshi dhidi ya upande dhaifu.
Mifano ya nguvu ngumu iliyotumiwa na wakoloni Tanzania
Vita vya Pangani
Wakoloni wa Kijerumani walitumia nguvu kubwa dhidi ya watu wa Pangani wakiongozwa na Abushiri bin Salum na Bwana Heri aliyeongoza mapambano huko Saadani kati ya mwaka 1888 na 1889. Jamii za pwani zilisimama kidete pale watawala wa Kijerumani waliposimika bandera yao kuashiria kuanza kwa utawala wao mwaka 1888. Kwa kuwa Wajerumani walikuwa na silaha za kisasa, walifanikiwa kushinda vita hivi na kuchukua utawala wa ukanda wa pwani mwaka 1889. Wajerumani walimkamata Abushiri na kumnyonga baada kusalitiwa na Jumbe Magaya wa Usagara mwaka 1889.
Vita vya Wahehe
Wajerumani walitumia mabavu ili kuingiza utawala wao wa kikoloni huko Iringa. Jamii ya Wahche chini ya kiongozi wao jasiri Mtwa Mkwawa walipambana dhidi ya utawala dhulumu wa Kijerumani kuanzia mwaka 1891 hadi 1898. Mkwawa alipigana na jeshi la kikoloni ili kuilinda uhuru wa kisiasa na wa kiuchumi wa jamii yake. Wajerumani walishindwa katika mapigano hayo huko Lugalo mwaka 1891. Hata hivyo, Wajerumani walijipanga upya kwa kuishambulia na kuiteka ngome ya Mkwawa huko Kalenga mwaka 1894. Mkwawa hakukubali kuitambua serikali ya Wajerumani, hivyo aliendea vita ya msituni kuanzia mwaka 1894 hadi mwaka 1898 ambapo ardhi ya Wahehe iliangukia mikono mwa Wajerumani. Mkwawa hakukubali dhihaka na aibu ya kukamatwa hivyo, alijiuua kwa kujipiga risasi kichwani.
Vita vya Maji Maji
Katika maeneo ya Umatumbi huko Kilwa, jamii za Kitanzania pia zilishuhudia matumizi makubwa ya nguvu kutoka kwa wakoloni wa Kijerumani. Katika eneo hili, jamii za Umatumbi zilipingana kulazimishwa kwa nguvu kulima na kufanya kazi kwenda mashamba ya pamba yaliyoanzishwa na serikali ya kikoloni ya Kijerumani. Jamii hizi, chini ya kiongozi mahiri Kinjekitile Ngwale, walipigana dhidi ya Wajerumani katika vita vya Maji Maji kuanzia mwaka 1905 hadi 1907 wakipingana kulazimishwa kulima pamba, kulipa kodi na unyanyasaji katika mazingira ya kazi.
| Nguvu Laini | Nguvu Ngumu |
|---|---|
| Hutumia ushawishi na diplomasia | Hutumia nguvu za kijeshi na mabavu |
| Haifanyi vita | Hufanya vita |
| Hujenga uhusiano wa hiari | Hulitisha utii kwa nguvu |
| Mifano: mikataka, dini, elimu | Mifano: vita, mauaji, kukamata viongozi |
| Ni ya muda mrefu | Ni ya haraka |
Katika maisha ya kila siku Tanzania, tunaweza kuangalia mbinu za nguvu laini na ngumu zinavyotumika. Kwa mfano, katika biashara ndogo nchini, wafanyabiashara wanaweza kutumia nguvu laini kushawishi wateja kununua bidhaa zao kwa kutumia matangazo mema na huduma nzuri, badala ya kutumia nguvu ngumu kama kushawishi kwa lazima. Pia, serikali ya Tanzania inatumia nguvu laini kupitia Elimu ya Maadili na Kiswahili kuwashawishi wananchi kuzingatia sheria na kanuni za nchi, sawa na jinsi wakoloni walivyotumia elimu kama nguvu laini wakati wa ukoloni.
Swali
Nguvu laini (soft power) katika ukoloni ina maana gani?
Ingia ili kuwasilisha jibu lako na lihesabiwe katika umahiri wako.
Ingia ili kufanya mazoeziMwalimu
Umekwama? Niulize chochote kuhusu mada hii.
Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu swali hili.
Ingia ili kuuliza