Mada za sehemu hiiUandishi Wa BaruaMada 1
- Barua za kirafiki
Uandishi wa barua
Barua
Ni maandishi yenye ujumbe yanayopelekwa kwa mtu mwingine kwa njia mbalimbali. Mfano wa njia hizo ni:
- Posta
- Mkono
- Basi au ndege n.k
Kuna aina mbalimbali za barua kama vile:
- Barua za kirafiki
- Barua rasmi
- Barua za mialiko
- Barua za kindugu
Barua za kirafiki
Hizi ni barua ziandikwazo kwa marafiki, jamaa, ndugu, wazazi.
Lengo la barua za kirafiki
- Kusalimiana na ndugu zetu
- Kuomba msaada
- Kutoa pongezi, hongera au pole
- Kuomba msamaha
Muundo wa barua za kirafiki
Barua za kirafiki huundwa na mambo muhimu yafuatayo:
- Anuani ya mwandishi
- Tarehe
- Mwanzo wa barua
- Mwisho wa barua
- Jina la mwandishi
Anuani ya mwandishi
Huandikwa juu kwenye pembe ya kulia ya karatasi. Huandikwa kwa waziwazi na kwa usahihi ili mwandikiwa aitumie kujibu barua aliyotumiwa. Huweza kuandikwa kwa muundo wa mshazari au wima.
Mfano wa mshazari
SHULE YA SEKONDARI MAKONGO S. L.P 60157 DAR ES SALAAM 19/07/2012
Mfano wa wima
SHULE YA SEKONDARI MAKONGO S. L.P 60157 DAR ES SALAAM 19/07/2012
Tarehe
Huandikwa chini kwenye anuani ya mwandishi ili kumjulisha mwandikiwa lini barua imeandikwa. Tarehe huweza kuandikwa kwa miundo mbalimbali mfano: 2-02-2012, 02/02/2012, 2.2.2012 au february.
Mwanzo wa barua
Huandikwa kushoto chini ya mstari wa tarehe. Huweza kuandikwa kwa kutajwa jina, eneo au wadhifa wa mtu anayeandikiwa.
Mfano: Mpendwa Baba, mama, kaka, mpenzi wangu. Pia sehemu hii kukaa maneno ya sehemu maamkizi ili kujulikana kati ya mwandishi na mwandikiwa.
Kiini cha barua
Sehemu hii hueleza kusudi au lengo la mwandishi, huelezea kusudi lake la kuandika barua.
Mfano:
- Kuomba kazi
- Kuomba msaada
- Kuomba msamaha
- Kujuliana hali
Mwisho wa barua
Hapa huwa na salamu za maagano na salamu hizo hutegemea mwandishi na mwandikiwa. Mwisho wa barua huwa na maneno yenye ladha na mvuto.
Mfano: Wasalamu au nisalimie wote wanaonifahamu na kusubiri kwa hamu n.k.
Jina la mwandishi
Ni muhimu mwandishi kuandika jina ili kumjulisha mwandikiwa barua imetoka kwa nani.
Angalizo: Uandishi wa barua za kirafiki hufuata taratibu zote za uandishi.
Mfano:
- Mkato
- Nukta
- Alama za kuuliza
- Mshangao n.k
Kielelezo cha muundo wa barua za kirafiki
SHULE YA SEKONDARI MAKONGO S. L.P 60157 DAR ES SALAAM 19/07/2012
Baba mpendwa;
Salamu sana, je! Hamjambo wote hapo nyumbani? Wale mbuzi wangu mapacha niliowaacha wamezaa tena? Natumaini wadogo zangu kulwa na doto wanaendelea vema na masomo.
Dhima la barua hii ni kutaka kukujulisha maendeleo yangu ya shuleni ya kidato cha kwanza. Pia tatizo kubwa linaloniandama hapa shuleni ni umaskini, sina hata shilingi moja ya kununua hata kipande cha mboga. Hivyo naomba nitumie hela ya matumizi ili nisome vizuri.
Wasalimie wote hapo nyumbani pamoja na marafiki zangu wote.
Wako akupendaye ELIMUKAZI
Mwalimu
Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.
Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.
Ingia ili kuuliza