Sonzaschool
Rudi

Sekondari ya Kawaida · Kidato cha Kwanza

Kiswahili

Insha za wasifu

takriban dakika 5 kusoma

Mada za sehemu hiiUandishi Wa InshaMada 1
  1. Insha za wasifu

Taratibu za Uandishi

Alama na mpangilio wa maneno ni mojawapo ya vigezo vya kutambulisha mwandishi bora hodari kaziiwezekuwa nzuri inayoeleweka na wasomaji, mwandishi hana budi kutumia mfumo wa alama ili kumsaidia msomaji wapi pa kumpumzisha, kuuliza swali n.k baadhiya alama zifuatazo hutumika katika uandishi.

Mkato (,)

Alama hii hutumika:

  1. kuweka pumziko fupi katika sentensi
  2. kutenga maneno yaliyo katika orodha
  3. huonyesha sehemu mbili za sentensi zilizo kinyume

Mfano: Umoja ni nguvu, utengano ni dhaifu

Nukta (.)

Alama hii hutumika:

  1. kukamilisha sentensi
  2. kuonyesha ufupisho wa maneno

Mfano: R.T.D (Radio Tanzania Dar es Salaam)

Nukta Mkato (;)

Alama hii hutumika Kuunga sentensi mbili zinazoweza kusimama zenyewe bila kutumia kiunganishi.

Mfano: Hapo zamani za kale wazee walijiheshimi; sikuhizi hawajiheshimu. Humpa msomaji pumziko fupi katika sentensi.

Nukta/Pukta Pacha (:)

Alama hii hutumika kuunga sentensi mbili zinazoweza kusema zenyewe, bila kutumia kiunganishi

  • kuunga/kuonesha vitu vilivyo katika orodha

Mfano: Nilileta vitu hivi: wino, karatasi, embe, ndizi na nanasi.

Alama ya Mshangao (!)

  1. Hutumika baada ya neno au usemi wa kushangaza au kushtuka
  2. Hutumika kuonesha msisitizo, kushangaa, kero n.k.

Mfano: Hivi ni kweli! Mwone alivyo.

Alama ya Kuuliza (?)

Huonesha hali ya kuuliza swali katika tungo/sentensi

Mfano:

  1. Wanakuja saa ngapi?
  2. Wanamaana gani?

Mabano [ ( ) ]

Hutumika kuonesha maana ya ziada katika sentensi

Mfano: Nchi yangu (Tanzania) naipenda sana

Kistari (-)

Hutumika kuunda maneno

Mfano: Ed-elfitr, Dar-es-salaam

Hutumika badala ya nukta mbili

Mfano: tulipofika mbugani – tuliwaona swala wamelala – Swala dume na watoto watatu.

  • Hutumika kuonesha kama neno limekatwa kwa kuwa limefika ukingoni.

Alama za Mtajo (" ")

Hutumika kuonesha maneno yaliyosemwa na mtu mwingine katika sentensi.

Mfano: Nguchiro alisema "hakika mzee Ngwale ni katili sana"

Hutumika kubainisha maneno ya kigeni katika lugha nyingine.

Mfano: ("yes") katika Kiswahili.

Mwalimu

Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.

Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.

Ingia ili kuuliza