Mada za sehemu hiiMaendeleo Ya Fasihi SimuliziMada 4
- Uwasilishaji na uenezaji wa kazi za fasihi simulizi
- Uhifadhi wa kazi za fasihi simulizi
- Kuhakiki kazi za fasihi simulizi
- Kutunga kazi za fasihi simulizi
Fasihi simulizi
- Fasihi simulizi ni sanaa ambayo hutumia mazungumzo na matendo katika kuwasilisha ujumbe Fulani kwa watazamaji au wasikilizaji.
- Mazungumzo hayo huweza kuwa ya kuimbwa, kutendwa au kuzungumzwa.
- Aina hii ya fasihi imepokelewa kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa njia ya mdomo.
Uwasilishaji wa Fasihi Simulizi
-
Msimulizi katika fasihi simulizi mbali na kutumia mdomo wake hutumia viungo vyake vya mwili kama:
- Mikono
- Miguu
- Ishara mbalimbali katika uso wake
- Kupandisha na kushusha sauti yake
-
Kwa ujumla anaweza kutumia mwili wake mzima katika kuwasilisha na kufanikisha ujumbe wake kwa hadhira yake ambayo huwa ana kwa ana.
-
Isitoshe, anafaulu katika kutoa picha halisi ya dhana anayotaka kuiwasilisha kama ni ya:
- Huzuni
- Furaha
- Kuchekesha n.k.
Ushirikishaji wa hadhira
-
Zaidi ya kusimulia, kuimba na kuigiza, msanii wa fasihi simulizi huwa na nafasi ya kushirikisha hadhira yake kama wahusika katika sanaa yake.
-
Anaweza kutimiza hayo kwa:
- Kumfanya mshiriki mmoja kuigiza jambo fulani
- Kufanya hadhira yote kuimba au kufanya matendo mbalimbali
-
Ufundi wa aina hii huhitaji umahiri wa hali ya juu.
-
Hali hii humpa msanii wahakiki wake hapohapo.
Majukumu ya Fasihi Simulizi
-
Fasihi simulizi hueleza jamii:
- Kiutamaduni
- Kiuchumi
- Kisiasa
-
Fasihi huzungumzia mambo ambayo huzunguka jamii husika.
-
Fasihi simulizi huathiri malezi ya watu kutoka kizazi kimoja hadi kingine kwa njia ya mdomo na matendo.
Uh
ai na mabadiliko
-
Fasihi simulizi huenda sambamba na mabadiliko ya jamii na kwa hivyo nayo hubadilika:
- Kimaudhui
- Kifani
- Kufuatia mabadiliko ya mifumo ya kisiasa, kijamii na kiuchumi
-
Fasihi simulizi ni utanzu wa kisanaa ulio hai na ambao hukua na kubadilika kutokana na mabadiliko ya wakati na ya mifumo ya jamii.
Hivyo fasihi simulizi ni tukio linafungamana na muktadha (mazingira) fulani ya jamii kutawaliwa na mwingiliano wa mambo yafuatayo:
- MSIMULIZI (FANANI) Huyu ni mtu ambaye anaitamba hadithi, kuimba wimbo kutoa methali au vitendawili.
- WASIKILIZAJI AU WATAZAMAJI (HADHIRA) Hawa huwa ni washiriki katika kutazama au kusikiliza fani za fasihi simulizi na mara nyingine huwa wanatumiwa na fanani kama wahusika wa fani yake.
- MAHALI (MANDHARI) Hapa ni jukwaa au mahali ambapo tukio la fasihi simulizi linatendeka mahali hapo panaweza kuwa nyumbani, uwanjani n.k.
- TUKIO Ni shughuli ya kijamii ambayo ndiyo muktadha wa utendaji huo wa sanaa mathalani harusi, kazi Fulani, sherehe, msiba, ibada n.k. utendaji huo waweza kuwa katika usimulizi wa hadithi, kutega vitendawili kuimba wimbo/nyimbo au kutoa methali.
- WAKATI Ni muda maalumu wa kihistoria au majira maalum ya utendaji huo.
Mwalimu
Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.
Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.
Ingia ili kuuliza