Sonzaschool
Rudi

Sekondari ya Kawaida · Kidato cha Kwanza

Kiswahili

Ufafanuzi wa aina za maneno

takriban dakika 3 kusoma

Mada za sehemu hiiLugha Na MawasilianoMada 5

NOMINO

  1. Nomino ni maneno yanayotaja majina ya watu, wanyama, mahali, vitu n.k.

  2. Tabia zake kimuundo:

    • Huchukua viambishi.
    • Huonyesha ngeli na idadi.
    • Hutawala kirai nomino.
  3. Mifano: jua, Seif, Morogoro.

Aina za Nomino

  1. Nomino za pekee – Huchukua herufi kubwa. Mfano: Nyerere, Ali, Singida, Nile.
  2. Nomino za kawaida – Zinataja vitu vyenye tabia za kifaradhi. Mfano: mtoto, mtu, nyumba.
  3. Nomino za jumla – Zinataja kundi la vitu. Mfano: jeshi, jamii, kundi.
  4. Nomino dhahania – Zinataja vitu visivyoonekana. Mfano: njaa, furaha, upepo.

VIWAKILISHI

  1. Huchukua nafasi ya nomino.
  2. Hubeba tabia za kinomino: kutawala kirai na kuchukua viambishi ngeli.
  3. Mifano: wewe, sisi.

Aina za Viwakilishi

  1. Viwakilishi nafsi

    • Nafsi huru

      • Umoja: Mimi (I), Wewe (II), Yeye (III)
      • Wingi: Sisi (I), Ninyi (II), Wao (III)
    • Nafsi viambata (huchangamana na vitenzi)

      • Mfano: Ninakuja, Tunakuja, Unakuja
  2. Viwakilishi vya kumiliki – angu, ako, enu, ake

  3. Viwakilishi vya kuuliza – kipi, gani, epi

  4. Viwakilishi vya kuonesha – huyu, hawa, kile

  5. Viwakilishi vya msisitizo – ndiye, ndiwe, ambaye

VIVUMISHI

  1. Huambatana na nomino/viwakilishi kutoa taarifa zake.
  2. Huchukua viambishi ngeli.
  3. Hutawala kirai vumishi.

Aina za Vivumishi

  1. Vivumishi vya sifa – zuri, hodari, mkubwa
  2. Vivumishi vya kuuliza – yupi?, gani?
  3. Vivumishi vya kumiliki – changu, yetu, yako
  4. Vivumishi vya kuonesha – hii, wale
  5. Vivumishi vya idadi – wawili, wengi, kidogo
  6. Vivumishi vya jina kwa jina – Mwalimu Zakia, Baba Juma
  7. Vivumishi vya -a- unganifu – nyumba ya baba
  8. Vivumishi vya -enye-, -enyewe- – mtoto mwenye, nyumba yenyewe
  9. Vivumishi vya o-te- – nyumba yoyote
  10. Vivumishi vya –ingine/-engine – kiti kingine, watu wengine

VITENZI

  1. Hueleza tendo au hali ya nomino.
  2. Huunda kirai tenzi, huonyesha vipatanisho vya kisanifu.

Aina za Vitenzi

  1. Vitenzi vikuu – vinaweza kusimama peke yao. Mfano: anacheza.

  2. Vitenzi visaidizi – husaidia kitenzi kikuu. Mfano: alikuwa anacheza.

  3. Vitenzi vishirikishi – vinaonesha uhusiano wa maneno. Mfano:

    • Juma ni mchezaji
    • Mtoto yumo ndani
Aina za Vitenzi Vishirikishi
  1. Vitenzi vya KUWA – alikuwa, hakuwa, ni, si
  2. Vitenzi vya kuwa NA – ana, alikuwa na
  3. Vitenzi vya PO, MO, KO – yupo, yumo, yuko
  4. Vitenzi vya msisitizo NDI – ndiye, siye
  5. Vitenzi vya msisitizo AMBA – ambaye, ambao

VIELEZI

  • Vielezi hufafanua vitenzi, vivumishi auielezi vingine.

Aina za Vielezi

Vielezi vya namna – polepole, kinyumenyume

  1. Vielezi vya mahali – magengeni
  2. Vielezi vya idadi – mara kwa mara
  3. Vielezi vya wakati – juzi
  4. Vielezi vingine – vya kasoro, sababu, hali ya masharti

VIUNGANISHI

  1. Maneno yanayounganisha maneno, virai, vishazi, au sentensi.
  2. Mifano: na, bali, lakini, pamoja na, ama

VIHISISHI

  1. Hueleza hisia au vionjo vya moyo.
  2. Huambatana na alama ya mshangao.
  3. Mifano: Ah!, Oya!, Oh!, Masalale!, Alaa!

Mwalimu

Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.

Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.

Ingia ili kuuliza