Mada za sehemu hiiLugha Na MawasilianoMada 5
Lugha
Lugha ni nini?
Lugha ni mfumo wa sauti za nasibu zenye kubeba maana zilizokubaliwa na jamii ya watu fulani ili zitumike katika mawasiliano.
- Lugha ndio nyenzo kuu ya mawasiliano baina ya binadamu na binadamu.
- Kimsingi lugha hutumia sauti zenye maneno ambayo yamepangiliwa kwa njia maalumu ili kuleta maana iliyo kusudiwa.
- Binadamu hutumia lugha ili kukidhi mahitaji yake ya kila siku, watu hutumia lugha kupashana habari, kubadilisha mawazo.
- Ili mawasiliano yawepo, mpangilio wa maneno huna budi kuleta maana.
- Lugha hutofautiana kulingana na watumiaji.
Mfano:
- Kihaya ni lugha inayotumika na wahaya
- Kibena ni lugha inayotumika na wabena
- Kijerumani ni lugha inayotumika na wajerumani
Maelezo kuhusu lugha na muundo wake
- Lugha hujengwa kwa maneno, na maneno huundwa kwa vitamkwa vilivyopangwa kwa mpangilio maalum.
- Mpangilio huo wa vitamkwa hutoa neno lenye maana.
- Maneno yakipangwa kwa njia maalum, hutoa kauli zenye maana.
- Lugha huwezesha mawasiliano kati ya wazungumzaji kwa kupangwa kuanzia vitamkwa, maneno hadi kauli.
Mfano wa mpangilio wa vitamkwa
- Vitamkwa: chu, ch, k, a, l, u, o
→ Vitamkwa hivi hujenga maneno kama:- chakula
- chuo
Herufi za alfabeti ya Kiswahili
Katika Kiswahili, vitamkwa huwakilishwa na herufi za alfabeti.
Aina za herufi
- Konsonanti (sauti mgumu):
b, c, d, f, g, h, j, k, l, m, n, p, q, r, s, t, v, w, x, y, z - Irabu (sauti nyororo):
a, e, i, o, u
Umuhimu wa vitamkwa na alfabeti katika lugha ya Kiswahili
- Kutokana na herufi hizi, maneno ya Kiswahili hujengwa.
- Hivyo, maneno ndiyo msingi wa lugha na mawasiliano, si kwa Watanzania tu, bali hata kwa mataifa mengine yanayotumia Kiswahili.
Lugha na mawasiliano
- Mawasiliano yasiyotumia sauti si lugha – kwa sababu hayatumi maneno au sauti.
- Mawasiliano ya wanyama au wadudu haiwezi kuitwa lugha, kwa sababu hayatumii maneno ya maana ya kisarufi.
Lugha fasaha
Ni lugha ambayo inafuata taratibu zote za lugha hiyo yaani, kimaana, kimuundo, kimatamshi na kimantiki. Ili mawasiliano yawe mazuri, wazungumzaji watumie lugha fasaha.
- Maana: Ili lugha iwe fasaha katika misingi ya maana au msamiati uliokusudiwa, mfano neno barabara lina maana mbili. Mtu anaweza kukosea badala ya kusema njia akasema sawasawa.
- Muundo: Ufasaha wa lugha hujitokeza kutokana na mpangilio wa maneno kuwa mzuri, mfano: kikubwa kitabu badala ya kitabu kikubwa.
- Matamshi: Sauti za lugha yoyote ile zitamkwe kama zinavyotakiwa ili kujenga ufasaha katika lugha hiyo. Mfano baadhi ya watu hushindwa kutamka baadhi ya maneno, mfano: zambi badala ya dhambi, zarura badala ya dharura.
- Mantiki: Ili maana iliyolengwa iweze kuwepo, kauli lazima ziwe na mantiki, mfano: Nimemkuta hayupo badala ya sijamkuta, chai imeingia nzi badala ya inzi ameingia kwenye chai.
Athari za kutumia lugha isiyofasaha
Lugha isipotumika kwa ufasaha:
- Yaweza kukwamisha mawasiliano
- Lugha hiyo kukosa hadhi na kuonekana kama ya wahuni
Mwalimu
Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.
Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.
Ingia ili kuuliza