Sonzaschool
Rudi

Sekondari ya Juu · Kidato cha Tano

Kiswahili 1

Uandishi wa barua na kadi za mialiko

takriban dakika 10 kusoma

Mada za sehemu hiiUtungajiMada 4
  1. insha
  2. Uandishi wa barua na kadi za mialiko
  3. Uandishi wa kazi za kifasihi
  4. Usimulizi ****

UTUNGAJI WA BARUA

Katika uandishi wa barua, mambo yafuatayo yazingatiwe:

  1. Barua za kirafiki
  2. Barua za kiofisi/kikazi
  3. Barua za simu
  4. Barua za mialiko
  5. Barua za magazeti
  6. Barua za kutoa taarifa
  • Mifano iongezwe katika barua za kikazi na magazeti.
  • Katika barua za mialiko mfano utolewe uonyeshwe.
  • Utungaji wa matangazo mfano utolewe/uonyeshwe.

Hizi ni barua rasmi ambazo huandikwa kwa madhumuni mbalimbali kama vile kuomba kazi, kutuma na kupokea taarifa rasmi, kuomba nafasi ya kusoma, kuomba likizo, kuomba uhamisho.

Mambo ya kuzingatia

  1. Anuani ya mwandishi ambayo hukaa juu upande wa kulia.
  2. Tarehe inayokaa chini ya anuani ya mwandishi.
  3. Anuani moja au zaidi ya mwandishi inayokaa upande wa kushoto baada ya kumbukumbu namba.
  4. Salamu "Ndimi".
  5. Barua yenyewe ufafanuzi wa kusudio la barua.
  6. Mwisho wa barua.
  7. Sahihi ya mwandishi.
  8. Jina la mwandishi (kamili).
  9. Cheo cha mwandishi.

Mfano

MTAA WA MTAKUJA, S.L.P 14631, MAJENGO – MOSHI.

13/11/2012

MENEJA MKUU, KIWANDA CHA MATOFALI, S.L.P 87, MOSHI.

Ndugu,

YAH: OMBI LA KUJA KUJIFUNZA KUFYATUA MATOFALI

Kichwa cha habari hapo juu chahusika. Sisi ni kikundi cha vijana kumi na tano (15) ambao tumeamua kujiarijiri wenyewe kwa kufanya kazi ya kufyatua matofali.

Tunaomba kutembelea kiwanda chako kwa lengo la kujifunza zaidi.

Ni matumaini yetu kwamba ombi letu litakubaliwa.

Wako mtiifu,

…………………..

Vai Selis Chalamila (Katibu wa kikundi)


Mwalimu

Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.

Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.

Ingia ili kuuliza