Mada za sehemu hiiTenzi Na NgonjeraMada 2
- Tenzi
- Ngonjera
Tenzi ni tungo ndefu za ushairi zinazoelezea juu ya jambo fulani na huwa na pande moja, yaani huwa na vina vya kati tu.
Utenzi huweza kuwa maelezo ya wasifu wa mtu fulani, jambo la kihistoria au jambo lolote zito linaloelezwa kwa maelezo marefu. Tenzi huwa na beti nyingi kuliko mashairi na pia hutegemea jambo lenyewe na ufundi wa mtunzi.
- Utenzi una beti nyingi kuliko mashairi.
- Utenzi una upande mmoja, yaani huwa na vina vya kati tu.
- Utenzi una mistari minne, ambapo mistari mitatu ya kwanza huwa na vina vyenye urari sawa, lakini mstari wa mwisho unakuwa na vina tofauti.
Sekunde huanza muda, Kuhesabu siyo shida, Maneno haya shahada, Shika vasikuponyoke. Dakika huenda mbio, Tena bila ya mlio, Sitini hila salin, Saa moja imetimu. Dazani moja ya saa, Na nyingi ongezea, Siku imeshatimia, Milango tunafungua. Siku zikifikia saba, Zenye saa si haba, Na dakika zenye hubar, Wiki tumekamilisha. Wiki nne zikifika, Mwezi umekamilika, Siku zaenda haraka, Mwaka tunachungulia. Miezi kumi na mbili, Yenye wingi wa shughuli, Siku zaenda haraka, Mwaka tunachungulia. Miaka kumi nasifu, Mwongo ulio timilifu, Sibashiri nakwarifu, Muda unasonga mbele. Karne miongo kumi, Aseme yeye na mimi, Tutamke kwa ulimi, Kame miaka mia. Miaka kufika elfu, Milenia timilifu, Karne kumi nasifu, Milenia kufikisha. Tamati nimefikia, Mwisho wa kufurahia, Hakuna wa kufikia, Ila dunia yenyewe.
Kuchambua ni kitendo cha kuichunguza kazi ya fasihi kwa makini, kuihakiki, kuitathmini na kuainisha ubora na udhaifu wake kwa kutumia vigezo vya fani na maudhui.
Maudhui ni jumla ya mawazo yote yanayozungumzwa pamoja na mtazamo wa mwandishi juu ya mawazo hayo. Maudhui hujumuisha mawazo pamoja na mafunzo mbalimbali yanayomsukuma msanii hadi akatunga kazi fulani ya kifasihi.
- Dhamira – Hili ni wazo kuu au mawazo mbalimbali yanayojitokeza katika kazi ya fasihi. Dhamira imegawanyika katika makundi mawili:
- Dhamira kuu
- Dhamira ndogondogo
- Migogoro – Hii ni mivutano na misuguano mbalimbali katika kazi ya fasihi, kama vile migogoro ya kiuchumi, kijamii, kisiasa, na migogoro ya nafsi.
- Ujumbe – Huu ni mafunzo mbalimbali ambayo hupatikana baada ya kuisoma kazi ya fasihi.
- Msimamo – Hii ni hali ya mwandishi kushikilia jambo fulani, hata kama linapingwa na wengi.
- Falsafa – Ni msimamo wa msanii katika maisha juu ya utatuzi wa matatizo katika jamii.
- Mtazamo – Huu ni uelewa wa mwandishi juu ya jambo fulani, kwa mfano, anaweza kulitazama kwa mtazamo wa kidini, kisayansi, n.k.
- Mafunzo – Mawazo ya kuelimisha yanayopatikana katika dhamira mbalimbali za kazi za fasihi.
Swali
Tenzi lina mistari mingapi kwa kila beti?
Ingia ili kuwasilisha jibu lako na lihesabiwe katika umahiri wako.
Ingia ili kufanya mazoeziMwalimu
Umekwama? Niulize chochote kuhusu mada hii.
Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu swali hili.
Ingia ili kuuliza