Sonzaschool
Rudi

Sekondari ya Kawaida · Kidato cha Pili

Kiswahili

Tamathari za semi

takriban dakika 2 kusoma

Mada za sehemu hiiUhakiki Wa Kazi Za Kifasihi SimuliziMada 9

Tamathari za semi

Sitiari

  • Mbinu za kulinganisha vitu pasipo kutumia viunganishi

Mfano:

  • Samaki wangu anaelea kimgongo mgongo (marehemu)
  • Nyumba yangu haina mlango (yai)
  • Mwarabu wangu mkali sana ukimshika hashikiki hana panga, hana shoka, hana kisu, hana mshale (moto)
  • Nyumba yangu ina mlango mdogo

Tabaini

  • Kusisitiza jambo kwa kutumia maneno kinzani

Mfano:

  • Yule anatuona sisi hatumuoni (Mungu)
  • Futi kufunika futi kufunua (nazi fuu, nazi maji)
  • Mkubwa ananiamkia, mdogo haniamkia (kunde kavu na mbichi)

Kejeli na dhihaka

Mfano:

  • Uzi mwembamba umefunga dume kubwa (usingizi)
  • Upara wa mwarabu unafuka moshi (chai, maziwa, ugali)
  • Kitu kidogo kimemtua mfalme kibini (hajandogo)
  • Mama mtu mweusi, watoto wekundu (pilipili)

Tashihisi

Mfano:

  • Popo mbili zavuka mto (macho)
  • Popote niendapo ananifuata (kivuli)
  • Ninapompiga mwanangu watu hucheza (ngoma)

Takriri

Mfano:

  • Huku fungu huku fungu katika bahari (nazi)
  • Mama kazaa mtoto na mtoto kazaa mtoto (kuku na yai)
  • Futi kufutika futi, futi kafutika futi (nazi – kumbi) (nazi na tui) (maji ya nazi)
  • Juu go, chini go katikati gogo (kinywa mdomo na ulimi)

Mbinu nyingine za kisanaa

1. Onomatopea (tanakali sauti)

Mfano:

  • Huku pi na kule pi (mkia wa kondoo atembeapo)
  • Chubwi aingia chubwi katoka (jiwe majini)
  • Pa funua pa funika (nyayo wakati wa kutembea)
  • Enda "parara" (kuti la mnazi)
  • Pakacha tiii! (ugonjwa wa matende)

2. Taswira au picha

  • Katika vitendawili kuna matumizi ya picha za miti, viungo vya mwili, wanyama, vitu.

Mfano:

  • Kuku wangu kataga mibani (nanasi)
  • Mzazi ana miguu bali mzaliwa hana (kuku na yai)
  • Mti mmoja una matawi saba, manne mabichi, pembe mbili, matatu makavu na mkia mmoja (jani lenye wazimu)
  • Wanangu wanne lakini hawakamatani

3. Kinaya

  • Hutumiwa kueleza usemi ambao una maana ya kinyume na usemavyo kijuujuu

Mfano: uzi mwembamba umefunga dume kubwa

4. Ucheshi au vichekesho

  • Kuna vitendawili ambavyo huweza kusababisha ucheshi kwa msomaji. Ucheshi huu hutokana na uhusiano uliopo kati ya kitendawili fulani na maana yake au kile kinachoongelewa nacho.

Mfano:

  • Mwarabu kavaa kilemba
  • Nimemwona bi kizee amejitwika machicha (mvi)
  • Baba apiga mbizi, akiibuka ndevu zimegeuka nyeupe (mwiko)

5. Utata

  • Ni ule ugumu uliopo wa kuamua maana inayokusudiwa au jibu la kitendawili, kuna baadhi ya vitendawili ambazo vina majibu mengi, jibu sahihi au linalokusudiwa hutegemea mazingira, mandhari, utamaduni, wakati n.k.

Mfano:

  • Inachurura inaganda (asali au gundi)
  • Gari la kila mtu (kifo, jeneza, miguu)
  • Hamwogopi mfalme wala bawabu (njaa au shida au kifo)

Mwalimu

Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.

Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.

Ingia ili kuuliza