Sonzaschool
Rudi

Sekondari ya Juu · Kidato cha Tano

Kiswahili 1

Maelezo ya fasihi

takriban dakika 13 kusoma

Mada za sehemu hiiFasihi Kwa UjumlaMada 3

KIELELEZO CHA SANAA

Kila kipengele cha Sanaa kinatofautiana na kingine kwa umbo na matumizi. Fasihi ni kipengele cha sanaa kinachotumia maneno kuumba huo uzuri wa kisanaa

TOFAUTI KATI YA FASIHI NA TANZU ZINGINE ZA SANAA

  1. LUGHA Kazi zote za fasihi zinaundwa kisanaa kwa kutumia lugha inayotamkika na inayoandikika ambayo hubeba ujumbe fulani tofauti na sanaa zingine kama vile.
    • Ufinyanzi hutumia udongo
    • Uchoraji hutumia kalamu, rangi, karatasi au kipande cha nguo.
  2. WAHUSIKA Kazi ya fasihi hulazimika kuwa na wahusika wake ambao matukio mbalimbali yanayohusu jamii inayowazungukia. Hutumika kutoa dhamira ya mwandishi, Pia hutumiwa kuwasilisha tabia za watuwaliomo ndani ya jamii
  3. MANDHARI Fasihi huwa na mandhari ambayo huonyesha tukio linapofanyika. Mandhari inaweza kuwa ya kubuni au ya ukweli.
  4. UTENDAJI Utendaji hujitokeza hasa katika kazi ya fasihi simulizi ambazo hushirikisha hadhira na fanani mahali pamoja na kwa wakati mmoja, Hapa fanani huweza kuonesha matendo katika usimuliaji wake.
  5. FANI NA MAUDHUI Fasihi ina sehemu hizi mbili za fani na maudhui ambazo hutegemeana na hufungamana. Fani ni namna msanii anavyosema kuhusu kile kinachosemwa wakati maudhui ni kile kinachosemwa na msanii.

USANAA WA FASIHI

Usanaa wa fasihi hujitokeza katika vipengele vifuatavyo:

  1. Mtindo Sanaa katika fasihi hujidhihirisha katika namna ya kueleza jambo, Hapa kinachoangaliwa zaidi ni zile mbinu mbalimbali zinazotumiwa na msanii katika kueleza jambo husika. Jambo huweza kuelezwa katika fumbo kwa kupitia; shairi, tamthiliya, hadithi, kitendawili n.k.
  2. Muundo Huu ni mpangilio mzuri wa visa na matukio. Matukio katika kazi za fasihi hupangwa kiufundi ili yaweze kuwasilishwa vizuri kwa hadhira au jamii husika.
  3. Uteuzi mzuri wa "lugha" Iliyojaa vionjo mbalimbali kama vile nahau, misemo, tamathali za semi, taswira na ishara. Lugha inaweza kuchekesha, kukosoa, kukejeli, kubeza, kushawishi n.k
  4. Uundaji mazuri wa "wahusika" Wahusika huumbwa kulingana na nia na lengo la mwandishi kwa hadhira wake.
  5. Ujenzi mzuri wa "Mandhari" Kazi ya fasihi ni lazima iwe kwenye madhari maalum. Mandhari ikijengwa vizuri husaidia sana kujenga hisia inayokusudiwa na mwandishi kwa hadhira wake ili iwezeshe pia kufiksha ujumbe mahsusi uliokusudiwa.

FASIHI NI KIOO

  1. Fasihi ni kioo kwa kuwa fasihi inaweza kufananishwa na kioo.
  2. Kioo katika maisha ya kawaida huweza kumuonesha binadamu mazuri aliyonayo au mapungufu aliyonayo ili aweze kujikubali au kujikataa.
  3. Hivyo fasihi pia ina uwezo wa kuonyesha mazuri au mapungufu yaliyomo ndani ya jamii, aidha kwa jamii au kwa baadhi ya vikundi vilivyomo ndani ya jamii ambavyo huweza kuwa tofauti na mahitaji ya jamii nzima.

Udhaifu

  1. Udhaifu unaojitokeza katika fasihi hii ni kwamba fasihi ina uwezo wa kuonesha mambo kama ni mabaya au mazuri lakini haina uwezo wa kuonesha njia ya kutatua matatizo hayo kama kilivyo kioo.
  2. Udhaifu wa fasili ya fasihi ni hisi.
  3. Je ni mara ngapi mwanafasihi ataguswa ndipo aweze kuandika kazi ya fasihi?
  4. Je ni mwandishi pekee ndiye anayetakiwa kuguswa?
  5. Ukweli ni kwamba sio kazi zote zinazoandikwa zinatokana na mguso unaompata mwandishi.

FASIHI NI MWAMVULI

  1. Fasili ya fasihi ni mwamvuli ilifananishwa na mwamvuli kwa jinsi inavyoweza kumhifadhi binadamu kwa jua au mvua.
  2. Lakini nadharia halisi ya fasili kufananishwa na mwamvuli ni katika uelekeo wa kwamba fasihi inauwezo wa kulinda amali za jamii zisipotee na zisiweze kurithishwa kutoka kizazi kimoja hadi kizazi kingine.

Udhaifu

  1. Fasili hii ilionesha udhaifu wa fasihi kutokuwa na uwezo wa kulinda amali za jamii yaani mila na desturi zilizopotea.
  2. Hii ni kwa sababu mila na desturi ndani ya jamii huwa zinaenda na wakati na hubadilika kulingana na mahitaji ya wakati huo.

FASIHI NI HISI

Dhana hii ilikuwa na maana kwamba kazi ya fasihi inapoletwa mtoaji/msanii ni lazima awe anaguswa na jambo fulani na ndipo aweze kuandika kazi hiyo.

FASIHI NI KIELELEZO CHA KISANAA

Fasihi inatazamwa kama ni ubunifu au ufundi wa aina fulani unaojidhihirisha katika maandishi.

Udhaifu

  1. Fasili hii huzingatia zaidi utoaji wa burudani tu.
  2. Haizungumzii lolote juu ya uelimshaji wa nini kifanyike juu ya tatizo alilolionesha msanii.

FASIHI

  1. Fasihi ni sanaa inayotumia lugha ambayo msanii huitumia ili kuweza kufikisha ujumbe kwa hadhira iliyokusudiwa.
  2. Fasihi huwa ina umbo timillifu. Mfano: kazi ya fasihi inaweza kuwa tamthiliya (igizo), hadithi au ushairi.
  3. Uhai wa lugha katika kazi ya fasihi inaongeza mvuto.
  4. Lugha inaweza kupewa uhai huo kwa kutumia tamathali za semi kama vile tashibiha, tasfida, sitiari, kejeli, dhihaka, balagha, kijembe n.k.
  5. Vipengele vingine vinavyotawala ufasihi ni:
    • Uundaji wa wahusika
    • Matumizi ya picha
    • Mandhari
    • Utendaji n.k.

Mfano: Mtoto aloumbika, mara mtoto laini Shingo yake ya birika, watabasamu moyoni Kweli asali tamu, wajua ilivyoundwa Hapa unaweza kupata ujumbe kwa kupitia maswali mbalimbali.

  1. Mhusika ameumbwaje?
  2. Shingo yake inafananishwa na nini
  3. Uzuri wa mototo umeoneshwaje?
  4. Asli imetumika kwa sababu gani?
  5. Swali lililo kwenye mstari wa mwisho limeulizwa kwa sababu gani?

Mwalimu

Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.

Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.

Ingia ili kuuliza