Mada za sehemu hiiKuonesha Uelewa Wa Jambo Ulilolisikiliza Au KulisomaMada 2
- Kusikiliza na Kuonesha Uelewa wa jambo Alilosikilia
- Kusoma kwa Ufasaha na Kuonesha Uelewa Wa matini Aliyosoma
UJUMBE KATIKA HADITHI Hadithi ya chui mla watu Hapo kale katika kijiji cha Isamila kulikuwa na chui mla watu. Chui huyo alivizia watoto walipokwenda kuchota maji kisimani na kumkamata mmoja na kumla. Mara nyingine aliua wazee kwa kuwa alijua hawana nguvu. Siku moja watu walikuwa shambani wanalima na kupanda mahindi: baadhi ya watoto wao walikuwa wanachunga ndama na mbuzi karibu na shamba. Wale watoto wakaanza kuwatania wale wazazi wao kwa kuita chui huyooo! Tuokoeni twafaa! Tuokoeni twafaa! Wazazi wao walipoenda na majembe yao hawakukuta chui, wakarudi kuendelea kulima, wakarudia tena. Mamaaaa! Chui mkali mamaa twafaa! Huku mtoto mmoja akilia kama chui, mara wazazi wao wakaenda tena, wakakuta hakuna chui, wakachukia sana na kuwaonya wasirudie tena mchezo huo. Mara kelele za wale watoto zikamfikia chui, chui akanusa harufu ya mbuzi na watu. Akaanza kufuatilia taratibu akapate kitoweo. Ghafla yule chui akamkamata mtoto mmoja, wale wengine wakapanda juu ya mti wakaanza kuita wa ukweli kamkamata katope tusaidiem, tusaidieni. Wale wazazi wakadhani ni mzaha tu, hawakuwajali. Wakaimba tena Anamla mkono Anamla tumbo Anamla macho Anamla katope Baba mzazi wa katope akaenda mbio baada ya kusikia jina la mwanae. Alipofika akamkuta chui kashiba amelala akampiga na mshale akamuua. Hadithi hii ina ujumbe ufuatao Mzaha mzaha mwisho hutunga usaha Asiyesikia la mkuu huvunjika guu Mchumajanga hula na wa kwao Mtoto akililia wembe mpe Kueleza maana ya ujumbe huo katika methali hizo Methali: Kuvuja kwa pakacha nafuu ya mchukuzi Maana: Pakacha ni kikapu kinachosukwa na makuti ya mnazi, iwapo pakacha litavuja, uzito wa mzigo utapungua. Mtu akisusa jambo, kuna wengine ambao watafaidika kwa kususia kwake. Ujumbe: Tusisuse jambo ambalo sisi ndio wanufaikaji. Kwa kufanya hivyo tutakuwa tumewarahisishia kazi wale waliotakiwa kututekelezea jambo hilo. Kusoma habari na kubaini ujumbe uliopo
Juzi tulimsikia nesi wa wilaya akitutahadharisha juu ya ugonjwa wa malaria. Nesi Eliza alitoa ujumbe kuwa malaria ni ugonjwa hatari unaoua kimyakimya. Wenyewe hauumizi kama UKIMWI, wala hauna fujo kama kipindupindu. Nesi Eliza alisema ugonjwa huu unaenezwa na mbujike wanaotuuma karibu kila siku majumbani na popote pale, mbu hao huwa na vijidudu vya ugonjwa wa malaria. Tunawezaje kujikinga na malaria? Bibi mmoja aliuliza na mara nesi akajibu, tuue mazalia yote, tufyeke vichaka karibu na nyumba, tukaushe madimbwi vote na kunyunyizia dawa. Mwisho inatupasa tulale kwenye vyandarua vyenye dawa, tupige dawa ndam wakati wajioni na wagonjwa wapelekwe hospitalini mapema ili wakatibiwe.
Kusoma mashairi na kubaini ujumbe
Muwa ni zao tamu, muwa huu wa pori Sukari hutosha hamu, utamu hutia mori Tukajilamba kwa zamu: kwa utamu wa korikori Sukari ni punje tamu, madhara yake kinywani Sukari kuweka chai: inanoga kwelikweli Utavutiwa na chai, kwavyo sukari halalai Daima twapenda chai, kwa sukari hii ghali Daima twapenda chai, kwa sukari hii ghali Sukari ni punje tamu, madhara yake kinywani Sipendi hii sukari, kinywani hii hatari Yaozesha meno sukari, yanukisha hatari Taugua kisukari, kwa kupenda sukari Sukari ni punje tamu, madhara yake kinywani Kubaini ujumbe uliomo katika shairi hili Ubeti wa kwanza una ujumbe wa muwa ni zao tamu Ubeti wa pili una ujumbe wa kuwa sukari inanoga sana Ubeti wa tatu umesema sukari inaozesha meno Mwisho shairi lote linataja sukari Mstari wa mwisho wa kila ubeti unasema sukari inaathiri kinywani
Kiimbo hutokea katika mazungumzo huonesha kupanda na kushuka kwa sauti unapozungumza Swali huonesha sauti ya juu Unatoka wapi? Umekula nini? Unalala wapi wewe? Unakwenda wapi? Maelezo kuhusu sauti ya kawaida Nimekula ugali na samaki Samahani, sijaelewa swali Amri huonesha hali ya ukali na sauti ya mkato Tokahapa! Njoo hapa! Nendakwenu! Mwehuwewe! Kuandika aina ya kiimbo katika sentesi hizi Sentensi Kiimbo wewe ni mtu wa namna gani? Sauti ya juu Nimekula wali na maharage sauti ya kawaida Toka hapa! sauti ya ukali Kha! Wewe! Ruka hapa! sauti va ukali na va mkato Sijala ugali sauti va kawaida
Kusikiliza maelekezo ya uelekeo wa pande nne za dunia na kuyatekeleza Dira huelekeza pande kuu nne za dunia ambazo ni mchoro Kaskazini Kusini Magharibi Mashariki Ukiwa Dar es Salaam, upande wa Mashariki kuna bahari ya Hindi Ukiwa Dar es Salaam, Arusha ipo kaskazini mwa Tanzania Ukiwa Dar es Salaam, Kigoma ipo upande wa Magharibi mwa Tanzania Kusoma kwa ufasaha na kuonesha uelewa wa matini aliyoisoma
Mwalimu
Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.
Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.
Ingia ili kuuliza