Sonzaschool
Rudi

Msingi · Darasa la Nne

Kiswahili

Kusikiliza na Kuonesha Uelewa wa jambo Alilosikilia

takriban dakika 1 kusoma

Mada za sehemu hiiKuonesha Uelewa Wa Jambo Ulilolisikiliza Au KulisomaMada 2
  1. Kusikiliza na Kuonesha Uelewa wa jambo Alilosikilia
  2. Kusoma kwa Ufasaha na Kuonesha Uelewa Wa matini Aliyosoma

Kusikiliza na kuonesha uelewa wa maneno mbalimbali

1. Vitendawili

Kusikiliza na kutegua vitendawili

  1. Kitendawili: Popoo mbili zavuka mto Jibu: Macho

  2. Kitendawili: Naapa hivi sitarudi tena kwa mjomba Jibu: Majani

  3. Kitendawili: Shamba langu kubwa lakini navunia kiganjani tu Jibu: Ndevu

  4. Kitendawili: Tega nikutege Jibu: Mwiba

  5. Kitendawili: Kila ninakoenda hunifuata Jibu: Kivuli

  6. Kitendawili: Babu kajenga nyumba lakini haina mlango Jibu: Yai

  7. Kitendawili: Kaa kule nami nikae huku turushe mawe pangoni Jibu: Kula ugali

  8. Kitendawili: Babu kalala ndani lakini kasahau ndevu nje Jibu: Mhindi

  9. Kitendawili: Kuku wetu hutagia miibani Jibu: Nanasi

  10. Kitendawili: Kulia kwake ni kicheko kwetu Jibu: Mvua

2. Nahau

Kueleza maana ya nahau zifuatazo

  1. Nahau: Kujikaza kisabuni Maana: kutia bidii

  2. Nahau: Kula bata Maana: Kula raha

  3. Nahau: Kuwa macho Maana: Kuwa mwangalifu

  4. Nahau: Sinahali Maana: Ni fukara

  5. Nahau: Kufa kishujaa Maana: Kufa lava kupigania haki

  6. Nahau: Piga kithembe Maana: Kushindwa kutamka maneno

  7. Nahau: Piga mbiu Maana: Toa tangazo kwa maneno

  8. Nahau: Unga mkono Maana: Kukubaliana jambo

Mwalimu

Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.

Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.

Ingia ili kuuliza