Mada za sehemu hiiUhakiki Wa Kazi Za Fasihi AndishiMada 2
- Kuongeza msamiati.
- Kukua na kuenea kwa lugha
Maneno
-
Kwa kawaida hakuna lugha inayojitosheleza kimawasiliano na kimantiki, hivyo hakuna lugha iliyo bora kuliko nyingine.
-
Ili lugha itosheleze mawasiliano inahitaji kuwa na msamiati wa kutosha.
-
Msamiati ndio unaowawezesha wazungumzaji wa lugha kujieleza na kubainisha hisia zao kwa wale wanaowasikiliza.
-
Ili kukamilisha mawasiliano, lugha inajikuta ikilazimika kuongeza msamiati wake.
-
Sababu kuu zinazopelekea idadi ya msamiati kuongezeka ni pamoja na:
-
Muingiliano wa kiutamaduni baina ya jamii moja na nyingine
- Mfano: utamaduni wa Waingereza umesababisha lugha ya Kiswahili kuwa na maneno yafuatayo: gauni, shati n.k
-
Maendeleo ya sayansi na teknolojia yamesababisha uvumbuzi wa dhana mbalimbali mpya
- Mfano: kabla ya uvumbuzi wa simu, televisheni n.k, maneno haya hayakuwepo
-
Jamii kutokana na matukio (misimu) mbalimbali huibua dhana mpya ambazo lugha hulazimika kuzitafutia msamiati
- Mfano: maneno mengi katika lugha ambayo yanaonesha uhusiano wa kijamii, kama kasheshe, changudoa n.k
-
Njia za kuongeza msamiati
Ubadilishaji wa vitamkwa
-
Lugha hubadilisha mpangilio wa fonimu/vitamkwa ili kuunda maneno tofauti.
-
Mfano wa vitamkwa: a, e, i, o, u vinaweza kuunda maneno yafuatayo:
- au, ua, ita, tai, uta, tua, tia, ute, utu, toi, tui, toa n.k
Unyumbulishaji wa maneno
- Lugha hunyambulisha maneno yake kuunda maneno mengi tofauti.
- Mfano: piga, pigo, pigana, piganiana, piganisha, pigishwa, pigeni n.k
Ukopaji wa maneno
- Lugha huchukua maneno kutoka lugha nyingine na kuyatumia kama yalivyo.
- Mfano wa maneno ya Kiswahili yaliyokopwa:
| LUGHA | MANENO |
|---|---|
| Kireno | Leso, meza n.k |
| Kijerumani | Shule, ela n.k |
| Kiingereza | Shati, gauni, skuli |
| Kiarabu | Sujudu, amini n.k |
| Kifaransa | Sabuni, divai |
| Kichina | Umma |
| Kihindi | Chapati, khanga, doti, manjumati n.k |
Kutohoa maneno
- Lugha hutumia maneno kutoka lugha nyingine kwa namna tofauti kimatamshi na kimaana.
- Mfano:
| LUGHA | NENO |
|---|---|
| Kiingereza | (mail) → meli |
| Kipare | kitivo |
| Kihaya | ngeli |
| Kinyakyusa | ugiligili (liquid) |
Ubatizaji wa maana
- Maneno yaliyopo hupewa maana mpya.
- Mfano: Mashabiki wa chama au mchezo huitwa wakereketwa
Uunganishaji wa maneno
-
Lugha huunganisha maneno tofauti kuunda neno jipya.
-
Mfano:
- Nomino + Nomino: Kuchwa + maji = kuchwamaji
- Kitenzi + Nomino: Funga + mlango = fungamlango, Ponda + mali = pondamali
- Kitenzi + Kitenzi: Kufa + Kwaja = kufakwaja
-
Hakuna ajuaye chimbuko la Kiswahili kwa uhakika.
-
Kuna nadharia mbalimbali zinazoelezea chimbuko la lugha:
- Lugha hutokana na tabia za kuiga.
- Binadamu wa kale waliiga sauti za wanyama, wadudu na mazingira.
- Sauti hizo zikazua lugha, na Kiswahili kuwa mojawapo ya lugha.
Kuna mitazamo tofauti kuhusu maana ya Mswahili:
-
- Mzaliwa wa pwani ya Afrika Mashariki
- Mtu yeyote anayezungumza Kiswahili
- Mtu mwenye asili ya Kiafrika
- Mtu mjanja, azungumzaye sana pia mwongo
Pijini
- Lugha inayozuka kutokana na mwingiliano wa lugha mbili tofauti.
- Inasemekana Kiswahili kilitokana na Kihārabu + lugha za kienyeji Afrika Mashariki.
Udhaifu
- Haielezei lugha za kienyeji zilizokuwepo kabla ya Waarabu kuja.
Kreoli
- Kreoli ni Pijini iliyokomaa kuwa lugha mama ya vizalia.
Udhaifu
- Haielezei muundo wa Kiswahili kwa kina – mfano vitenzi, sarufi, matamshi.
Kiswahili ni Kiarabu
Inasema Kiswahili ni Kiarabu kwa sababu:
-
- 41% ya msamiati wa Kiswahili ni wa Kiarabu
- Kuna mfungamano wa kiutamaduni kati ya Waswahili na Waarabu
- Neno Swahili linatokana na Sahel (pwani)
Udhaifu
- Lugha nyingi hukopa maneno – si hoja kuwa ni lugha hiyo.
- Mwingiliano wa kiutamaduni haubadilishi asili.
- Jina la kigeni si hoja ya kubadilisha utaifa au asili.
- Watetezi wengi wa nadharia hii ni wageni.
Kiswahili ni Kibantu
Nadharia hii inazingatia:
-
- Muundo wa lugha (vitenzi, majina, sintaksia, matamshi, msamiati)
- Historia ya wenyeji wa pwani, utamaduni na mwingiliano wa watu
Mfano wa hoja za kiisimu:
Msamiati:
| LUGHA | MANENO |
|---|---|
| Kiswahili | maji |
| Kibena | lulenga |
| Kihaya | amaiz |
| Kinyakyusa | amaisi |
Kisintaksia:
| LUGHA | SENTENSI |
|---|---|
| Kiswahili | Mtoto analia sana |
| Kipare | Mwana eiya muno |
| Kibena | Mwana ivemba sana |
| Kimeru | Mwanaakeiya muno |
| Kihaya | Omwana nalila muno |
| Kijita | Omwana kalila muno |
| Kinyakyusa | Mwana akulila fijo |
| Kichaga | Mana nekefila mno |
Muundo wa kitenzi:
- Hali yakinishi huishia na -a: soma, piga, pita
- Vitenzi vya Kibantu hunyambulika: pigana, piganiwa, pigwa
- Huundwa majina kutoka vitenzi: soma → somo
Ngeli za majina:
- Mtoto – Watoto
- Mti – Miti
Utafiti wa Profesa Melcom Guthrie:
- Aligundua mizizi 22,000 ya maneno inayopatikana katika lugha zote za Kibantu.
-
Kiswahili kilikuwepo kabla ya ujio wa wageni.
-
Hoja hutegemea ushahidi wa kihistoria kutoka:
- Asili ya Wabantu kusini mwa Cameroon (karne ya 5)
- Kusambaa kwao hadi Afrika Mashariki, visiwani, na kusini
- Kundi la Wabantu walilopitia maeneo ya Shungwaya na baadaye kuhamia kusini mwa mto Tana
Mfano wa ushahidi:
-
Ibn Batuta (1331 BC):
- "Nilisafiri kutoka Mombasa mwendo wa siku mbili... tulipofika Mafya, tuliwakuta wenyeji wakiwa hawana chakula, wanatoa nafaka uswahilini."
Mwalimu
Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.
Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.
Ingia ili kuuliza