Mada za sehemu hiiShairiMada 2
- Maana ya shairi
- Muundo wa shairi
Muundo wa Shairi
Shairi huundwa na vitu vifuatavyo:
Beti/Ubeti
Hiki ni kifungu kimoja cha shairi au aya ya shairi ambayo ina uzani sawa.
Vina
Hizi ni silabi zenye sauti zinazofanana. Vina kwenye shairi huwa kati au mwisho wa sentensi.
Mfano: Karudi baba mmoja: toka safari ya mbali Kavimba yote mapaja na kutetemeka mwili Watoto wake wakaja, ili kumtaka hali Wakataka na kauli: iwafae maishani
Vina vya kati ni: ja Vina vya mwisho ni: li
Mizani
Ni idadi zilizo sawa za silabi katika mstari kutoka ubeti hadi ubeti.
Mfano: Karudibabammoja, tokasafari ya mbali (mizani 8 kwa kila sehemu) Mstari mzima mizani 16
Mshororo
Huu ni mstari mmoja wa maneno katika shairi.
Kituo/Kibwagizo
Huu ni mstari wa mwisho wa ubeti. Kuna aina tatu za vituo:
- Kituo Bahari — Huu ni mstari unaotoka mwanzo hadi mwisho bila kubadilika katika kila ubeti.
- Kituo Kimalizio — Ni kituo ambacho mstari wa mwisho maneno yake hubadilika ubeti hadi ubeti.
- Kituo Nusu Bahari — Ni mstari wa mwisho ambao maneno yake nusu hubadilika na nusu hubaki kama yalivyo.
Shairi lina sifa zifuatazo:
- Huwa na lugha teule.
- Hayazingatii kanuni za kisarufi.
- Hutumia lugha maalum ya kisanaa.
Mwalimu
Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.
Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.
Ingia ili kuuliza