Mada za sehemu hiiUfahamuMada 2
- Ufahamu wa kusoma
- Matumizi ya kamusi
Ufahamu ni hali ya kujua jambo na kuweza kulifafanua au kutoa taarifa zinazohusiana na habari hiyo. Hutokana na kusoma, kusikiliza, na kutafakari.
Dhimaya ufahamu
- Husaidia kuokoa muda kwa kutoa taarifa kwa muhtasari.
- Hubadilisha tabia ya mtu baada ya kugundua mambo mazuri na mabaya.
- Humsaidia msomaji kutafakari kwa kina.
- Huongeza ujuzi, maarifa na burudani kwa msomaji.
Aina za ufahamu
-
Ufahamu wa Kusikiliza
- Kutokana na kusikiliza na kuelewa taarifa.
-
Ufahamu wa Kusoma
- Kutokana na kusoma na kuelewa maana ya maneno, sentensi, na habari.
Ufahamu wa Kusikiliza ni ule unaotokana na kusikiliza taarifa. Mambo muhimu ya kuzingatia:
- Kuwa makini kwa kile kinachosimuliwa.
- Kujua matamshi sahihi ya lugha.
- Kuhusisha mambo muhimu na habari inayosimuliwa.
- Kubainisha mawazo makuu.
Ufahamu wa Kusoma hutokana na kusoma na kuelewa maana ya maneno na sentensi. Msomaji anahitaji:
- Kubuni mawazo makuu.
- Kutambua maana ya maneno na misemo.
- Kujibu maswali yatokanayo na habari aliyosoma.
Aina za kusoma:
-
Kusoma kwa Sauti
- Kutamka maneno kwa sahihi na kuelewa maudhui.
-
Kusoma Kimya
- Kusoma kwa haraka ili kupata ujumbe wa jumla bila umakini mkubwa.
-
Kusoma kwa Makini
- Kusoma kwa undani na kutafakari maneno na sentensi kwa umakini.
Baada ya kusoma, ufahamu unaweza kupimwa kwa maswali:
- Kubaini mawazo makuu.
- Maana ya maneno na misemo: Kuelewa matumizi sahihi ya maneno katika muktadha.
Mfano wa maneno magumu:
- Kufilisika - Hali ya mashirika kushindwa kuzalisha mali.
- Ruzuku - Fedha zitolewazo serikalini kusaidia mashirika.
Kufupisha Habari ni kitendo cha kubaini mawazo makuu na kuunganisha habari kwa kutumia maneno ya mwenyewe, huku ukihakikisha maana inabaki sawa.
Hatua za kufupisha habari:
- Kusoma habari yote na kuielewa.
- Kuchagua taarifa maalumu na maneno muhimu.
- Kuandika muktasari kwa usahihi.
- Kulinganisha usawa wa ufupisho na habari ya asili.
- Kuandika kichwa cha habari kisichozidi maneno matano.
Mwalimu
Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.
Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.
Ingia ili kuuliza