Mada za sehemu hiiUandishi Wa Insha Na BaruaMada 3
- Kuandika insha za wasifu za kisanaa na zisizo za kisanaa
- Kuandika barua ya kirafiki
- Ubainishaji wa Tanzu za fasihi simulizi.
Fasihi simulizi hujitokeza katika tanzu kuu nne, ambazo ni hadithi, semi, ushairi, na maigizo. Tanzania hizi zinaweza kuonyeshwa katika mchoro ufuatao:

Ni tungo za fasihi simulizi zitumiazo lugha ya ujazo na maongezi ya kila siku. Masimulizi huwa ni mafupi yaliyopangwa katika mtiririko unaokamilisha visa.
Vipera vya hadithi
- Ngano
- Tarihi
- Vigano
- Soga
Ngano
Hizi ni hadithi zitumiazo wahusika kama wanyama, miti na watu kuelezea au kuonya.
Tarihi
Ni hadithi ambazo husimulia kuhusu matukio ya kihistoria, matukio hayo yanaweza kuwa ya kweli au ya kubuni.
Vigano
Ni hadithi fupi zinazoelezea makosa au uovu wa watu fulani na kueleza maadili yanayofaa. Vigano hutumia methali kama msingi wa maadili yake.
Soga
Ni hadithi fupi za kuchekesha na kukejeli. Wahusika wa soga ni watu wa kubuni. Soga husema ukweli unaohimiza lakini ukweli huo hujenga vichekesho ili kupunguza makali.
Ushairi katika fasihi simulizi ni fungu linalojumuisha tungo zote zenye kutumia mapigo ya sauti kwa utaratibu maalumu.
Vipera vya ushairi
- Mashairi
- Utenzi
- Nyimbo
- Ngonjera
Mashairi
Ni tungo zenye mpangilio maalumu wa silabi na lugha ya mkato.
Utenzi
Ni tungo ndefu ya kimasimulizi au kimawaidha utenzi kutofautiana na ushauri kwa kuwa na mistari mifupimifupi isiyozidi mizani.
Nyimbo
Ni tungo zenye mpangilio maalumu wa maneno na mahadhi yaani hupenda kuimbwa na kuambatana na ala za muziki au sanaa.
Ngonjera
Zina muundo wa mashahiri ya kimapokeo na huwa katika muundo wa mazungumzo baina ya watu wawili au makundi ya watu wanaolumbana na mwishowe kufikia mwafaka au suluhisho.
Ni tungo za fasihi simulizi ambazo ni fupi na zenye kutumia lugha ya picha.
Vipera vya semi
- Methali
- Mafumbo
- Nahau
- Vitendawili
Methali
Ni misemo ambayo hutoa hekima na busara kwa kuundwa kwa mpangilio wa pande mbili za fikra.
Mfano:
- Kidole kimoja hakivunji chawa
- Haba na haba hujaza kibaba
Mafumbo
Ni kauli zinazoeleza maana waziwazi na kutumia maficho.
Mfano:
- Hakamataki hashikiki (moshi)
- Uzalendo umemshina (umeshindwa kuvumilia)
Vitendawili
Ni usemi uliofumbwa hutolewa kwa hadhira, ufumbuliwe, kitendawili kufanya kazi ya kumfikisha msikilizaji.
Mfano:
- Uzi mwembamba umefunga dume (usingizi)
Nahau
Ni kauli zilizojengwa kwa picha kwa kutumia maneno ya kawaida lakini zinatoa maana isiyo ya kawaida.
Mfano:
- Amepata jiko (ameoa)
- Ana mkono mrefu (mwizi)
- Ana mkono wa birika (mchoyo)
- Amevaa miwani (amelewa)
Ni masimulizi yenye utendaji ambayo huonesha mambo yaliyotokea, yatakayotokea lengo ni kufikisha ujumbe.
Vipera vyake ni:
- Michezo ya kuigiza
- Majigambo
- Ngonjera
- Vichekesho
Michezo ya kuigiza
Ni maigizo marafu ya visa vinavyowakilisha maisha ya jamii fulani. Michezo mingine huafiki na mingine hulaani mambo yasiyofaa, michezo ya watoto wadogo pia huwasaidia kujifunza maadili ya jamii hiyo.
Majigambo
Ni maigizo ya kujitapa au kujigamba kutokana na kuweza kufanya jambo la kishujaa au lisilo la kawaida. Mtambaji husimulia na kutenda akionyesha jinsi alivyofanya jambo lile.
Mfano:
- Askari aliyerudi vitani, mtu aliyemuua simba n.k
Ngonjera
Ni maigizo ya kutumia mashairi, huwa kuna pande mbili unapinga na unaelewa jambo na mwisho kufikia muafaka.
Vichekesho
Ni maigizo mafupi ya kufurahisha hadhira.
Mfano:
- Mizengwe
- Original komedi
- Vituko show
Kazi ya fasihi lazima iwe na fani na maudhui, vipengele hivi ni sura za falsafa moja si rahisi kuzitenganisha fani iko ndani ya maudhui.
Fani
Ni umbo la nje la kazi ya fasihi.
Maudhui
Ni jambo analosema muandishi katika kazi yake ya fasihi.
Vipengele vya Fani
- Matumizi ya lugha
- Mtindo
- Muundo
- Mandhari au mazingira
- Wahusika
- Jina la kitabu
Matumizi ya lugha
Msanii hutoa lugha kwa mpangilio maalumu wa maneno, tamathali za semi hutumiwa kwa upekee kulingana na mahitaji ya kazi hiyo.
Mtindo
Hii ni tabia ya pekee mtunzi katika simulizi au uandishi mtindo kutofautiana hali ya mtunzi na mtunzi.
Mandhari
Ni sura ya mahali mazingira ambapo kazi ya fasihi husika.
Wahusika
Ni watu, miti au viumbe hai vinavyowakilisha watendaji katika kuonyesha sifa za ndani na nje.
Vipengele vya Maudhui
Kuna vipengee (5) vya maudhui navyo ni:
- Dhamira
- Ujumbe
- Falsafa
- Migogoro
- Mafunzo
Dhamira
Ni lengo la mtunzi wa kazi za fasihi. Mtunzi anaweza kutoa dhamira kuu na kujenga dhamira ndogo ndogo dhamira huweza kukosoa.
Ujumbe
Ni funzo analotoa mtunzi katika kazi ya fasihi kulingana na dhamira alizotoa.
Falsafa
Ni mawazo makuu ya mtunzi kuhusu maisha. Ni imani ya maandishi kuhusu maisha.
Migogoro
Ni hali ya kutoelewa baina ya pande mbili au zaidi.
Mafunzo
Ni mafunzo makuu ya mtunzi kuhusu maisha. Wakati mwingine hadhira inaweza kupata mafunzo mabaya au mazuri kwa wahusika wakazi hiyo.
Maana
Uhakiki ni kazi au kitendo cha kuchambua na kufafanua kazi ya fasihi ili kuweza kupata maadili na ujumbe uliomo katika kazi ya fasihi.
Au
Uhakiki ni sayansi maalum ya kuchambua kazi ya sanaa kwa undani na kuona ubora wa kazi ya fasihi kwa kutumia vipengele vya fani na maudhui na kuangalia uwiano na uhusiano wake na jamii.
Umuhimu wa Uhakiki wa Kazi za Fasihi Simulizi
- Kuchambua na kuweka wazi fumbo ambalo litapatikana na kazi ya fasihi.
- Kuchambua na kufafanua picha za kisanii zilizotumika katika kazi ya fasihi.
- Kumshauri mwandishi ili afanye kazi bora.
- Kumuelekeza msomaji ili apate faida zaidi kuliko yale ambayo angeweza kuyapata bila diraya muhakikiki (mhakiki ni mwalimu wa jamii)
- Kuhimiza na kushirikisha fikra za kihakiki katika kazi za fasihi.
- Kukuza kiwango cha utunzi na usomaji.
- Kutafuta na kuweka sawa nadharia ya vitabu teule.
Kufafanua Vigezo vya Uhakiki wa Kazi za Fasihi Simulizi
- Ukweli wa mambo yanayoelezwa.
- Uhalisikaji wa watu, mazingira na matukio katika jamii.
- Umuhimu wa kazi ya fasihi kwa jamii inayohusika lazima ufikiriwe.
Uhakiki wa Kazi za Fasihi Simulizi katika Fani
- Wahusika
- Mandhari
- Mtindo
- Maudhui
- Ujumbe
Mwalimu
Unasoma somo hili? Niulize nikuelezee chochote kilichomo.
Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu mada hii.
Ingia ili kuuliza