Mada za sehemu hiiLugha Ya PichaMada 3
- Vitendawili
- Methali
- Nahau
Nahau ni semi fupi zinazotumia maneno ya kawaida lakini hutoa maana tofauti na ile ya moja kwa moja. Zina undani wa maana ambao unaweza kueleweka tu kwa watu wanaofahamu muktadha wa lugha.
Mfano wa nahau na maana zake
- Ana mkono mrefu – Mwizi
- Ana inda – Ana wivu
- Ametutupa mkono – Amefariki
Nahau katika sentensi
1. Ilikuwa ni safari ya hatari lakini tulifika bila matatizo.
Salama salimini
2. Maendeleo ya mazao yangu sasa yananipa faraja.
Tia moyo
3. Boti ilizama taratibu mwishowe ikazama vote.
Zama
4. Dereva wa basi alijitahidi kwa kila njia gari lisianguke.
Fanya juu chini
-
Baba aliugua sana lakini kwa sasa afya yake ni nzuri sana.
Buheri wa afya -
Hili banda lilikaribia sana kuangushwa na upepo.
Nusurika
Maana za nahau zifuatazo
- Ahadi ni deni – Timiza ahadi yako.
- Amevaa miwani – Amelewa pombe (chakari).
- Chemsha bongo – Fikiri kwa makini.
- Kuchungulia kaburi – Kunusurika kifo.
- Fyata mkia – Nyamaza kwa hofu au aibu.
- Hawapikiki chungu kimoja – Hawapatani kamwe.
- Kumvika kilemba cha ukoka – Kumsifu mtu kwa unafiki.
- Kula mlungula – Kula rushwa.
- Mezea mate – Kutamani.
- Vunjika moyo – Kata tamaa.
- Meza maneno – Kutunza siri moyoni.
- Kalia kitako – Kumsengenya mtu.
- Paka mafuta kwa mgongo wa chupa – Kumsengenya mtu.
- Mangimeza – Kiongozi anayependa kuamrisha watu.
- Sina hali – Sijiwezi.
Swali
Ni nini maana ya nahau «Ana inda»?
Ingia ili kuwasilisha jibu lako na lihesabiwe katika umahiri wako.
Ingia ili kufanya mazoeziMwalimu
Umekwama? Niulize chochote kuhusu mada hii.
Ingia ili kumuuliza Mwalimu wa AI wa Sonza kuhusu swali hili.
Ingia ili kuuliza